WALI
WA MCHELE NA TUI LA KARANGA
MAHITAJI : Mchele
: Tui
la Karanga
: Chumvi
: Maji
Utayarishaji na
mapishi
Ø
Chagua
Mchele
Ø
Loweka
unga wa Karanga kwa maji safi
ya vuguvugu kwa dakika 10
Ø
Kamua
tui kwa kutumia maji ya vuguvugu hii inasaidia kutoa tui na lenye mafuta mengi
Ø
Weki
tui jikoni linapokaribia kuchemka punguza tui zito la juu na hifadhi vizuri.
Ø
Ongeza
mchele, koroga, usifunike. Pika hadi maji yabakie kidogo, halafu funika
Ø
Ongeza
tui ulilopunguza (tui zito). Punguza moto kabisa ivisha taratibu ukishakaukia
geuza
Ø
Palia
kwa dakika 10-15 wali utakuwa tayari
MATUMUZI:-
Kula
pamoja na nyama au samaki au maharage na mboga za majani na matunda
¬
Machicha
ya karanga yanayoaaaabakia yanaweza kutumika kuungia mboga ya majani au
maharage.*
Imeandaliwa na Edgar Kajolo Kapagi Mbeya
MOBILE: 0754 807401 –
0788 029500
2: UJI WA KIMEA
MAHITAJI:- Unga wa nafaka ya mahindi au mtama au ulezi
iliyooteshwa, kukaushwa
na kusagwa.
: Sukari
: Maji
: Chumvi
Utayarishaji na
mapishi.
- Pima unga wa kawaida wa mahindi au mtama
- Pika uji mzito mpaka uive kabisa
- Epua, pooza kidogo
- Ongeza unga wa kimea kiasi cha kijiko kimoja au zaidi kulingana na kiasi cha uji uliopika, endelea kukoroga mpaka uji ulainike.
- Rudisha tena uji jikonoi chemsha kwa muda ongeza sukari au chumvi
- Epua
Matumizi.
Mlishe mtoto kwa kutumia kijiko na kikombe
au sahani au bakuli. Pia unaweza kutumika kama
kifungua kinywa kwa watoto wa shule na Familia.
Kumbuka : unaweza
kuongeza karanga au maharage au mboga za majani au unga wa Soya au yai au
maziwa kuongeza ubora wa uji unga wa kimea
unasaidia kulainisha uji wa mtoto na kumfanya anywe kiasi kikubwa kumwezesha
kupata viini lishe vya nguvu kwa wingi.
Imeandaliwa na Edgar Kajolo Kapagi Mbeya
MOBILE: 0754 807401 –
0788 029500