Familia;
Compositae
Jamii
za porini za Artemisia hustawi katika hali ya hewa ya joto dunia nzima.
Artemisia arfa ni ya asili na imekuwa ikitumiwa miaka mingi iliyopita na watu
kwa kutibu homa na magonjwa mengine. Huko nchini China na Vietnam wanatumia
Artemisia annua ya mbegu mbili tofauti iliyotokana na mimea ya asili ya huko ya
Artemisia. Na Artemisia annua ndiyo inayotumika kutengeneza dawa mseto ya
malaria hapa Tanzania. Artemisia arfa inastawi katika maeneo ya tropiki, hutoa
majani kwa wingi, na majani haya yana Arteminisin kwa wingi, kitu ambacho kinafaa
sana kutibu malaria, mmea huu hukua hadi kufikia urefu wa mita 3 lakini
haustahimili theluji. Hapa nchini Tanzania Artemisia arfa huota porini. Kwa
kuzingatia faida ya mmea huu umefika wakati kwa watanzania kuanza kuotesha
katika bustani zetu ili usije ukapotea.
Mmea
wa Artemisia arfa pamoja na kutibu malaria pia hutibu magonjwa kemkem yakiwamo kuvimba kwa utumbo mkubwa (colitis),
Ukimwi kwa kuwa waathirika wa ukimwi
wana upungufu wa kinga ya cellular na kinga ya humoral iliyo juu, vichomi,
huleta hamu ya kula, utando mweupe mdomoni (candida), majipu, kichocho,
kikohozi, mafua, sinusitis, magonjwa ya macho na conjunctivitis, macho mekundu,
homa ya matumbo(Typhoid) ikichanganywa na mmea wa Cape Gooseberry. Watu wa
mwambao wa pwani (Tanga) hutumia mmea huu kwa kuuchoma kama ubani kwa kuondoa
mapepo mabaya (mashetani) huuita kwa jina la pakanga. Pia hutumika kutengeneza
juisi kwa maji baridi yaliyo salama kwa kuchanganya na malimao na sukari.
Kinywaji hiki ni mbadala mzuri wa soda ya dukani ukizingatia faida zake.
Hutumika
kutengeneza dawa ya magonjwa ya ngozi kwa kuchanganya na mafuta ya mbogamboga.
Hutumika kuhifadhia nafaka ili zisiharibiwe na wadudu. Ni dawa ya kuzuia magugu
yasiote kwa kusambaza majani kwenye ardhi. Wizara ya afya na ustawi wa jamii
kitengo cha utafiti wa tiba asilia kifanye utafiti wa mmea huu kwa kushirikiana
na waganga wa tiba asili na mbadala.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya
ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali
ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali
wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi
(Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa
hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,
vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine
mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Ntaweza kuzipata walimlemen mbegu zake
ReplyDeleteWapewe wagonjwa wa Corona.
ReplyDeleteMnapatkana wap
ReplyDelete