Pages

Thursday, August 11, 2022

PANDA MIMEA YA BAHATI NYUMBANI KWAKO

Miti na mimea ni zawadi bora kwa binadamu na hutoa chakula , hewa safi, makazi na mahitaji yote ya maisha.Ni manufaa sana kuwa na mimea karibu nasi  kama iwezekanavyo . Kwasababu hiyo ,bustani ya ndani ni kuwa moyo .Inasaidia katika kutunza nyumba ya kijani na safi , mimea ya ndani pia huwa na manufaa mengi ya afya .Baadhi ya mimea ya ndani au mimea bustani ni kufanyika kumfikisha bahati na mafanikio katika nyumba. Mimea hii inasemekana kung’ara nishati chanya popote kukua . Orodha ya mimea michache unaweza kupanda katika nyumba yako kuleta furaha na bahati ni kama ifuatavyo.

Kurimbasi(Basil) huleta upendo ,shauku,mali,bahati na uzuri wa nyumba yako,na tunaweza wote kutumia kidogo.Kurimbasi unaweza kuitumia kwa radha ya chakula chako . Na pia inajulikana kwa kuwa dawa ya mfadhaiko , antiseptic na antibacteria pia.

Rosemary kuongezeka ubongo wako nguvu , unaweza kukusaidia kupata kupumzika usiku mzuri . Mimea hii huvutia upendo na moyo tamaa , inatabia ya ulinzi na utakaso , husaidia na uponyaji , na unaweza hata kutumia katika mapepo .

Mimea aina ya miniature roses ina nguvu kubwa ya viumbe hai wote . Huvutia upendo , uponyaji na bahati , kutoa ulinzi na uponyaji na kusaidia na uganga wa kila aina .

Roses maua meupe husaidia kusafishwa na uponyaji na nguvu chanya . Roses nyeupe na nyekundu husaidia ibada na uchu. Roses rangi ya peach husaidia amani, kiroho na urafiki . Roses rangi ya pink husaidia kimapenzi upendo , utamu , furaha na kucheza . Roses aina fuchsia husaidia tamaa kwa maisha , asili kujitegemea upendo , upendo wa kina na kukubalika ya mwili yako ya kimwili.

Roses rangi ya lavender husaidia kiroho. Roses rangi nyekundu husaidia uchu, kina na upendo wa kweli. Ndio maana biashara ya maua ya roses ni kubwa huko ulaya na Asia.

Jasmine huvutia upendo wa fedha katika nyumba yako, na moyo ndoto unabii. Jasmine mafuta inajulikana kwa kuwa  moja wa kuamsha tamaa ya kiume au kike nguvu zaidi, hivyo hii ni mimea ya ajabu kwa watoto wachanga moja au mtu kutaka kuweka mahaba hai. Maua jasmine mara nyingi huvaliwa na makuhani juu. Cha ajabu maua jasmine hufungua maua usiku, ambayo kwa mawazo yangu inawafanya hata baridi.

 Limao na ndimu pamoja na kuwa mkali na furaha limao na ndimu ni kitu ya ajabu  kwa kuwa karibu na nyumba. Ni mfano wa utakaso na urafiki. Panda karibu na nyumba yako.

 

 

 

 

 

 

Sage ni maalum kwa ajili ya sifa yake ya ulinzi, pia inawakilisha kutokufa, maisha marefu, hekima na utoaji wa matakwa. Panda nyumbani kwako mimea ya sage.

 kwa leo naishia hapa tutaendelea wiki ijayo

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

 


Mazingira Natural Products

Mbeya

Simu; +255 754 807401, +255 719 564276

Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Blogu: mazingiranp.blogspot.com

 

NSEBHE MTI UNAOTIBU MAGONJWA MENGI.

 


NSEBHE ni mti unaotibu magonjwa.NSEBHE hupatikana katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Morogoro, Tabora, Arusha, Mikoa ya Pwani na Kagera(Rulangaranga) nk. Jina la kibotania huitwa Erythrina Abyssinica. Wanyakyusa huita NSEBHE. Wasafwa huita Lisebhe.

Mti huu sitauelezea sana ila naomba watanzania wote na wale wenye mapenzi mema na mimea, tuupande, tuutunze na kuulinda mti huu kwa sababu hutibu magonjwa mengi sana, Majani hutibu vidonda vya tumbo, kuharisha, vidonda na maumivu ya viungo kwa kuweka kwenye vidonda na kuchua kwenye viungo, kutapisha, kwa wanyama hutibu magonjwa ya ngozi. Maua yakitwangwa hutibu kuhara kwa damu, magome yakirostiwa na kutwangwa kuwa unga yanatibu vidonda vya kuungua, vidonda vinavyotoa usaha na uvimbe. Rojo linalotokana na vishina vya kijani vya mti huu hutibu ugonjwa wa Conjunctivitis unaosababishwa na Chlamydia trachomatis(trachoma).

Magome hutibu Malaria, magonjwa ya zinaa kama kaswende,kisonono, Amiba, kikohozi, kuumwa na nyoka, maumivu ya Ini, maumivu ya tumbo, kusokotwa na tumbo na surua(measles). Maua yakitwangwa hutibu maumivu ya sikio, mizizi hutibu vidonda vya tumbo,malaria, epilepsy, kichocho na blennorrhagia.

Wavuvi hutumia magome yake kama maboya ya kuvulia samaki, pia sisi zamani magome yake tulikuwa tunatumia kutengenezea mihuri kwa matumizi mbalimbali.Mti huu hutumika kutengeneza vinyago, stuli, ngoma, mizinga ya nyuki na bidhaa za mikono. Mbegu zake hutumika kutengeneza urembo wa shanga za kuvaa shingoni.

 

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

 


Mazingira Natural Products

Mbeya

Simu; +255 754 807401, +255 719 564276

Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Blogu: mazingiranp.blogspot.com

 

SALADI HUONDOA SUMU MWILINI

 

 


Kilimo cha saladi ni moja ya kilimo cha mbogamboga aina ya kabichi ambacho wengi hawajui na hawakithamini hii ni tofauti na mataifa yaliyoendelea, ambao wao hutumia muda mwingi kufikiri namna ya kutunza afya zao.

Wakati huu twaweza kujiuliza kuwa ni wangapi wenye uwezo wa kupanda saladi na tukaitumia kuboresha afya zetu hapa Tanzania.

Jibu ni wachache sana, lakini nisizunguke sana labda nikukaribishe katika kilimo cha pekee ambacho hakina magonjwa mengi nacho ni kilimo cha saladi.

Jina la kibotania huitwa Lactuca Sativa. Waingereza huita Lettuce.

Saladi ziko aina nyeupe, kijani, nyeusi na nyekundu. Saladi ya kijani na nyekundu ndio zenye virutubisho bora.

Aina za saladi Romaine, Crisphead (Ice berg), Butterhead (Boston na Bibb) na Nyekundu na Kijani. Saladi zina vitamin A kwa wingi, Protini, Calcium, Vitamini C, Chuma, Vitamini K, Omega – 3 Fatty acids, Folate na potassium.

Saladi ikiliwa mara kwa mara husaidia kupunguza uzito, moyo kufanya kazi vizuri, kuondoa uwezekano wa kupata lehemu  ( Cholesterol). Wanaokosa usingizi watumie saladi, huondoa sumu mwilini, husaidia macho kuona vizuri, husaidia ngozi ya mwili kuwa na mwonekano mzuri, Huondoa anxiety, Husaidia uwezekano wa kutopata saratani ya damu na matiti na husaidia ubongo kufanya kazi yake vizuri na kuepuka ugonjwa wa Alzheimer’s.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

 


Mazingira Natural Products

Mbeya

Simu; +255 754 807401, +255 719 564276

Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Blogu: mazingiranp.blogspot.com

 

MUHOGO ZAO LA KARNE YA 21

 


            Leo nimekuandalia zao la muhogo .Na asili ya zao la muhogo ni Amerika ya kusini hasa brazil. Muhogo ni zao lenye  kustahimili hali mbaya kama ukame na mvua zisizoaminika,kutoa mazao mengi kwa eneo na  kustahimili mashambulizi ya magonjwa na wadudu.Jina la kibotania huitwa manihot esculenta au manihot utilisima.majina mengine huitwa manioc ,yucca root.waingereza huita cassava. zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini.kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula  kikuu ambacho kinachukua 75%  ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya lindi na mtwara .kwa siku za karibuni muhogo unaongoza kwa kuongezeka katika umaarufu  kuliko mazao yote ya chakula nchini .Majani ya muhogo yana protini,vitamin B12,B-2,Beta Carotene na niacin, Iysine, Isoleucine, leucine, valine.Muhogo ukiliwa huzuia saratani na kutibu Arthritis,Conjunctivitis,kuharisha,flu,maumivu ya kichwa(headaches),kuongeza nguvu mwilini,kulinda na kurekebisha tishu za mwili ,kupunguza lehemu mwilini,kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo,kujenga mifupa na meno kuwa na nguvu(imara),kutunza metabolism kuwa ya kawaida, inasaidia kurekebisha moyo utende kazi yake vizuri na blood pressure(BP) na wale wenye heart rhythm wanashauriwa kula mihogo mara kwa mara kwa kuwa una potassium kwa wingi,huzuia kukosa choo na kupunguza uzito,huimarisha uzazi(enhanced fertility) na ndio maana watu wengi siku hizi wanakula mihogo mibichi, wale walio na tatizo la celiac watumie mihogo mara kwa mara mihogo haina Gluten,wenye kisukari wale mihogo kwa kuwa inapunguza kiwango cha sukari,huzuia saratani,huimarisha Probiotics na kuongeza kinga ya mwili, inazuia Neural damage in brain na kuzuia Alzheimer kwa matatizo haya tumia majani machanga ya muhogo kwa kuwa yana vitamin kwa wingi ,huzuia anemia na kusaidia damu kubeba oksijeni vizuri na husaidia kupunguza msongo na fadhaa.

         Majani ya muhogo muhogo wenyewe yana kiwango kikubwa cha sumu aina ya hydrocyanic acid amabayo ni hatari kwa mwili lakini vitu hivyo vikipikwa sumu hiyo huondoka na kuwa salama kwa mtumiaji.      

  Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

 


Mazingira Natural Products

Mbeya

Simu; +255 754 807401, +255 719 564276

Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Blogu: mazingiranp.blogspot.com

 

MBAAZI HUTIBU HOMA YA MANJANO


 

Ni mmea wenye jamii ya mikunde. Mbaazi ni zao lenye matumizi mengi na huvumilia ukame. Matumizi muhimu zaidi yanatokana na mbegu zake ambazo zinatumika kuanzia zikiwa mbichi na baada ya kukauka. Jina la kibotania huitwa Cajanus Cajan. Wanyakyusa huita IMBANGE, wagogo huita Mhanje na Wakaguru huita Mhange. Waingereza huita Pigeon pea. Matumizi mengine ya mmea wa mbaazi ni shina lake linalotumiwa kama kuni, majani yanatumika kama dawa na chakula cha mifugo na mizizi yake ni dawa na hurutubisha ardhi. Mbaazi hulimwa katika nchi nyingi za kitropiki kama Tanzania, Kenya, Malawi, Uganda na Nigeria. Mbaazi ni chanzo kizuri cha vitamin B, chuma, na Calcium nk.  Majani hutibu kikohozi, kuharisha, maumivu ya tumbo, vidonda vinavyotoa usaha (sores), Surua, maumivu ya njia ya mkojo, homa ya manjano, upungufu wa damu, hepatitis, kisukari na muwasho wa ngozi sehemu za utupu za mwanamke. Maua yakichemshwa hutibu Mkamba (Bronchitis), Nimonia (pneumonia), kikohozi cha kawaida, kuhara damu na matatizo ya hedhi.  Mizizi hutibu kikohozi (cha kawaida) chimba mizizi ya mbaazi vipande vitano. Chemsha katika maji kiasi cha nusu lita mpaka ibakie kikombe kimoja. Iache ipoe, matumizi mgonjwa mtu mzima anywe nusu kikombe mara tatu kwa siku. Mtoto anywe kijiko kimoja kikubwa mara tatu kwa siku. Itumiwe kwa siku 3.

Ukitafuna mizizi hutibu maumivu ya meno. Mizizi pia hutibu magonjwa ya zinaa  ikichanganywa na mizizi ya ndulele. Mbaazi mbichi na kavu hutumika kwa mapishi mbali mbali ni mmea unaofaa sana kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

 


Mazingira Natural Products

Mbeya

Simu; +255 754 807401, +255 719 564276

Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Blogu: mazingiranp.blogspot.com