Mgomba
Mwitu ni jamii ya migomba. Nimelazimika kuandika makala ya mmea huu, nilienda
safari wilayani Rungwe niliona nyani wawili wakila ndizi za mmea huu. Nyani hao
walinikumbusha mbali wakati wa utoto wangu tukichunga ng’ombe tulikuwa tunakula
ndizi zake kutuliza njaa. Miaka hiyo nilikuwa sijui faida ya mmea huo zaidi ya
kutuliza njaa na kiu ya maji. Mmea huu hulimwa sana Ethiopia kwa ajili ya
chakula. Hapa Tanzania huota porini na wengine hupanda majumbani mwao kama
mapambo. Jina la kibotania huitwa Ensete Ventricosum, majina mengine huitwa
Ethiopian Banana, Abyssinian banana, na Ensete false banana. Kwa Kiswahili
huitwa mgomba mwitu. Wanyakyusa huita Ibangalala, wameru huita mukobo. Ndugu
Erick Saimon Ngao alisema wasafwa huita Kogo(makogo). Ndugu Asunta Ndunguru
alisema wamatengo huita mahigo. Mmea huu hupatikana Sudani, Ethiopia, West DR
Congo, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Tanzania, Angola, Zambia, Malawi,
Zimbabwe na Msumbiji.
Majani na shina hutibu
Ini, Hepatitis na wanawake ambao mimba zinaharibika mara kwa mara, kurahizisha
wanawake kujifungua vizuri wanapokuwa na uchungu, kuunga mifupa iliyovunjika
kutokana na ajali.
Matatizo ya Ini na
Hepatitis hutibiwa na majivu ya Tunda la mmea huu na majani, pia hutoa mimba
zilizoharibika tumboni, utomvu wa tunda lake hutibu tatizo la kimeo kirefu kwa
watoto, wamatengo hutumia kumpa maji ya mmea huu na mbatawata mtoto aliyetoka
kukatika kitovu ili atoke nje na kuonana na watu wengine. Jimbi (Corm) lake
hutumika kuondoa kondo la nyuma kwa ng’ombe. Wengine hupanda kama mapambo
nyumbani na wengine hupanda kuzuia radi isilete madhara.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
Habari. Mizizi yake ipoje mgomba mwitu
ReplyDeleteHabari. Tiba ya mgomba mwitu kwa mifupa iliyovunjika.
ReplyDeleteMimi huwa asumbuliwa na uti wa mgongo
Delete