Kwanini
tunahitaji maji mwilini.?
Je
tunahitaji maji kiasi gani.?
Haya ni
maswali ambayo kila binadamu anapaswa kujiuliza, kwasababu haina maana yeyote
kama tunakunywa maji kila wakati,lakini tusijue faida yake mwilini.
Maji ni
muhimu kwa makuzi na ulinzi wa miili yetu kwa kuwa yana kazi nyingi za mchakato
wa kibaolojia mwilini.
Maji ni
sehemu muhimu ya mlo wowote wa binadamu na hata wanyama.Ndio maana mtu yeyote akishakula
lazima atatafuta maji ya kunywa. Katika
mwili wa mtu mzima, asilimia kati ya 50 hadi 70 ya uzito wake ni majimaji, na
bila maji muda wa uhai wa mwili unakuwa hatarini katika kipindi cha saa au siku
chache.
Watu wengi
hawanywi maji ya kutosha kwa siku, na matokeo yake ni kukaukiwa maji mwilini,
na kusababisha madhara mengine kama ya kuumwa kichwa, uchovu na kushindwa kuwa
makini.Mchakato wote wa lishe hauwezi kufantika vizuri bila ya maji. Maji ni
muhimu sana mwilini kwani: Hurekebisha joto la mwili, Husaidia katika
uyeyushaji wa chakula
Kukauka maji
kwa muda mrefu mwilini kunaweza kuchangia matatizo kadhaa ya kiafya kama vile
kutoenda haja kubwa na ugonjwa wa figo.
Je unahitaji
maji kiasi gani.?
Kwanza ni muhimu
kuanza kunywa maji angalau glasi moja tu mara unapoamka asubuhi.
Pili jiwekee
birika la maji mezani kwako, iwapo upo kazini, ili iwe rahisi kwako kunywa maji
kila unapohitaji wakati wa kazi.
Kama upo
katika mahangaiko wakati wote wa mchana, ni vyema ukabeba chupa ya maji, ili
uweze kunywa maji wakati wote utakapojisikia kiu.
Ongeza kiwango
chako cha ulaji matunda na mboga, kwani mboga na matunda yana kiwango kikubwa
cha maji na faida nyingine kadhaa za kiafya.
Mwili wa
binadamu na wanyama hupata maji yake kwa njia kuu tatu. Kwanza kunywa maji
yenyewe kama kinywaji au kwakunywa viburudisho vingine kama vile soda. Maji pia
yapo katika vyakula vigumu tunavyokula.
Yapo pia
maji yanayotengenezwa katika mwili ikiwa ni matokeo ya mmeng’enyo wa kikemikali
ndani ya mwili.
Mtu mzima
kwa wastani anatakiwa kunywa angalau lita 2.5 za maji kwa siku, kati ya kiasi
hiki, 1.8 lazima ipatikane kwenye vinywaji halisi, ikiwa na maana ya glasi 6 au
7 hivi kwa siku.
Unywaji huu
unatakiwa kuongezwa wakati wa majira ya joto au baada ya kufanya kazi
iliohitaji nguvu ili kurejesha uwiano wa maji katika mwili.kunywa maji
yasiyochanganywa na chochote,bado ndio njia madhubuti ya kurejesha maji
yanayopotea kutoka mwilini.
Maji ni
mojawapo ya zawadi ya pekee ambayo mungu alitupatia. Karibia magonjwa yote
yanayomsibu mwanadamu yanatibika kwa kuyatumia maji tu. Unapotumia Tiba ya maji
unaepukana na kuumwa ugonjwa wa kichwa, presha, upungufu wa damu, kupooza,
mapigo ya kasi ya moyo na kuzimia,kikohozi,pumu,kifua kikuu,kiungulia,kuharisha
damu, bawasiri,kisukari,,matatizo ya macho,matatizo ya pua,masikio na koo.
Baada ya
kuamka asubuhi mapema, kabla ya kupiga mswaki na kunawa uso, kunywa bilauri nne
za maji, usile wala kunywa chochote mpaka dakika 45. Baada ya kunywa bilauri za
maji ndipo upige mswaki na kunawa uso. Usinywe maji pale umalizapo kula chakula
cha asubuhi, cha mchana au cha usiku
hadi baada ya saa moja au saa mbili zipite epuka kwenda kulala mara tu baada ya
kumaliza kula chakula.
Kwa wagonjwa
waliodhaifu inashauriwa waanze mpango huu kwa wakunywa bilauri moja au mbili na
polepole waongeze idadi hata kufikia bilauri nne. Shinikizo la damu kunywa
mwezi mmoja, matatizo ya gesi siku kumi, kufunga choo miezi sita, kisukari
mwezi mmoja, kifua kikuu miezi mitatu, saratani miezi sita, Tumia maji salama
kila wakati.
No comments:
Post a Comment