NSEBHE ni mti unaotibu magonjwa.NSEBHE hupatikana katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Morogoro, Tabora, Arusha, Mikoa ya Pwani na Kagera(Rulangaranga) nk. Jina la kibotania huitwa Erythrina Abyssinica. Wanyakyusa huita NSEBHE. Wasafwa huita Lisebhe.
Mti huu sitauelezea sana ila naomba watanzania wote na wale wenye mapenzi mema na mimea, tuupande, tuutunze na kuulinda mti huu kwa sababu hutibu magonjwa mengi sana, Majani hutibu vidonda vya tumbo, kuharisha, vidonda na maumivu ya viungo kwa kuweka kwenye vidonda na kuchua kwenye viungo, kutapisha, kwa wanyama hutibu magonjwa ya ngozi. Maua yakitwangwa hutibu kuhara kwa damu, magome yakirostiwa na kutwangwa kuwa unga yanatibu vidonda vya kuungua, vidonda vinavyotoa usaha na uvimbe. Rojo linalotokana na vishina vya kijani vya mti huu hutibu ugonjwa wa Conjunctivitis unaosababishwa na Chlamydia trachomatis(trachoma).
Magome hutibu Malaria, magonjwa ya zinaa kama kaswende,kisonono, Amiba, kikohozi, kuumwa na nyoka, maumivu ya Ini, maumivu ya tumbo, kusokotwa na tumbo na surua(measles). Maua yakitwangwa hutibu maumivu ya sikio, mizizi hutibu vidonda vya tumbo,malaria, epilepsy, kichocho na blennorrhagia.
Wavuvi hutumia magome yake kama maboya ya kuvulia samaki, pia sisi zamani magome yake tulikuwa tunatumia kutengenezea mihuri kwa matumizi mbalimbali.Mti huu hutumika kutengeneza vinyago, stuli, ngoma, mizinga ya nyuki na bidhaa za mikono. Mbegu zake hutumika kutengeneza urembo wa shanga za kuvaa shingoni.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment