Machungwa
ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa kwa wingi Tanzania. Machungwa ni
zawadi nzuri ya asili toka kwa mwenyezi Mungu. Asili ya machungwa ni china.
Kuna aina za machungwa Navely, mandarin,
caracara, blood oranges, valencia na Seville nk. Jina
la kibotania huitwa Citrus sinensis au citrus aurantium. Waingereza huita orange na wandali huita uluki.
Machungwa yana vitaminim B,C, calcium, thiamin, riboflavin, nia cin, vitamin
B6, folate, pantothenic acid, phosphorus, magnesium, manganese, selenium, na
shaba. Chungwa moja lina asilimia
130 ya vitamin C kiwango kikubwa kuliko matunda mengine, na ambacho huhitajika
kutumika mwilini kila siku, vitamini A asilimia 2, calcium asilimia 6. Pia machungwa yana choline,
zeaxanthin na carotenoids ambavyo ni muhimu kuimarisha misuli ya mwili, kuleta
usingizi mzuri, kuimarisha kumbukumbu na kuzuia saratani ya tezi dume. Matumizi
ya juisi ya machungwa hukinga na kutibu kiharusi yakichanganywa na Barungi kwa
kiharusi kinachowapata wanawake aina ya Ischemic, kupunguza shinikizo la juu la
damu, kupunguza saratani ya damu kwa watoto (childhood leukemia), kuimarisha
afya ya moyo kwa kuwa machungwa yana nyuzi nyuzi, potassium, vitamini C, na
choline kwa wingi. Wenye kisukari nao pia watumie machungwa pia hukinga/hutibu
Beriberi, homa, hasa homa ya matumbo, Tb na Surua dyspepsia, kufunga choo,
mifupa na meno, maradhi ya watoto kama upungufu wa damu na matege, Juisi yake
ikichanganywa na chumvi kidogo na kijiko kimoja cha asali hufaa kwa wenye TB,
pumu, Bronchitis, kikohozi na common colds, matatizo ya kifua, kuungua mishipa
ya damu, kusafisha damu, kuimarisha kinga ya mwili kuimarisha nguvu za uzazi
kusaga chakula, kuimarisha mirija ya uzazi,
kutuliza kichefuchefu kwa wajawazito, kuimarisha ngozi ya mwili isiwe na
mikunjo na figo. Ni vizuri unapotumia juisi ya machungwa weka na Asali. Wenye
mafua waongeze maji ya moto katika juisi ya chungwa kisha wainywe. Maganda yake yakisuguliwa usoni ni
dawa ya chunusi zote (pimples & acne). Maua yaliyokaushwa yakisagwa na
kutiwa katika maji moto ni dawa ya shinikizo la mishipa ya Fahamu. Kwa pumu,
kikohozi, kuumwa kichwa (kipandauso) chemsha kiganja 1 cha majani katika
lita 1 ya maji kwa dakika 3 na kunywa
siku moja. Pia machungwa hutumika kutengeneza Juisi, Jamu, mamaledi na mvinyo.
Pia Ganda linaleta hamu ya chakula na kusaidia kuyeyusha chakula. Katakata
ganda chemsha vijiko 10 vya mezani katika lita moja ya maji kwa dakika 3, kamua
na kunywa siku nzima.
pia tunatoa ushauri, mafuta ya waliopooza na
Tiba
Mazingira
Natural Products
Simu:
+225 754 807401-0719 564 276
Barua
pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment