I
Karafuu
ni tumba lililokauka la maua yasiyofunguka yanayopatikana kutoka mti mzuri wa
kati na kijani. Mti huu una shina lilinyooka na hukua kufikia kimo cha mita 10
hadi 12.
Karafuu
imekuwa ikitumiwa India na Uchina kwa zaidi ya kwa zaidi ya miaka 2000 kama
kiungo cha kulinda kuoza meno na kutoa harufu mbaya yaaani pumzi mbaya.
Mti
wa karafuu una asili ya visiwa vya Molluca. Wachina walipata kiungo hiki mnamo
karne ya 3 K.K (Kabla ya Kuzaliwa Kristo).
Karafuu
ziliingizwa Alexandria mapema mwaka 176 B.K (Baada ya Kuzaliwa Kristo). Mnamo
karne ya 4 hivi B.K ulijulikana vema katika meditarrania na katika karne ya 8
ulaya nzima.
Inasemekana
huko visiwa vya pemba na unguja (Zanzibar) karafuu ililetwa na sultani mmoja
ikiwa imewekwa kwenye fimbo ya mwanzi leo hii Zanzibar ndio mzalishaji
anayeongoza kwa kuzalisha karafuu nyingi ulimwenguni.
Sifa
ilizonazo karafuu ni wanga (carbohydrates), Protini, mafuta (Volatile oil),
nyuzinyuzi (crude fibre), jivu la hydrochloric acid, calcium, phosphorus, iron,
sodium, Potassium, thiamine (Vit B1), Riboflavin (Vit B2), Niacin (Vitamin B3),
vitamin A na C.
Mafuta
hupatikana kwenye vitumba vya karafuu, kikonyo na majani.
Karafuu
hutibu magonjwa mengi kama kutuliza maumivu ya meno, kutoa gesi tumboni,
kuchafuliwa moyo, kuyeyusha chakula tumboni, kuimarisha viungo vya kiume (Sex
Stimulant), kuimarisha mzunguko wa damu mwilini, kuzuia kutapika, kipindupindu,
kikohozi, Asthma, Masikio, maumivu ya Misuli (Muscular Cramps), kuumwa kichwa,
styes (an inflammation around the eyelash).
Matumizi
mengine ya karafuu huchanganywa kwenye curry powder, pilipili, mdalasini,
binzari na viungo vingine. Wahindi hutumia kuongeza ladha kwenye betel quid
(pan pati). Mafuta ya Karafuu pia hutumika katika viwanda ya perfume, sabuni,
ni kuongeza ladha kwenye madawa n.k
Tunashauri
kila familia kuzingatia matumizi ya karafuu ili kulinda afya zetu.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Matatizo ya
meno, Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi
tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni
pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi
wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo
ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka
moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na
mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mnapatikana wapi kwa hapa Dar es salaam
ReplyDelete