DRACAENA
USAMBARENSIS
(Tetesyeri,
Tsheleli-Kisafwa, Msigandi, Mukwanga-Wadigo, Mtetemu-Wamwera)
Dracaena,
Usambarensis au Tetesyeri, Tsheleli-kisafwa ni mti unaopatikana katika mikoa ya
Mbeya, Iringa, Rukwa, Ruvuma na Tanga(Lushoto) nk.
Mti
huu umeonekana kuwa na faida kubwa sana kwa afya ya binadamu kwa vile hutibu
maradhi mbalimbali. Mti huu umekuwa ukitumiwa na mababu zetu toka siku nyingi. Mti huu hutumika hata kwenye
matambiko mbalimbali kwa mfano kukiwa na uhaba wa mvua wazee wa kisafwa hutumia
kutambikia na uhaba wa mvua unatoweka na hata kama yatatokea maradhi ya ajabu
ajabu. Pia miti yake hupandwa kuzunguka zizi la ng’ombe kuzuia watu
wabaya(wachawi) ili wasiharibu mifugo na watu wengine hupanda majumbani mwao
kama maua. Pia watu wengine hutumia majani
yake kumuoshea mtu anayesadikiwa amerogwa. Majani yake hutumika kutoa kondo la
nyuma kwa mwanamke aliyetoka kujifungua. Pia majani yake ni dawa ya degedege
kwa watoto. Mizizi yake hutibu maumivu ya tumbo hasa linaloandamana na kisonono.
Pia mizizi hutumika kwa maumivu ya kifua . Hili ni muhimu kwa kila Mtanzania
kulifanyia utafiti zaidi kwani watu wengi wamepanda hasa wenye nyumba za kisasa
hata baadhi ya makanisa hutumia kupamba wakati wa sherehe mbali mbali kama
maua. Pia mti huu unatunza mazingira
kwenye vyanzo vya maji. Napenda watanzania wenzangu waujue huu mti manufaa yake
kwa jamii.
Dr
Edgar Kajolo Kapagi.
Mazingira Natural Product Mbeya
Simu namba: 0754807401
Email: mnp.kaka@gmail.comaa
No comments:
Post a Comment