K
Kurimbasi
ni mmea wa msimu, hukua karibu na nyumba na una harufu nzuri, watanzania wengi
hawaujui mmea huu vizuri lakini wahindi, wagiriki na wazungu wanaujua vizuri
sana.
Jina
la kibotania huitwa Ocimum basilicum. Waingereza huita Basil, wagiriki huita
Basilikon yaani mmea Mtukufu. Na inasemekana asili yake ni India, pia una
majina mengine common basil, sweet basil, Garden basil, great basil na saint
Joseph’s-wort.
Mmea
huu una protini, vitamin A, vitamin B6, vitamin C, vitamin E, vitamin K, Riboflavin,
Thiamine, Niacin, Folate, Choline, Calcium, Magnesium, Chuma, Phosphorus,
Sodium, Manganisi, Potassium na Zinki kidogo. Mmea huu hutibu maumivu ya tumbo,
usagaji wa chakula, mfumo wa neva, kuondoa gesi tumboni, Colic, mafua,
influenza, kichefuchefu, gastro- enteritis, kipanda uso,uchovu, sonona, kukosa
usingizi, kikohozi, kumbukumbu, kuongeza utokaji wa mkojo, wasiwasi, kuongeza
utokaji wa maziwa kwa akina mama, maumivu ya misuli na kuteguka, kuumwa na
wadudu kama nyuki, nyoka na matatizo ya ngozi.
Mbegu
hutibu kisonono, kuhara damu na kuharisha. Kurimbasi hufukuza mbu na wadudu wengineo.
Pia wengine huweka kwenye mapishi kuongeza ladha.
Matumizi,
tumia gramu 2-4 za unga wa mmea huu mara tatu kwa siku, pia unaweza kutumia
majani mabichi.
Tahadhari:
kurimbasi ina nguvu sana unaweza kusababisha kuwasha ngozi kwa watu wengine,
kila mara tumia kwa uangalifu , wajawazito wasitumie bila ushauri wa daktari.
Na kadri mgonjwa anapofika na
kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira
Natural Products
Mbeya
Simu;
+255 754 807401, +255 719 564276
Blogu:
mazingiranp.blogspot.com
K