Pages

Thursday, July 10, 2025

E KUKU WAKO WANASUMBULIWA NA MAGONJWA MATANO FAHAMU YANAYOSUMBUA ZAIDI

JE KUKU WAKO WANASUMBULIWA NA MAGONJWA MATANO

FAHAMU YANAYOSUMBUA ZAIDI

1.    Coccidiosis  (koksidiasis)

DALILI

A.  Kinyesi cha Damu au kilichochanganyika na damu au chenye rangi ya kutu (redish brown)

B.   Kushusha mabawa chini/ kuvaa koti na kuzubaa

C.   Kupungua uzito kudhoofika na baadae kufa

DAWA

ESB3, AMPROLIUM

Kuzuia ugonjwa hakikisha banda ni safi pia safisha banda ni safi pia safisha vyombo vya chakula na maji mara kwa mara (kila siku)

INFECTIOUS CORYZA (MAFUA MAKALI)

DALILI

       i.            Kuvimba uso na macho

    ii.            Kukosa hamu ya kula

 iii.            Kupumua kwas shida na kutoka ute wenye harufu mbaya puani

 iv.            Kukohoa, kudhoofika na hatimaye vifo

DAWA

1.    OXYTETRACYCLINE (OTC,) Tylodox, trimazin na tylosin.

3.FOWL TYPHOID (TAIFODI YA KUKU)

DALILI

a)    Uharo wa njano au mweupe au mchanganyiko wa mweupe na njano  (huu haugandi sehemu ya haja kubwa)

b)   Kukosa hamu ya kula na kutochangamka.

c)    Vifo ndani ya muda mfupi tangu dalili kujitokeza

DAWA

TRIMA FARM , ESB3 na TRIMAZINI

4. BACILLARY WHITE DIARRHEA (UHARO MWEUPE)

Huathiri zaidi vifaranga wenye umri chini ya wiki tatu 3 ingawa Wakubwa pia wanaweza kuugua

DALILI

a)    Uharo mweupe mzito unaoganda  na kuziba sehemu ya haja kubwa

b)   Kukosa hamu ya kula

c)    Kupumua kwa shida

d)   Vif vya ghafla  au polepole kwa vifaranga

DAWA

 TRISULMYCIN, SULFAD na TRIMAFARM

Angalizo safisha sehemu ya haja kubwa kwa maji ya uvugu vugu  yaliyochanganywa na dawa ya kuua vijidudu (disinfectant) kwa taratibu sana.

FOWL POX (Ndui ya kuku )

Ndui ya Kuku Inaathiri kuku wa rika  zote  lakini huathiri zaidi vifaranga

DALILI

Vidonda vikavu mithili ya vipele au mabonge yenye rangi ya kahawia (brown) kwenye ngozi yaliyo wazi kama machoni na kwenye Upanga Mashavu (WATTLES)

DRY POX (NDUI KAVU)

Kuhema kwa shida, wakati mwingine kuacha mdomo wazi na kukoroma au kupumua kwa tabu kukosa hamu ya kula au kushindwa kula kabisa na vifo kwa vifaranga.

TIBA

UGONJWA HUSABABISHWA NA VIRUSI VYA KUKU WACHANJE

Hakuna dawa ya kutibu wape vitamin kuimarisha kinga na OTC (antibiotics) na kutibu magonjwa nyemelezi

 

  

No comments:

Post a Comment