Pages

Thursday, August 31, 2017

KURIMBASI MMEA UNAOTIBU MAGONJWA MENGI



K


Kurimbasi ni mmea wa msimu, hukua karibu na nyumba na una harufu nzuri, watanzania wengi hawaujui mmea huu vizuri lakini wahindi, wagiriki na wazungu wanaujua vizuri sana.
Jina la kibotania huitwa Ocimum basilicum. Waingereza huita Basil, wagiriki huita Basilikon yaani mmea Mtukufu. Na inasemekana asili yake ni India, pia una majina mengine common basil, sweet basil, Garden basil, great basil na saint Joseph’s-wort.
Mmea huu una protini, vitamin A, vitamin B6, vitamin C, vitamin E, vitamin K, Riboflavin, Thiamine, Niacin, Folate, Choline, Calcium, Magnesium, Chuma, Phosphorus, Sodium, Manganisi, Potassium na Zinki kidogo. Mmea huu hutibu maumivu ya tumbo, usagaji wa chakula, mfumo wa neva, kuondoa gesi tumboni, Colic, mafua, influenza, kichefuchefu, gastro- enteritis, kipanda uso,uchovu, sonona, kukosa usingizi, kikohozi, kumbukumbu, kuongeza utokaji wa mkojo, wasiwasi, kuongeza utokaji wa maziwa kwa akina mama, maumivu ya misuli na kuteguka, kuumwa na wadudu kama nyuki, nyoka na matatizo ya ngozi.
Mbegu hutibu kisonono, kuhara damu na kuharisha. Kurimbasi hufukuza mbu na wadudu wengineo. Pia wengine huweka kwenye mapishi kuongeza ladha.
Matumizi, tumia gramu 2-4 za unga wa mmea huu mara tatu kwa siku, pia unaweza kutumia majani mabichi.
Tahadhari: kurimbasi ina nguvu sana unaweza kusababisha kuwasha ngozi kwa watu wengine, kila mara tumia kwa uangalifu , wajawazito wasitumie bila ushauri wa daktari.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


K

No comments:

Post a Comment