Mafuta ya mawese hutokana na mmea wa
mchikichi. Mchikichi huzalisha mafuta ya kupikia, dawa mbalimbali, diseli na
mise. Mti wa mchikichi huweza kukua kufikia kimo cha meta 30. Matunda ni madogo
yakiwa na shingo, Jumla mti mmoja unatoa kilo 50 za matunda.
Asili ya mchikichi ni Afrika magharibi
ukanda wa Guinea.
Siku hizi michikichi inakuzwa zaidi
Amerika na hasa Asia ya kusini, Malaysia na Indonesia.
Nchi Asilia za michikichi, kitropiki
ya Afrika kanda ya Guinea, DR Congo, Benin, Nigeria, Senegal, Sierra leone na
Togo. Afrika mashariki inapatikana Kenya, Tanzania na Uganda. Kuna aina mbili
ya michikichi, Elaeis guineensis inayolimwa Afrika na Asia kusini. Elaeis
oleifera inalimwa Amerika, michikichi ni zao mojawapo ya mazao ya mafuta ambalo
hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kigoma, Mbeya na Tanga. Aidha zao hili
hulimwa pia kwa kiasi kidogo katika mikoa ya Kagera, Pwani, Rukwa, Morogoro na
Visiwa vya Pemba na Unguja. Kigoma ikiwa ni eneo muhimu kwa uzalishaji,
huzalisha zaidi ya tani 2,000 za mawese na zaidi ya Tani 450 za mafuta ya mise.
Wasomaji wenzangu wa makala hii,
mawese ninayoyaeleza ni yale yenye uhalisia wa rangi nyekundu na chungwa na si
vinginevyo.
Kwenye mafuta ya mawese kuna vitamin
A, D, E (Tocopherols) na Beta – Carotene kwa wingi. Mafuta ya mawese huongeza
nguvu mwilini, huimarisha uwezo wa kuona, watu warika zote tuyatumie kwani
wengi tuna matatizo ya macho kutokuona vizuri, huzuia uwezekano wa kupata
Cardiovascular, Hupunguza uwezekano wa kupata saratani aina mbalimbali kwa kuwa
yana Vitamini E kwa wingi, huimarisha Hormonal balance, huzuia upungufu wa
vitamin kwa wakina mama wanaonyonyesha na watoto, huzuia uwezekano wa kupata
magonjwa ya Alzheimes, huimarisha afya kwa wajawazito, kuimarisha kinga ya
mwili na kuzuia kuzeeka haraka
TAHADHARI
Watu ambao wana
lehemu mwilini (Had cholesterol) wasitumie mafuta ya mawese.
Carotenoids
(Alpha, beta na gamma – carotenes)
Sterols
(Sitosterol, stigmasterol na campesterol)
Vitamini E (tocopherols
na tocotrienols)
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment