Asparagus |
Broccoli |
Leo nitaeleza
maelezo ya aina gani ya vyakula ambavyo husaidia kuongeza idadi ya mbegu za kiume
zenye afya na ujazo wake na faida zingine za afya ya uzazi.
Mboga
ijulikanayo kama Asparagus Officinalis ambayo huwa na kiasi kikubwa cha vitamin
C ambayo ina wigo mkubwa katika kusaidia utengenezwaji wa mbegu za kiume.
Vitamini C hutoa
ulinzi kwa seli zilizopo katika kokwa za kiume (korodani) zisidhuriwe na radiko
huru (Free radicals), hivyo kufanya kiwanda cha mbegu za kiume kutengeneza
mbegu zenye afya na zenye uwezo wa kupiga mbizi kwa kasi.
Broccoli ni aina
ya mboga ambazo zipo hapa nchini ingawa watanzania wengi hatuli, ila katika
migahawa ya magharibi na ya kichina. Broccoli ina kiasi kikubwa cha foliki
ambayo hujulikana pia kama vitamin B9. Vitamini B9 ilishajulikana kwa kusaidia
wanawake waliokuwa wagumba kuweza kushika mimba, kwa sasa pia inajulikana
kusaidia wanaume wagumba.
Spinachi ni moja
ya mboga mboga ambayo inakubalika kusheheni tindikali ya foliki ambayo ni
muhimu sana katika utengenezwaji wa mbegu za kiume. Ingawa mboga zote za kijani
zinakubalika kutokana na kusheheni vitamini mbalimbali.
Pale mwanaume
anapokuwa na kiwango kidogo cha folate husababisha kuzalisha mbegu za kiume
zisizotimilifu. Mbegu za namna hii zinakua na wakati mgumu katika kufikia na
kupenya katika tando za kijiyai cha kike wakati wa Urutubishaji.
Hali kama hii
inaweza kusababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye hitilafu za kimaumbile kwa sababu
ya kijiyai cha kike kurutubishwa na mbegu yenye hitilafu.
Tunda
lijulikanalo kama komamanga ambalo lipo pia katika jamii yetu linajulikana
kusaidia kutengenezwa idadi kubwa ya mbegu zenye ubora ndio maana wahindi
hutumia sana.
Ndizi ni moja ya
tunda ambalo limesheheni vitamin A, B1 na C ambazo husaidia mwili kutengeneza
mbegu za kiume zenye afya na vilevile kuongeza wingi wa mbegu hizo.
Pia, Ndizi huwa
na kimeng’enya aina ya Bromelain ambacho huzuia mlipuko wa kinga ya mwili,
hivyo kusaidia kuongezeka wingi wa mbegu za kiume pamoja na kasi yake.
Mayai ni moja ya
vyakula vinavyokubalika kusaidia kuongeza wingi wa mbegu za kiume na vilevile
kusaidia kuongeza kasi ya mbegu za kiume.
Kutokana na
mayai kusheheni vitamin E na Protini ambavyo vyote kwa pamoja husaidia kulinda
mwili kutoka kwa sumu za radiko ambazo hupunguza wingi wa mbegu za kiume.
Vilevile
virutubisho hivyo vilivyopo katika mayai husaidia kutengenezwa kwa mbegu imara
zeneye afya jambo ambalo ni muhimu kwa Urutubishwaji wa kijiyai cha kike.
Chocholate yenye
rangi ya kahawia iliyokolea inajulikana zaidi duniani, sababu kubwa ni kutokana
na aina hii ya chocolate kuwa na Tindikali ya amino (Protini) ijulikanayo kama
L-Arginine HCL ambayo husaidia kuongeza ujazo wa mbegu za kiume na wingi wake.
Vilevile huongeza msisimko wa kilele cha tendo la ndoa.
Nyanya chungu au
Ngogwe nazo husaidia sana kuimarisha tendo la ndoa zikitumiwa mara kwa mara.
Na kadri mgonjwa
anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji
tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment