Mboga za maboga zinatokana na mmea wa maboga. Mboga za maboga
huliwa sana na wanyakyusa na wasafwa mkoani Mbeya. Watu wengi wanakula bila
kujua faida zake kiafya. Waingereza huita pumpkin leaves.Mboga za maboga zina
virutubisho vifuatavyo vitamin A, C, E, B6, calcium, Thiamine, Riboflavin,
Niacin, Chuma, Protini, Shaba, Potassium, Magnesium, Phosphorus, manganizi,
Nyuzi Lishe na Folic acid.
Mboga za maboga huzuia/ hutibu kifafa kwa kuchanganya majani
mateke ya mboga za maboga, maji ya nazi na chumvi kidogo. Na hupewa mgonjwa
ale, hupunguza lehemu mwilini, majani ya maboga yana hypoglycaemic kwa wingi
yanafaa kuliwa na wanaosumbuliwa na kisukari, Huimarisha afya ya macho, majani
ya maboga yana Anti – oxidants kwa wingi yakiliwa hupunguza kuzeeka mapema,
majani ya maboga yana nyuzi lishe kwa wingi, vitamin na madini kwa hiyo huzuia
uwezekano wa kupata saratani, mboga za maboga huongeza spermatogenesis kwa
wingi kwa hiyo hufaa kwa wenye matatizo ya
kutokupata watoto (Infertility), mboga za maboga zina vitamin C kwa
wingi hufaa kwa kuimarisha ngozi ya mwili na kutibu vidonda na kuimarisha
mifupa, mboga za maboga zinafaa sana kwa mama wanaonyonyesha kwa kuwa zinaongeza
kiwango cha maziwa, mboga za maboga huzuia maambukizi ya Bakteria mwilini
zikiliwa mara kwa mara, Huongeza kinga ya mwili, Huongeza protini mwilini,
mboga za maboga zina nyuzi lishe kwa wingi zikiliwa vizuri na kumfanya mtumiaji
kwenda haja vizuri na ni nzuri kwa wenye matatizo ya Anemia.
Pika majani ya mboga za maboga, mafuta ya Alizeti au
mzeituni, chumvi kidogo na kitunguu saumu. Pika kwa dakika kumi. Kitunguu saumu
weka baada ya kuiva (mwishoni).
Kula mara kwa mara. Wenye kisukari wasiweke chumvi
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
PikA Kwa dakika 5 sio 10
ReplyDeleteAsante kwa elimu. Ktk tiba hii ya kifafa hayo majani yanapikwa au yanachanganywa vipi! Na tiba inafanyika kwa mda gani
ReplyDeleteTunashukuru elimu ni nzuri
ReplyDeleteTunashukuru kwa elimu hii nzuri
ReplyDeleteMboga naipenda Sana hii
ReplyDeleteMboga naipenda Sana hii
ReplyDeleteWallah mmenikosha kweli kweli
ReplyDeleteAssente sana kwa kufaidika kwa majani ya maboga
ReplyDeleteAsante kwa elimu ya lishe
ReplyDelete