)
Maajabu ya Mmea wa Rumex
(Sorrel) Usambarensis katika kutibu mkanda wa Jeshi Msemwasemwa (Kinyakyusa),
Kchambo (Wapare. Rumex (Sorrel)
Usambarensis- Botanic ni mimea inayoota kwa mtindo wa vichaka vichaka inayopatikana
katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Njombe, Ruvuma, Iringa na Kilimanjaro n.k mmea
huu umeonekana kuwa na faida kubwa sana kwa afya ya binadamu na wanyama, kwa
vile hutibu maradhi mbalimbali.
Tafiti mbalimbali
zilizowahi kufanyika nchini Tanzania na Kenya
zinaonyesha umuhimu wa mmea huu kutibu magonjwa mbalimbali kwa mfano majani
hutibu kikohozi na maumivu ya tumbo.
Mizizi yake na vikonyo
vichanga hutumika kutibu kikohozi cha kawaida na Nimonia(Pneumonia), vidonda na
majipu.
Pia mizizi yake ikitumiwa
na mimea mingine ni dawa ya baadhi ya minyoo inayosumbua sana watu. Pia wazee
wa zamani wal;itumia mmea mzima kwa kutibu ndui (Small Pox) kwa kuwaogesha
wagonjwa.
Mazingira Natural
Products ya Mbeya tumefanya utafiti wa mmea huu ukichanganywa na mimea mingine
kama Black Nightshade n.k hutibu vizuri sana mkanda wa Jeshi (Herper Zoster’s)
wa aina zote. Na ukitumiwa vizuri huimarisha kinga ya mwili kwa mtumiaji.
Lakini mmea huu hauishii
hapo kwa wale wafugaji wa kuku hapa Mbeya wale wanaotumia watakubali bila
shaka yoyote ile kuwa mmea huu unafaa
sana kuwalisha kuku hasa wale wanaotaga mayai hufanya kiini kuwa cha njano sana
na kupunguza matatizo ya kuku kudonoana
ovyo.
Hili ni muhimu kwa
mwananchi yeyote wa Tanzaniania kulifanyia kazi kwa kupanda na kutumia katika
mazingira yake.
Imeandaliwa na Mtafiti Dr.
Edgar Kajolo Kapagi
Mazingira
Natural Products
Mbeya
Simu;
0754 807401, 0719 564276
Barua pepe: mnp.kaka@gmail.com