Machauchau
ni miongoni mwa mimea inayodharaulika na watanzania wengi pengine kwa kutokujua
faida zake kwa afya ya binadamu. Hapa Tanzania wanyakyusa na wachaga matunda
yake hulisha Ng’ombe, mbuzi na Nguruwe. Wanyakyusa mboga yake huliwa wakati
mboga zingine ni adimu.
Asili ya
machauchau ni Mexico, Costa Rica na Brazil nk.
Jina la kibotania
huitwa Sechium Edule. Waingereza huita chayote. wachaga huita machauchau. Australia huita
choko, Brazil – chuchu, Philipines -
Sayote , Hawaii – pipinola, Jamhuri ya Dominic – Tayota.
Machauchau
ni mmea unaotambaa kama pasheni na kuwa na matunda yanayofanana na baadhi ya
maboga lakini matunda yake ni madogo kuliko maboga. Machauchau yana vitamin B1 (Thiamin), B2 (Riboflavin),
B3 (Niacin), B5 (Pantothenic acid), B6 (Pyridoxine), B9 (Folate, Folic acid),
choline, vitamin E (Alpha – tocopherol), vitamin K (Phylloquinone), vitamini C
kwa wingi, calcium, chuma, magnesium, phosphorus, potassium, sodium. Zinki,
shaba, manganese na selenium kidogo na Amino Acids
Machauchau
hupunguza uzito wa mwili, Huzuia watoto kuzaliwa bila hitilafu, Hupunguza
lehemu, Huzuia saratani, Ni chanzo kizuri cha stamina, Huzuia kuzeeka mapema,
chanzo kizuri cha Antioxidants, Hutibu mawe ya kwenye figo, huzuia kutopata
choo (constipation), Hushusha shinikizo la juu la damu (HBP – high blood
pressure), Hutibu gesi tumboni, Huzuia magonjwa ya moyo, Huzuia Anemia,
Hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi, Hutunza thyroid kuwa na afya njema,
Husaidia kuzuia maumivu ya miguu na kuongeza kinga ya mwili. Watanzania tuanze
kuchangamkia mmea huu kwa ajili ya afya zetu.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment