Pages

Thursday, August 31, 2017

KURIMBASI MMEA UNAOTIBU MAGONJWA MENGI



K


Kurimbasi ni mmea wa msimu, hukua karibu na nyumba na una harufu nzuri, watanzania wengi hawaujui mmea huu vizuri lakini wahindi, wagiriki na wazungu wanaujua vizuri sana.
Jina la kibotania huitwa Ocimum basilicum. Waingereza huita Basil, wagiriki huita Basilikon yaani mmea Mtukufu. Na inasemekana asili yake ni India, pia una majina mengine common basil, sweet basil, Garden basil, great basil na saint Joseph’s-wort.
Mmea huu una protini, vitamin A, vitamin B6, vitamin C, vitamin E, vitamin K, Riboflavin, Thiamine, Niacin, Folate, Choline, Calcium, Magnesium, Chuma, Phosphorus, Sodium, Manganisi, Potassium na Zinki kidogo. Mmea huu hutibu maumivu ya tumbo, usagaji wa chakula, mfumo wa neva, kuondoa gesi tumboni, Colic, mafua, influenza, kichefuchefu, gastro- enteritis, kipanda uso,uchovu, sonona, kukosa usingizi, kikohozi, kumbukumbu, kuongeza utokaji wa mkojo, wasiwasi, kuongeza utokaji wa maziwa kwa akina mama, maumivu ya misuli na kuteguka, kuumwa na wadudu kama nyuki, nyoka na matatizo ya ngozi.
Mbegu hutibu kisonono, kuhara damu na kuharisha. Kurimbasi hufukuza mbu na wadudu wengineo. Pia wengine huweka kwenye mapishi kuongeza ladha.
Matumizi, tumia gramu 2-4 za unga wa mmea huu mara tatu kwa siku, pia unaweza kutumia majani mabichi.
Tahadhari: kurimbasi ina nguvu sana unaweza kusababisha kuwasha ngozi kwa watu wengine, kila mara tumia kwa uangalifu , wajawazito wasitumie bila ushauri wa daktari.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


K

MAAJABU YA KARANGA PORI KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI



 Zao la karanga pori ni miongoni mwa zao lisilopewa kipaumbele sana hapa Tanzania, zamani wakati wa ujana wangu, bibi mzaa mama alipanda miti miwili, ilikuwa inakuwa na karanga nyingi tulikuwa tunakula bila kujua faida yake kwa mwili wa binadamu.
Mama mkwe wangu Tamali Mwasomola amepanda miti mitatu na ukifika msimu wa karanga watoto huja kununua.
Miaka ya hivi karibuni kampuni ya maparachichi Rungwe na Enterprise works walikuwa wakihamasisha wananchi wa mkoa wa Mbeya kupanda karanga pori zinazoanza kuzaa kwa muda mfupi tofauti na zingine.
Asili ya karanga pori ni Australia. Pia nchi zingine zinazolima kwa wingi ni Brazil, Indonesia, Kenya, New Zealand na Afrika kusini. Karanga pori ya Hawaii ina ladha nzuri, kuna aina saba ya karanga pori, lakini zinazoliwa ni aina mbili.
Ø  Majina ya kibotania huitwa Macadamia Integrifolia na  Macadamia Tetraphylla, waingereza huita Macadamia Majina mengine huitwa Australia nut, Queen sland nut na Bush nut.
 . Nchini Kenya wanaita Njugu ya macadamia. Hapa Tanzania hustawi sehemu za Rungwe, Ifakara, Morogoro, Kilolo, Arusha, Hai na Lushoto nk.
Karanga pori ina vitamin A, Protini, Chuma, Thiamin, rifboflavin, niacin,folates, zinki, shaba, calcium,phosphorus,potassium na magnesium. Karanga pori ina kizuia Oxidants kama polyphenols, Amino acids, flavones na selenium. Pia kuna sucrose, fructose, glucose na maltose nk.
Faida zitokanazo na kula mara  kwa mara karanga pori ni kukinga magonjwa ya moyo (Heart Disease) kwa kuondoa lehemu, kupunguza uzito, kuimarisha afya ya mifupa, inaboresha akili ukichanganya na maziwa pia zabibu. Ina nyuzi lishe inayosaidia umeng’enyaji wa chakula tumboni na kuondoa ukosefu wa kwenda haja kubwa kwa shida, ina mafuta ya Oleic acid yanayohamasisha kuwa na kumbukumbu nzuri.
Hufanya seli na tishu za mwili ziwe na nguvu, Hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, saratani na arthritis kwa kuwa kuna omega – 3 na Omega – 6 fatty acids, kuondoa radiko huru (free radicals) ambayo husababisha magonjwa ya saratani ya matiti, kizazi na saratani ya Tezi dume. Huchelewesha ngozi kuzeeka haraka, Huzuia ugonjwa wa trans- epidermal water loss (TEWL), Hulinda ngozi na nywele zisiharibirike haraka, Huzuia kukatika ovyo kwa nywele zisiharibike haraka, inasaidia kuboresha afya kwa wale waishio na VVU na Ukimwi hasa kwa kuongeza kinga ya mwili na karanga pori, hutumika kutengenezea mafuta ya kula, kuongeza ladha kwenye chokoleti, ice cream, keki, sherbets, maandazi, brittles, candies, mafuta ya kupaka mwili na mafuta ya nywele.
Pia karanga pori huliwa zikiwa mbichi, kavu au kuchoma kwenye moto.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com



KULA MAHINDI YA NJANO UEPUKANE NA KISUKARI




Kwa maoni yangu, mhindi ni mmea wenye utaratibu wa kuvutia. Kuanzia majani yake hadi kwenye mbegu zilizo kwenye hindi lenyewe , kila kitu kimepangwa kwa mpangilio hususa wenye kupendeza.  Isitoshe, mmea huu unapokua “unazungumza” nawe. Unakuambia ikiwa una kiu au hauna lishe ya kutosha.  Kwa kawaida mtoto wa kibinadamu hulia anapohitaji kitu.  Kama tu mimea mingine, mhindi hutoa ishara zinazoonekana, kama vile kubadili rangi na umbo la majani yake, ili kueleza mahitaji yake.  Unahitaji kuelewa ishara hizo.  Huenda majani yenye rangi nyekundu na Zambarau yakaonyesha kwamba mhindi hauna Fosfati.
             Dalili nyingine zinaweza kuonyesha ukosefu wa magnesi, nitrojeni, au potashi. Pia anapoungalia Mkulima anaweza kutambua ikiwa mhindi wake una ugonjwa au umeathiriwa na kemikali.  Mhindi ulianza  kukuzwa huko. Amerika , huenda katika nchi ya Mexico, na kuenea ulimwenguni pote.  Waperu walioishi kabla ya enzi ya wainka waliabudu Mungu wa kike wa mahindi aliyepambwa kwa taji lililotengenezwa kwa bunzi za mhindi. Bunzi hizo zilitokea kichwani mwake kama nyaya katika gurudumu.Wakaaji wa ulaya waligundua mhindi mnamo mwaka 1492 baada ya mvumbuzi Christopher Columbus kuwasili katika visiwa vya karibea.
              Kuna aina nyingi za mahindi zinazogawanya katika vikundi sita vikuu: dent,flint,Flour,sweet,waxy, na popcorn.  Mahindi aina ya sweet hayakuzwi sana kama aina nyingine. Utamu unaopatikana katika aina hii ya mahindi unatokana na kasoro Fulani ambayo huizuia kubadili kiasi cha kutosha cha sukari kuwa wanga.  Zaidi ya asilimia 60 ya mahindi inayouzwa ulimwenguni hutumiwa kulisha mifugo huku asilimia 20  hivi ikilisha  wanadamu.  Asilimia iliyobaki hutumiwa viwandani au kama mbegu. Jina la kibotaniahuitwa ZEA MAYS. Huko India huita CORN (Makai) na Amerika (India corn) haya mahindi ni ya njano mengine ya kawaida na mengine ya Bisi (Popcorn) haya ndiyo nitaelezea umuhimu wake kwa afya zetu.
               Haya mahindi ya njano ya kitumiwa vizuri yanapunguza kuongezeka uzito (weight gain), mahindi haya yana magnesium kwa wingi yanayosaidia kuyaweka matumbo yetu yawe vizuri (wonderful bowel regulator), yanasaidia kujenga mifupa na misuli.  Yana phosphorus kwa wingi inayosaidia kujenga ubongo vizuri na mfumo wa fahamu,Yana madini ya zinki yanayosaidia kuimarisha nguvu za uzazi ukiongeza kikombe kimoja cha unga wa njano kwenye mlo unakua na 2mg za madini ya zinki, kupunguza lehemu kwenye damu (blood cholesterol levels), pia yanamadini ya chuma yanayosaidia kuongeza nguvu mwilini na kinga ya mwili kwa kuzisaidia seli nyeupe za damu ili kupambana na maradhi, yanavitamini “A” nyingi ambayo inatoa kinga dhidi ya magonjwa. Inazuia upofu kwa watoto, inaimarisha misuli ya macho kwa wazee, yana nyuzinyuzi (fiber) ambayo inazuia kisukari na unene,  kuondoa chunusi usoni nk, kuku wa kisasa wakilishwa mahindi ya njano kiini cha yai kinabadilika toka weupe na kuwa njano, hata    kwa upande wa bisi husafisha meno, kuimarisha nguvu za uzazi, kupunguza sukari mwilini, kusafisha damu,hata watu wengine na waathirika wa UKIMWI wazitumie kuboresha afya.Mhindi una kitu kimoja kinaitwa ndevu za mahindi zina faida kubwa kwa binadamu zina Potassium nyingi ambazo zinasaidia kutibu magonjwa yafuatayo kwa wanaokojoa kitandani, maumivu ya tezi dume (prostate), maumivu ya mfumo wa mkojo (UTI) , mawe kwenye figo, moyo kutokufanya kazi yake vizuri(Congestive heart failure), kisukari ukichanganya na Drum stick,uchovu, BP (HBP), kupunguza lehemu (Cholesterd), nk.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com