Pages

Wednesday, November 6, 2013

ROSELLE (HIBISCUS SABDARIFFA)



.

Mmea wenye faida nyingi kwa binadamu

 Mmea huu asili yake ni nchi ya Sudan, sasa unapatikana katika maeneo yote ya tropiki. Bara la Asia unapatikana nchi za India, Korea, China n.k. Afrika magharibi unapatikana nchi za Mali, Burkina faso, Senegal na Ivory Coast na Afrika Kaskazini. Afrika mashariki kenya, Uganda na Tanzania. Katika Tanzania hulimwa katika mikoa ya Dodoma na Ruvuma, Mbeya ndio wameanza kuchangamkia kulima. Mkoani Dodoma hutumia maua yake kutengeneza juisi na pombe ya kienyeji (Choya) na mvinyo. Roselle hutumika kama chai ya kuburudisha na chai yake ina nguvu ya kuongeza mkojo na huleta kuongezeka kwa utoaji wa nyongo na jasho.
Roselle ina vitamin C, D, B-1, B-2, Chuma (Irion), Phosphorus, Calcium. Magnesium, Omega -3, Beta-Carotene na Amino Acid 18 zilizo muhimu kwa mwili wa binadamu kama lysine na agrinine.
Maua ya Roselle hutumika kuongeza damu (HB), kuimarisha mifupa( Prevents Osteoporosis), kuimarisha utendaji wa Ubongo ( antioxidant for brain), Kuimarisha afya ya ngozi (preserve the skin smooth and reduce wrinkles), kuimarisha utendaji wa utumbo (increased intestinal peristaltic), kupunguza shinikizo la damu( anti hypertension). Kuzuia magonjwa ya figo na moyo (inhibit kidney damage, diabetes, coronary heart diseases and growth of cancer for anti oxidant content is very high).
Majani hutumika kwa kikohozi, matatizo ya figo, kupunguza shinikizo la damu na kuimarisha utendaji wa utumbo. Mbegu zake nazo zina faida nyingi kiafya, mizizi na majani yake pia hutumika kutibu magamba ya miguuni (cracks in the feet), majipu na vidonda vilivyooza na kuvifanya vipone haraka pia ukitengeneza losheni ya majani hutibu vidonda.
Mizizi yake hutumika kuongeza hamu ya chakula. Katika majaribio ya Roselle ulionyesha tendo la kuchelewesha ukuaji wa bacteria za kifua kikuu, kwa hiyo kunywa chai hii mara kwa mara kwa tiba yoyote uliyopewa ya kifua kikuu.
Ni vema kila familia kupanda katika maeneo yetu ili kuboresha afya zetu.
Pia tunatibu Taifodi (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Hyper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda, Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo na kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi n.k
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

1 comment: