MAFENESI
au Jackfruits kwa lugha ya kiingereza na majina mengine Langka na Nangka ni
matamu kwa ladha yake. Lakini pia yana umuhimu katika mwili wa binadamu.
Hakuna
anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yake ni katika misitu
ya mvua nyingi ya Magharibi ya ghats (western ghats).
Lakini
kwa sasa inalimwa katika nchi za india, Burma, Sri lanka, China, Malaya, East
in indies, Qeens land, Maturities, Hawaii, Suriname, Brazil, Kenya, Uganda na
Tanzania,
Na
nchini Tanzania hulimwa Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na
Mbeya(Kyela) nk.
Na
sehemu zinazotumika ni majani, matunda, utomvu, mizizi na magamba. Na mfenesi
unaweza kukua hadi kufikia kimo cha mita 20.
Mafenesi
yana vitamin B1 na B2, vitamin C, flavonoids na ni chanzo kizuri cha
carotenoids na Potassium nk. Katika nchi kama Thailand majani machanga na maua
machanga ya kiume hupikwa kama mboga. Matunda yaliyoiva hulimwa yakiwa mabichi
au yakiwa yamepikwa na nazi au hutengeneza ice cream, chatine(chutney), jam, jeli,
(jelly) na pesti.
Mfenesi
una faida nyingi tukianzia na majani hutibu homa magonjwa ya ngozi majipu, vidonda na kisukari.
Tunda lina wingi wa vitamin C ambayo kiafya inasaidia kuongeza kinga ya mwili,
tunda hili linasaidia kupunguza mafua, kifua na homa. Vitamin C hiyo husaidia
kuondoa sumu mwilini na kuukinga mwili na maradhi pale linapotumiwa ipasavyo.
Fenesi
pia linasaidia kuupa mwili nguvu kwani lina madini ya wanga na sukari ambayo
husaidia kuupa mwili nguvu kwa haraka. Fenesi linaweza kuondoa sumu mwilini
hivyo linakinga na saratani za aina mbalimbali kama ile ya mapafu. Mdomo na
kinywa na tumbo. Fenesi hutia nguvu
mwili na kwenda haja vizuri. Kwa wale wenye matatizo ya shinikizo la damu,
Fenesi ni tiba nzuri kwani ina madini ya potassium ambayo husaidia kwa namna
moja au nyingine kupunguza uwezekano wa kupata
shinikizo la damu na kukuondoa katika hatari ya kupata kiharusi. Mizizi
yake hutibu homa, kuharisha, magonjwa ya ngozi
na asthma. Utomvu wake ukichanganywa na siki hutibu tambazi (abscesses),
kuumwa na nyoka na uvimbe wa tezi (glandular) nk. Magamba yake hutibu vidonda
kwa kuweka kibandiko (poultices)
Mbegu
zake zikikaangwa huongeza tendo la kujamiiana.
Watanzania
tuanze kula fenesi baada ya kula husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula kwa
sababu ni tunda muhimu na linasaidia pia kuzuiwa kuvimbiwa. Pia kwa wenye
matatizo ya macho na kutokuona vyema, tunda hili ni mkombozi mkubwa kwani lina wingi wa vitamin C ambayo huongeza
kiwango cha kuona (uoni), pia lina uwezo wa kuondoa sumu, hufanya kazi katika
retina na kuifanya iwe imara.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya
ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali
ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali
wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi
(Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa
hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,
vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine
mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
Asante Sana kwa elimu Na kutufariji kwa namna moja ama nyingine Asante Sana
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu hiyo ya kilimo cha mafenesi. Binafsi napenda kujua wapi nitapata mbegu za mafenesi yenye kuzalisha matunda bora.
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu hiyo ya kilimo cha mafenesi. Binafsi napenda kujua wapi nitapata mbegu za mafenesi yenye kuzalisha matunda bora.
ReplyDeleteHakika watu huangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6) Mungu ameumba kila aina ya tunda kama dawa ila wanadamu kwa kupuuza tunapatwa na magonjwa. Asanteni kwa uchanganuzi went. Barikiwa na BWANA.
ReplyDeleteHakika watu huangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6).
ReplyDeleteShukrani nlikua nauliza inaweza kutibu athritis
ReplyDelete