Pages

Saturday, April 28, 2018

MUHOGO ZAO LA KARNE YA 21




            Leo nimekuandalia zao la muhogo .Na asili ya zao la muhogo ni Amerika ya kusini hasa brazil. Muhogo ni zao lenye  kustahimili hali mbaya kama ukame na mvua zisizoaminika,kutoa mazao mengi kwa eneo na  kustahimili mashambulizi ya magonjwa na wadudu.Jina la kibotania huitwa manihot esculenta au manihot utilisima.majina mengine huitwa manioc ,yucca root.waingereza huita cassava. zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini.kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula  kikuu ambacho kinachukua 75%  ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya lindi na mtwara .kwa siku za karibuni muhogo unaongoza kwa kuongezeka katika umaarufu  kuliko mazao yote ya chakula nchini .Majani ya muhogo yana protini,vitamin B12,B-2,Beta Carotene na niacin, Iysine, Isoleucine, leucine, valine.Muhogo ukiliwa huzuia saratani na kutibu Arthritis,Conjunctivitis,kuharisha,flu,maumivu ya kichwa(headaches),kuongeza nguvu mwilini,kulinda na kurekebisha tishu za mwili ,kupunguza lehemu mwilini,kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo,kujenga mifupa na meno kuwa na nguvu(imara),kutunza metabolism kuwa ya kawaida, inasaidia kurekebisha moyo utende kazi yake vizuri na blood pressure(BP) na wale wenye heart rhythm wanashauriwa kula mihogo mara kwa mara kwa kuwa una potassium kwa wingi,huzuia kukosa choo na kupunguza uzito,huimarisha uzazi(enhanced fertility) na ndio maana watu wengi siku hizi wanakula mihogo mibichi, wale walio na tatizo la celiac watumie mihogo mara kwa mara mihogo haina Gluten,wenye kisukari wale mihogo kwa kuwa inapunguza kiwango cha sukari,huzuia saratani,huimarisha Probiotics na kuongeza kinga ya mwili, inazuia Neural damage in brain na kuzuia Alzheimer kwa matatizo haya tumia majani machanga ya muhogo kwa kuwa yana vitamin kwa wingi ,huzuia anemia na kusaidia damu kubeba oksijeni vizuri na husaidia kupunguza msongo na fadhaa.
         Majani ya muhogo muhogo wenyewe yana kiwango kikubwa cha sumu aina ya hydrocyanic acid amabayo ni hatari kwa mwili lakini vitu hivyo vikipikwa sumu hiyo huondoka na kuwa salama kwa mtumiaji.      
  Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

MGOMBA MWITU HUTIBU MIFUPA ILIYOVUNJIKA




 Mgomba Mwitu ni jamii ya migomba. Nimelazimika kuandika makala ya mmea huu, nilienda safari wilayani Rungwe niliona nyani wawili wakila ndizi za mmea huu. Nyani hao walinikumbusha mbali wakati wa utoto wangu tukichunga ng’ombe tulikuwa tunakula ndizi zake kutuliza njaa. Miaka hiyo nilikuwa sijui faida ya mmea huo zaidi ya kutuliza njaa na kiu ya maji. Mmea huu hulimwa sana Ethiopia kwa ajili ya chakula. Hapa Tanzania huota porini na wengine hupanda majumbani mwao kama mapambo. Jina la kibotania huitwa Ensete Ventricosum, majina mengine huitwa Ethiopian Banana, Abyssinian banana, na Ensete false banana. Kwa Kiswahili huitwa mgomba mwitu. Wanyakyusa huita Ibangalala, wameru huita mukobo. Ndugu Erick Saimon Ngao alisema wasafwa huita Kogo(makogo). Ndugu Asunta Ndunguru alisema wamatengo huita mahigo. Mmea huu hupatikana Sudani, Ethiopia, West DR Congo, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Tanzania, Angola, Zambia, Malawi, Zimbabwe na Msumbiji.
Majani na shina hutibu Ini, Hepatitis na wanawake ambao mimba zinaharibika mara kwa mara, kurahizisha wanawake kujifungua vizuri wanapokuwa na uchungu, kuunga mifupa iliyovunjika kutokana na ajali.
Matatizo ya Ini na Hepatitis hutibiwa na majivu ya Tunda la mmea huu na majani, pia hutoa mimba zilizoharibika tumboni, utomvu wa tunda lake hutibu tatizo la kimeo kirefu kwa watoto, wamatengo hutumia kumpa maji ya mmea huu na mbatawata mtoto aliyetoka kukatika kitovu ili atoke nje na kuonana na watu wengine. Jimbi (Corm) lake hutumika kuondoa kondo la nyuma kwa ng’ombe. Wengine hupanda kama mapambo nyumbani na wengine hupanda kuzuia radi isilete madhara.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

MAFUTA YA MAWESE HUZUIA UWEZEKANO WA KUPATA SARATANI MBALIMBALI




Mafuta ya mawese hutokana na mmea wa mchikichi. Mchikichi huzalisha mafuta ya kupikia, dawa mbalimbali, diseli na mise. Mti wa mchikichi huweza kukua kufikia kimo cha meta 30. Matunda ni madogo yakiwa na shingo, Jumla mti mmoja unatoa kilo 50 za matunda.
Asili ya mchikichi ni Afrika magharibi ukanda wa Guinea.
Siku hizi michikichi inakuzwa zaidi Amerika na hasa Asia ya kusini, Malaysia na Indonesia.
Nchi Asilia za michikichi, kitropiki ya Afrika kanda ya Guinea, DR Congo, Benin, Nigeria, Senegal, Sierra leone na Togo. Afrika mashariki inapatikana Kenya, Tanzania na Uganda. Kuna aina mbili ya michikichi, Elaeis guineensis inayolimwa Afrika na Asia kusini. Elaeis oleifera inalimwa Amerika, michikichi ni zao mojawapo ya mazao ya mafuta ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kigoma, Mbeya na Tanga. Aidha zao hili hulimwa pia kwa kiasi kidogo katika mikoa ya Kagera, Pwani, Rukwa, Morogoro na Visiwa vya Pemba na Unguja. Kigoma ikiwa ni eneo muhimu kwa uzalishaji, huzalisha zaidi ya tani 2,000 za mawese na zaidi ya Tani 450 za mafuta ya mise.
Wasomaji wenzangu wa makala hii, mawese ninayoyaeleza ni yale yenye uhalisia wa rangi nyekundu na chungwa na si vinginevyo.
Kwenye mafuta ya mawese kuna vitamin A, D, E (Tocopherols) na Beta – Carotene kwa wingi. Mafuta ya mawese huongeza nguvu mwilini, huimarisha uwezo wa kuona, watu warika zote tuyatumie kwani wengi tuna matatizo ya macho kutokuona vizuri, huzuia uwezekano wa kupata Cardiovascular, Hupunguza uwezekano wa kupata saratani aina mbalimbali kwa kuwa yana Vitamini E kwa wingi, huimarisha Hormonal balance, huzuia upungufu wa vitamin kwa wakina mama wanaonyonyesha na watoto, huzuia uwezekano wa kupata magonjwa ya Alzheimes, huimarisha afya kwa wajawazito, kuimarisha kinga ya mwili na kuzuia kuzeeka haraka
TAHADHARI
Watu ambao wana lehemu mwilini (Had cholesterol) wasitumie mafuta ya mawese.
Carotenoids (Alpha, beta na gamma – carotenes)
Sterols (Sitosterol, stigmasterol na campesterol)
Vitamini E (tocopherols na tocotrienols)


Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

MACHUNGWA HUZUIA KUPATA SARATANI YA TEZI DUME



Machungwa ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa kwa wingi Tanzania. Machungwa ni zawadi nzuri ya asili toka kwa mwenyezi Mungu. Asili ya machungwa ni china. Kuna aina  za machungwa Navely, mandarin, caracara, blood oranges, valencia na Seville nk.  Jina  la kibotania huitwa Citrus sinensis au citrus aurantium. Waingereza  huita orange na wandali huita uluki. Machungwa yana vitaminim B,C, calcium, thiamin, riboflavin, nia cin, vitamin B6, folate, pantothenic acid, phosphorus, magnesium, manganese, selenium,  na  shaba. Chungwa  moja lina asilimia 130 ya vitamin C kiwango kikubwa kuliko matunda mengine, na ambacho huhitajika kutumika mwilini kila siku, vitamini A asilimia 2, calcium  asilimia 6. Pia machungwa yana choline, zeaxanthin na carotenoids ambavyo ni muhimu kuimarisha misuli ya mwili, kuleta usingizi mzuri, kuimarisha kumbukumbu na kuzuia saratani ya tezi dume. Matumizi ya juisi ya machungwa hukinga na kutibu kiharusi yakichanganywa na Barungi kwa kiharusi kinachowapata wanawake aina ya Ischemic, kupunguza shinikizo la juu la damu, kupunguza saratani ya damu kwa watoto (childhood leukemia), kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa machungwa yana nyuzi nyuzi, potassium, vitamini C, na choline kwa wingi. Wenye kisukari nao pia watumie machungwa pia hukinga/hutibu Beriberi, homa, hasa homa ya matumbo, Tb na Surua dyspepsia, kufunga choo, mifupa na meno, maradhi ya watoto kama upungufu wa damu na matege, Juisi yake ikichanganywa na chumvi kidogo na kijiko kimoja cha asali hufaa kwa wenye TB, pumu, Bronchitis, kikohozi na common colds, matatizo ya kifua, kuungua mishipa ya damu, kusafisha damu, kuimarisha kinga ya mwili kuimarisha nguvu za uzazi kusaga chakula, kuimarisha mirija ya uzazi,  kutuliza kichefuchefu kwa wajawazito, kuimarisha ngozi ya mwili isiwe na mikunjo na figo. Ni vizuri unapotumia juisi ya machungwa weka na Asali. Wenye mafua waongeze maji ya moto katika juisi ya chungwa kisha  wainywe. Maganda yake yakisuguliwa usoni ni dawa ya chunusi zote (pimples & acne). Maua yaliyokaushwa yakisagwa na kutiwa katika maji moto ni dawa ya shinikizo la mishipa ya Fahamu. Kwa pumu, kikohozi, kuumwa kichwa (kipandauso) chemsha kiganja 1 cha majani katika lita  1 ya maji kwa dakika 3 na kunywa siku moja. Pia machungwa hutumika kutengeneza Juisi, Jamu, mamaledi na mvinyo. Pia Ganda linaleta hamu ya chakula na kusaidia kuyeyusha chakula. Katakata ganda chemsha vijiko 10 vya mezani katika lita moja ya maji kwa dakika 3, kamua na kunywa siku nzima.
 pia tunatoa ushauri, mafuta ya waliopooza na Tiba
Mazingira Natural Products
Simu: +225 754 807401-0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com