Nilipokuwa kwenye
shughuli zangu za utafiti wa mimea 4/6/2017. Niliona mimea aina ya LEONOTIS
NEPETIFOLIA maua yake yakiwa yamezungukwa na nyuki wengi sana wakitafuta chakula.
Nyuki hao ndiyo walionifanya niandike makala fupi ya mmea huu.
Leonotis Nepetifolia
una majina mengine kama Annual lion’s ear, lion’s ear, klip dagga, gran
tiparani, Flor de mundo, mota, Christmas candlestick, shandilay, na bradi-bita.
Mmea huu hukua kutoka mita moja mpaka tatu. Mbegu zake husambazwa na maji,
matope sehemu yauamopita magari na wanyama.
Leonotis Nepetifolia
una alkaloids (leonurine na stachydrene), Iridoid glycoside (Leonuride),
Iridoid glycosides (leonurin and leonuridine) diterpenoids (leocardin), flavonoids
(rutin, quercetin, hyperoside, apigenin), volatile oil, tannins na vitamin A.
Mmea huu maua yake
hupendwa sana na wachunga ng’ombe na vijana huko vijijini wananyonya maji
matamu yaliyomo ndani ya maua yaani nectar.
Majani hutibu matatizo
ya tumbo, kuuma tumbo, arthritic, kisukari aina ya-2 diabetes mellitus, kizuia
pumu, kuzuia kuharisha, homa, malaria, kikohozi, womb prolapsed, kutuliza
kiherehere cha moyo, hufanya moyo uwe na nguvu katika utendaji wa kazi,
tachycardia, mapigo yasiyo ya kawaida ya moyo (irregular heart beats), kuongeza
utokaji wa mkojo, uvimbe, thrush, plasta kwenye vidonda na kaswende. Mchemko wa
majani na ukanywewa hutibu kuwasha na magonjwa ya ngozi.
Mizizi hutibu matatizo
ya Tumbo. Kwa wale wanaoshughulika na mambo ya nyuki na Asali mmea huu unafaa
sana kuwa chanzo cha kupata Asali nzuri.
Na kadri mgonjwa
anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji
tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment