Kwa maoni yangu, mhindi ni mmea wenye utaratibu wa
kuvutia. Kuanzia majani yake hadi kwenye mbegu zilizo kwenye hindi lenyewe ,
kila kitu kimepangwa kwa mpangilio hususa wenye kupendeza. Isitoshe, mmea huu unapokua “unazungumza”
nawe. Unakuambia ikiwa una kiu au hauna lishe ya kutosha. Kwa kawaida mtoto wa kibinadamu hulia
anapohitaji kitu. Kama tu mimea mingine,
mhindi hutoa ishara zinazoonekana, kama vile kubadili rangi na umbo la majani
yake, ili kueleza mahitaji yake.
Unahitaji kuelewa ishara hizo.
Huenda majani yenye rangi nyekundu na Zambarau yakaonyesha kwamba mhindi
hauna Fosfati.
Dalili nyingine zinaweza kuonyesha ukosefu wa magnesi, nitrojeni, au
potashi. Pia anapoungalia Mkulima anaweza kutambua ikiwa mhindi wake una
ugonjwa au umeathiriwa na kemikali.
Mhindi ulianza kukuzwa huko.
Amerika , huenda katika nchi ya Mexico, na kuenea ulimwenguni pote. Waperu walioishi kabla ya enzi ya wainka
waliabudu Mungu wa kike wa mahindi aliyepambwa kwa taji lililotengenezwa kwa
bunzi za mhindi. Bunzi hizo zilitokea kichwani mwake kama nyaya katika
gurudumu.Wakaaji wa ulaya waligundua mhindi mnamo mwaka 1492 baada ya mvumbuzi
Christopher Columbus kuwasili katika visiwa vya karibea.
Kuna
aina nyingi za mahindi zinazogawanya katika vikundi sita vikuu:
dent,flint,Flour,sweet,waxy, na popcorn.
Mahindi aina ya sweet hayakuzwi sana kama aina nyingine. Utamu
unaopatikana katika aina hii ya mahindi unatokana na kasoro Fulani ambayo
huizuia kubadili kiasi cha kutosha cha sukari kuwa wanga. Zaidi ya asilimia 60 ya mahindi inayouzwa
ulimwenguni hutumiwa kulisha mifugo huku asilimia 20 hivi ikilisha
wanadamu. Asilimia iliyobaki
hutumiwa viwandani au kama mbegu. Jina la kibotaniahuitwa ZEA MAYS. Huko India
huita CORN (Makai) na Amerika (India corn) haya mahindi ni ya njano mengine ya
kawaida na mengine ya Bisi (Popcorn) haya ndiyo nitaelezea umuhimu wake kwa
afya zetu.
Haya mahindi ya njano ya
kitumiwa vizuri yanapunguza kuongezeka uzito (weight gain), mahindi haya yana
magnesium kwa wingi yanayosaidia kuyaweka matumbo yetu yawe vizuri (wonderful
bowel regulator), yanasaidia kujenga mifupa na misuli. Yana phosphorus kwa wingi inayosaidia kujenga
ubongo vizuri na mfumo wa fahamu,Yana madini ya zinki yanayosaidia kuimarisha
nguvu za uzazi ukiongeza kikombe kimoja cha unga wa njano kwenye mlo unakua na
2mg za madini ya zinki, kupunguza lehemu kwenye damu (blood cholesterol
levels), pia yanamadini ya chuma yanayosaidia kuongeza nguvu mwilini na kinga
ya mwili kwa kuzisaidia seli nyeupe za damu ili kupambana na maradhi,
yanavitamini “A” nyingi ambayo inatoa kinga dhidi ya magonjwa. Inazuia upofu
kwa watoto, inaimarisha misuli ya macho kwa wazee, yana nyuzinyuzi (fiber)
ambayo inazuia kisukari na unene,
kuondoa chunusi usoni nk, kuku wa kisasa wakilishwa mahindi ya njano
kiini cha yai kinabadilika toka weupe na kuwa njano, hata kwa upande wa bisi husafisha meno,
kuimarisha nguvu za uzazi, kupunguza sukari mwilini, kusafisha damu,hata watu
wengine na waathirika wa UKIMWI wazitumie kuboresha afya.Mhindi una kitu kimoja
kinaitwa ndevu za mahindi zina faida kubwa kwa binadamu zina Potassium nyingi
ambazo zinasaidia kutibu magonjwa yafuatayo kwa wanaokojoa kitandani, maumivu
ya tezi dume (prostate), maumivu ya mfumo wa mkojo (UTI) , mawe kwenye figo,
moyo kutokufanya kazi yake vizuri(Congestive heart failure), kisukari
ukichanganya na Drum stick,uchovu, BP (HBP), kupunguza lehemu (Cholesterd), nk.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
Habari mkuu, nnahitaj mbegu za mahindi ya njano(bisi) ntayapataje? Niko Arusha
ReplyDeleteHabari ndugu na Mimi pia nahitaji mbegu ya mahindi ya njano kwa maana ya bisi nipo Rukwa sumbawanga na maelekezo ya sehemu ambayo yanaweza kupandwa joto au baridi
DeleteHabari Mkuu naomba nijue Mahindi ya njano nayapata wapi ? Hata mbengu
ReplyDeleteUpon maeneo gani naweza kukusaidia kupata mbegu na mahind
DeleteInaponya high blood pressure kabisaa??
ReplyDeleteArticle Nzuri sana mkuu. Naweza pata mbegu za mahindi ya njano nipo dar es salaam.
ReplyDeleteUjatueleza zaidi hizo ndevu za nahindi unazitumiaje ?
ReplyDeleteNashukuru Kwa elimu yako.
ReplyDelete