CENTELLA ASIATICA au Gotu
Kola, Indian Pennywort, Marsh Penny ni mmea unaoota kwa kutambaa. Na huota sehemu
zilizo na unyevu mwingi na kwenye kingo za mito. Mmea huu umekuwa ukitumika sana
huko mashariki ya mbali India, China, Japan, Indonesia na nchi za Amerika. Hapa
nchini Tanzania ni watu wachache sana wanaotumia, na hii inatokana na watu
wengi kutoufahamu kazi yake japo wanauona wanapokuwa kwenye shughuli zao
nyingine. Mmea huu una virutubisho vingi vinavyoweza kumsaidia binadamu
kuboresha afya yake. Watu wengi wakifikia umri wa miaka 50 na kuendelea kumbukumbu
zao kichwani huanza kupungua. Mmea huu ukitumiwa vizuri utaimarisha kumbukumbu
zetu vizuri. Mmea huu hauishii hapo tu unatibu na magonjwa mengine kama
kisukari huko India, China, Japan, Indonesia n.k hutumia sana. Magonjwa ya
kuharisha damu kwa watoto katika hatua za mwanzo na matatizo ya tumbo kwa
watoto. Matatizo ya tumbo kwa watoto huchanganywa na majani ya Fenugreek (Methi
kwa kihindi). Ni mmea mzuri kwa mfumo wa neva (Nervous Disorders). Ni mmea
mzuri kwa watu wenye matende (elephantiasis) juisi yake hupakwa sehemu
zilizoathirika.
Pia ni mmea mzuri sana ukichanganywa na mmea wa Trichodesma Indicum kutibu utasa
kwa wanawake (Female Sterility) Hapa ni vizuri tukaelewana kuwa mwanamke asiwe
na matatizo ya hedhi (Menstrual Pain) kutoka uchafu sehemu za siri (Usaha),
uzito mkubwa sana n.k kama ana matatizo haya atibu kwanza. Pia hutibu magonjwa
ya ngozi na vidonda vinavyotokana na kaswende. (Syphilitic Sores).
Pia majani yake huko
India hutumika kutengeneza supu, Chatne, Chai, Juisi na kuchanganya kwenye
chapati.
Tahadhari: Inashauriwa kutumia juisi kidogo ya mmea huu kwa
sababu ina nguvu sana.
Kwa kuwa huu mmea unaweza
kupanda kwenye bustani au kwenye makopo ya kupandia maua tunashauri kila
familia ipande ili kuboresha afya.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya
ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali
ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali
wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi
(Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa
hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,
vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine
mengi ambayo si ahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.