Pages

Thursday, August 11, 2022

SALADI HUONDOA SUMU MWILINI

 

 


Kilimo cha saladi ni moja ya kilimo cha mbogamboga aina ya kabichi ambacho wengi hawajui na hawakithamini hii ni tofauti na mataifa yaliyoendelea, ambao wao hutumia muda mwingi kufikiri namna ya kutunza afya zao.

Wakati huu twaweza kujiuliza kuwa ni wangapi wenye uwezo wa kupanda saladi na tukaitumia kuboresha afya zetu hapa Tanzania.

Jibu ni wachache sana, lakini nisizunguke sana labda nikukaribishe katika kilimo cha pekee ambacho hakina magonjwa mengi nacho ni kilimo cha saladi.

Jina la kibotania huitwa Lactuca Sativa. Waingereza huita Lettuce.

Saladi ziko aina nyeupe, kijani, nyeusi na nyekundu. Saladi ya kijani na nyekundu ndio zenye virutubisho bora.

Aina za saladi Romaine, Crisphead (Ice berg), Butterhead (Boston na Bibb) na Nyekundu na Kijani. Saladi zina vitamin A kwa wingi, Protini, Calcium, Vitamini C, Chuma, Vitamini K, Omega – 3 Fatty acids, Folate na potassium.

Saladi ikiliwa mara kwa mara husaidia kupunguza uzito, moyo kufanya kazi vizuri, kuondoa uwezekano wa kupata lehemu  ( Cholesterol). Wanaokosa usingizi watumie saladi, huondoa sumu mwilini, husaidia macho kuona vizuri, husaidia ngozi ya mwili kuwa na mwonekano mzuri, Huondoa anxiety, Husaidia uwezekano wa kutopata saratani ya damu na matiti na husaidia ubongo kufanya kazi yake vizuri na kuepuka ugonjwa wa Alzheimer’s.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

 


Mazingira Natural Products

Mbeya

Simu; +255 754 807401, +255 719 564276

Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Blogu: mazingiranp.blogspot.com

 

No comments:

Post a Comment