Pages

Tuesday, December 17, 2013

ARTEMISIA ARFA KIBOKO YA MALARIA



Familia; Compositae
Jamii za porini za Artemisia hustawi katika hali ya hewa ya joto dunia nzima. Artemisia arfa ni ya asili na imekuwa ikitumiwa miaka mingi iliyopita na watu kwa kutibu homa na magonjwa mengine. Huko nchini China na Vietnam wanatumia Artemisia annua ya mbegu mbili tofauti iliyotokana na mimea ya asili ya huko ya Artemisia. Na Artemisia annua ndiyo inayotumika kutengeneza dawa mseto ya malaria hapa Tanzania. Artemisia arfa inastawi katika maeneo ya tropiki, hutoa majani kwa wingi, na majani haya yana Arteminisin kwa wingi, kitu ambacho kinafaa sana kutibu malaria, mmea huu hukua hadi kufikia urefu wa mita 3 lakini haustahimili theluji. Hapa nchini Tanzania Artemisia arfa huota porini. Kwa kuzingatia faida ya mmea huu umefika wakati kwa watanzania kuanza kuotesha katika bustani zetu ili usije ukapotea.
Mmea wa Artemisia arfa pamoja na kutibu malaria pia hutibu magonjwa kemkem  yakiwamo kuvimba kwa utumbo mkubwa (colitis), Ukimwi kwa  kuwa waathirika wa ukimwi wana upungufu wa kinga ya cellular na kinga ya humoral iliyo juu, vichomi, huleta hamu ya kula, utando mweupe mdomoni (candida), majipu, kichocho, kikohozi, mafua, sinusitis, magonjwa ya macho na conjunctivitis, macho mekundu, homa ya matumbo(Typhoid) ikichanganywa na mmea wa Cape Gooseberry. Watu wa mwambao wa pwani (Tanga) hutumia mmea huu kwa kuuchoma kama ubani kwa kuondoa mapepo mabaya (mashetani) huuita kwa jina la pakanga. Pia hutumika kutengeneza juisi kwa maji baridi yaliyo salama kwa kuchanganya na malimao na sukari. Kinywaji hiki ni mbadala mzuri wa soda ya dukani ukizingatia faida zake.
Hutumika kutengeneza dawa ya magonjwa ya ngozi kwa kuchanganya na mafuta ya mbogamboga. Hutumika kuhifadhia nafaka ili zisiharibiwe na wadudu. Ni dawa ya kuzuia magugu yasiote kwa kusambaza majani kwenye ardhi. Wizara ya afya na ustawi wa jamii kitengo cha utafiti wa tiba asilia kifanye utafiti wa mmea huu kwa kushirikiana na waganga wa tiba asili na mbadala.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

UYOGA CHAKULA KITAMU, FAIDA NA HASARA ZAKE KWA BINADAMU.



Uyoga ni  chakula, tena wanaokifahamu  vizuri  wanakwambia  ni  chakula  kitamu. Mbali ya kuula , Uyoga UYOGA una faida nyingi kwa binadamu. Uyoga  kama  chakula  una tumika  kwa  namna nyingi tofauti naunaliwa  karibu  katika  kira sehemu  duniani. Wakati kwa  AFRIKA, UYOGA unaonekana kwamba nichakula  cha  kawaida ,kwaULAYA na  MASHARIKI MBALI (ASIA) ni chakula muhimu  na cha gharama  kubwa. kwa leo nitaelezea uyoga aina chaza  (OYSTER MUSHROOM) Pleorotus  florida (PFM) – mweupe Pleorotus floridanus(PFST )-Kahawia na wa porini. Uyoga wa Pleorotus  florida (PFM) na Pleorotus  Floridanus (PFST) ndio unaolimwa sasa katika mikoa ya mbeya, iringa, Ruvuma,  Morogoro, Rukwa,pwani DSM, Arusha ,Kilimanjaro ,NK. Watanzania naomba tuchangamkie  kilimo cha uyoga.
Kina faida nyingi. wengine wanaula katika saladi, wengine wanatumia kuongeza ladha  katika mayai, nyama, mchuzi wa tambi, wengine wanatengeneza supu na matumizi mengine tofauti.
VIINI LISHE NA FAIDA ZA UYOGA KATIKA KULINDA AFYA YA MWANADAMU.
Siku  hizi watu  wengi zaidi wanakuwa makini sana na vyakula wanavyokula ilikulinda afya zao .Baadhi ya vyakula hususanif  vile vyenye LEHEMU ama mafuta mengi husababisha maradhi mbalimbali mwilini kama shinikizo  la damu na mengineyo. Uyoga unapotumiwa kwa chakula kamwe hauleti madhara  yoyote bali faida nyingi hazipatikani katika vyakula vingi tunavyotumia. Katika uyoga kuna kiasi cha kutosha  cha protini ,kabohaidreti  na nishati. Lehemu (cholesterol) ambayo husababisha shinikizo la damu  na mengineyo ambayo hupatikana katika aina mbalimbali za protini, haipo kabisa katika uyoga.
Kadhalika ni katika protini za uyoga pekee ambako hupatikana aina zote tisa (9) muhimu za amino asidi ambazo ni muhimu katika kila mlo wa binadamu. Milinganisho ya protini, kabohaidreti , na lehemu na nguvu kati ya UYOGA  na aina mbalimbali za nyama ni kama ifuatavyo . ASIDI ambazo ni muhimu katika kila mlo kamili wa mwanadamu .


Virutubisho
Nyama mbichi ya kuku
Nyama mbichi ya ng’ombe
Samaki kibua mbichi
Uyoga
Protini (mg/100g)
20.5
2013
17.4
12.2
Kabohaidreti (mg/100g)
0
0
0
5.1
Lehemu/ mafuta (mg/100g)
69
59
50
0
Nishati/Nguvu (kj/100g)
506
514
518
334

Kadhalika uyoga una aina mbili za vitamini, zikiwemo Thiamine (vitamin b1) riboflavin (vitaminiB2) Ascorbic Acid (vitamin C) Pamoja na folic acid. Utumiaji wa mara kwa mara wa uyoga hutoa ulinzi wa kutosha dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu  wa vitamin mwilini (kama  vile Beriberi,Pellagra Na Scurvy).
Uyoga mkavu una viini lishe vifuatavyo (1) Protini 20% -45% (2) vitamini B,C,D,E,K,        (3) Madini Calcium, Phosphorus, Chuma, na kiasi  kidogo cha mafuta na mengineyo .
TIBA: Husaidia kutibu/ kupunguza shinikizo la damu, kisukari, vidonda vya tumbo, saratani (kansa), Figo, moyo, uvimbe, vidonda vya mwili, kiungulia, vipara, fangasi aina zote, kifua kikuu, kuongeza kinga ya mwili na kuuwezesha kupigana na magonjwa mbalimbali, kuyeyusha na kusaga takataka zenye asili ya kaboni. Huongeza maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha, saratani ya damu (Leukemia), Ini na mengineyo mengi.
Uyoga unafaa sana kwa waathirika wa UKIMWI.
Faida nyingine ya uyoga ni kusafisha mazingira kwa vile uyoga huoteshwa kwa kutumia mabaki yatokayo mashambani, viwandani na nyasi (majani ya maharagwe, mpunga, randa za mbao n.k). Kuotesha uyoga kwa kutumia takataka hizo ambazo zingekuwa kero kwa jamii ni njia mojawapo ya kusafisha mazingira na mabaki yakishatumika kuoteshea uyoga yanafaa sana kurutubisha ardhi (Mbolea).
MADHARA/ HASARA: - Si uyoga wote unaofaa kwa chakula, kwa sababu aina nyingine za uyoga una sumu inayoweza kumdhuru mtumiaji hadi kumletea kifo. Hakikisha unakula uyoga unaokubalika na si kila aina ya uyoga.
Jinsi ya kufanya kilimo cha uyoga au kuotesha wasiliana nami.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com





GRAVIOLA TREE (Annona Senegalensis, Soursop-Guyabano)


Tumaini jipya la kutibu Saratani siku zijazo. Wadigo huita Mbokwe.


GRAVIOLA TREE (Annona Senegalensis, Soursop-Guyabano kwa Kiswahili linaitwa Topetope au Stafeli ni mti ulioonyesha kufanya miujiza kutibu saratani mbalimbali zinazosumbua wanadamu. Nchini Tanzania unaweza kupata topetope au stafeli katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Bukoba n.k
Huko Brazil watafiti wanahangaika na topetope au stafeli katika kutibu saratani aina mbalimbali kwa kuwa imeonesha kwamba stafeli lina uwezo mkubwa wa kutibu saratani vizuri kuliko tiba za dawa za viwandani (chemotherapy) aina ya Adriamycin-iliyozoeleka kutibu saratani zaidi ya kuwa ndiyo tiba ya saratani, pia ina dawa ya kuua bacteria na fangasi na wadudu ndani ya tumbo kama aina zote za minyoo! Linashusha shinikizo la damu( Blood pressure) iliyo juu na linatuliza neva zilizosisimka. Mungu alisema ni chakula alikuwa na maana hiyo.
Licha topetope (Stafeli) kutibu saratani kwa usalama na rahisi bila madhara, au kupungua uzito wala kunyonyoka nywele, pia linalinda na kujenga mfumo wa mwili usiambukizwe pia tunda linachangamsha mwili na kumpa mtu afya ya ujana wake. Tafiti zinazoendelea kufanyika huko Brazil na Korea ya Kusini zinaonyesha aina zote za seli za saratani huuawa na topetope katika mwanzo tu wa kutumia stafeli na aina 12 za kwanza ikiwemo saratani ya matiti, glandi ya prosteti, utumbo mpana, mapafu na kongosho ndizo zinamalizwa mapema kabisa. Cha ajabu, tafiti zimeonyesha kuwa lishe ya topetope ikiwa imeshayeyushwa na kufyonzwa mwilini, inaua seli za saratani na sio zile zenye manufaa za mwili, ulimbo(gundi) ya mti huo hutibu vidonda vya kujikata. Pia tunda la tope tope  hutibu kuharisha, kuhara damu na kutapika.
Ni muhimu kila familia ikaangalia uwezekano wa kupanda miti ya stafeli/ topetope ili kuboresha afya zetu.
Pia tunatibu Taifodi (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Hyper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda, Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo na kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi n.k
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Wednesday, November 6, 2013

MAAJABU YA Gotu Kola



KUIMARISHA KUMBUKUMBU (IMPROVING MEMORY)
CENTELLA ASIATICA au Gotu Kola, Indian Pennywort, Marsh Penny ni mmea unaoota kwa kutambaa. Na huota sehemu zilizo na unyevu mwingi na kwenye kingo za mito. Mmea huu umekuwa ukitumika sana huko mashariki ya mbali India, China, Japan, Indonesia na nchi za Amerika. Hapa nchini Tanzania ni watu wachache sana wanaotumia, na hii inatokana na watu wengi kutoufahamu kazi yake japo wanauona wanapokuwa kwenye shughuli zao nyingine. Mmea huu una virutubisho vingi vinavyoweza kumsaidia binadamu kuboresha afya yake. Watu wengi wakifikia umri wa miaka 50 na kuendelea kumbukumbu zao kichwani huanza kupungua. Mmea huu ukitumiwa vizuri utaimarisha kumbukumbu zetu vizuri. Mmea huu hauishii hapo tu unatibu na magonjwa mengine kama kisukari huko India, China, Japan, Indonesia n.k hutumia sana. Magonjwa ya kuharisha damu kwa watoto katika hatua za mwanzo na matatizo ya tumbo kwa watoto. Matatizo ya tumbo kwa watoto huchanganywa na majani ya Fenugreek (Methi kwa kihindi). Ni mmea mzuri kwa mfumo wa neva (Nervous Disorders). Ni mmea mzuri kwa watu wenye matende (elephantiasis) juisi yake hupakwa sehemu zilizoathirika.
Pia ni mmea mzuri sana ukichanganywa  na mmea wa Trichodesma Indicum kutibu utasa kwa wanawake (Female Sterility) Hapa ni vizuri tukaelewana kuwa mwanamke asiwe na matatizo ya hedhi (Menstrual Pain) kutoka uchafu sehemu za siri (Usaha), uzito mkubwa sana n.k kama ana matatizo haya atibu kwanza. Pia hutibu magonjwa ya ngozi na vidonda vinavyotokana na kaswende. (Syphilitic Sores).
Pia majani yake huko India hutumika kutengeneza supu, Chatne, Chai, Juisi na kuchanganya kwenye chapati.
Tahadhari: Inashauriwa kutumia juisi kidogo ya mmea huu kwa sababu ina nguvu sana.
Kwa kuwa huu mmea unaweza kupanda kwenye bustani au kwenye makopo ya kupandia maua tunashauri kila familia ipande ili kuboresha afya.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si ahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.