Dengu ni chanzo kizuri cha vitamin muhimu kama vile riboflavian ( vit B2), niacin ( vit B3), thiamin ( vit B1), Folate na vitamin A (B-Carotene) kama ilivyo mikunde mingine Dengu ina sababu za kuondoa virutubisho visivyofaa ( anti – nutritional factors) kutokana na mbinu mbalimbali za mapishi Dengu zina faida kadhaa kiafya na muunganiko wake na mikunde na nafaka nyingine unaweza kuwa na athari nzuri kwa magonjwa ya binadamu kama vile kisukari aina ya pili ( type 2 diabetes) magonjwa ya mmeng’enyo wa chakula, na baadhi ya saratani, kuondoa udhaifu wa mwili, uchovu na mengineyo, homa, magonjwa ya mfumo wa kupumua na kukojoa, abscesses, husaidia upungufu wa damu mwilini, hurekebisha lehemu ( cholesterol) na mengineyo.
Kwa wale wenye kusumbuliwa na matatizo ya nguvu za uzazi na hawana matatizo ya mzunguko wa damu watumie mara kwa mara, mfumo wa neva , mfumo wa mkojo, homoni na kemikali na utendaji wa viungo vingine ni vizuri wakatumia Dengu mara kwa mara. Wananchi wa nchi za Asia kama India , China ,Japan , Indonesia na nyingine zinatumia sana Dengu, soya, nk. Nchi hizi zina watu wengi duniani kuliko hata ukubwa wa nchi zao. Na utumiaji wa Dengu mara kwa mara kwa watu wenye kisukari hurekebisha kiwango cha sukari kwenye insulin. Watanzania wote tuanze kutumia Dengu mara kwa mara ili kuimarisha nguvu za uzazi kwani sasa hivi vijana wengi wanalalamika kuwa hawana nguvu za uzazi .
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
Thanks for ur education
ReplyDeleteGood lesson give us more
ReplyDeleteGood idea
ReplyDelete