Wafugaji wengi wa kuku Tanzania wanafuga kuku kwa mazoea ya kizamani. Leo nimeamua kuwaelezea mimea imayofaa kwa kuku. Lysine inayokuza kuku kwa haraka na kuongeza uzalishaji na methionine inayokuza kuku kwa haraka na kuongeza utagaji wa mayai mengi.
1. Mmea aina ya Tumbaku ya wazuka (Dandelions) watu wengi hupanda kama maua ya bustani. Lakini kwa binadamu unatibu zaidi ya magonjwa 18. Mmea huu una vitamin A,B,C,E na K. Pia una madini ya chuma, magnesium, phosphorus, potassium, zinc na calcium. Ukiwalisha kuku mara kwa mara hufanya kiini cha yai kiwe cha njano sana.
2. Majani ya mchicha nafaka na mbegu zake ni chakula bora sana kwa kuku na mbegu zake zina lysine kwa wingi.
3. Majani ya Russian comfrey ukiwalisha kuku mara kwa mara kiini cha yai huwa cha njano sana
4. Mmea wa msemwasemwa (kyusa) (Rumex usambarensis) ukilisha kuku hufanya kiini cha yai kuwa cha njano sana.
5. Majani ya mlonge (Moringa oleifera) hufanya kiini cha yai kuwa cha njano sana.
6. Majani ya upupu unaowasha (sting’ing nettle) yana vitamin A,C,D,K na B complex. Yana calcium, magnesium, Chromium, cobalt, chuma, phosphorus, potassium, zinc, shaba na salfa. Ukikausha majani yake kivulini au kwenye kaushio la jua (solar drier) yanafaa sana kwa kulisha kuku kwa kuchanganya kwenye vyakula.
Tunashughulika na utafiti wa mimea tiba na tiba lishe. Pia mambo mbalimbali yahusuyo ujasiriamali, usindikaji, kilimo cha uyoga na masuala ya mazingira. Jipatie ushauri mbalimbali kuhusu afya ya mwili, ujasiriamali na vyakula mbalimbali vilivyosindikwa kama vile achali ya embe na uyoga, wine na mvinyo aina zote na za matunda mbalimbali, kilimo cha uyoga, bila kusahau semina mbalimbali za mafunzo ya ujasiriamali kama utengenezaji sabuni, usindikaji vyakula na kilimo cha uyoga.
Thursday, August 11, 2022
WAFUGAJI WA KUKU CHANGAMKIENI MIMEA HII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment