Pages

Saturday, May 26, 2018

FAIDA YA NDIZI


 Ndizi ni zao moja kati ya mazao ya matunda ambayo huzallishwa kwa wingi katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Kigoma, Tanga, Kagera na Mara. Jina la Kibotania linaitwa Musa paradisiaca na Kingereza huitwa banana.  Wandali huita Indunye na Wanyakyusa huita Amabifu /Amatoki, zao hili hutumika kama zao la chakula na tunda pia. Kando ya kula kama chakula tu, kuna malighafi nyingine tele katika mmea huu inayoweza kuufaidisha mwili wa binadamu kama tiba kwa magonjwa mbalimbali. Asili au tabia ya mmea huu inanukia, imetulia, kizuia vidonda, kiongeza mkojo na ni  kiamshi. Ndizi  ina vitamin, Virutubisho vya kuleta nguvu pamoja na aina nyingi za lishe muhimu. Pia ina madini ya chuma, potassium, Calcium, Sodium, Magnesium, Shaba, Manganese, Phosphorus, Sulphur, Silica, na Chlorine nk. Ndizi husaidia katika kuboresha hali za watu kwa maana zina kemikali za serotonin “na” dopamine” ambazo humfanya mtu kujisikia vizuri.  Ndizi hutibu athari zinazotokana na pombe kwa kusawazisha Msukumo wa damu (kwa msaada wa potassium) pamoja na kuzuia kiungulia. Maua ya ndizi  hupunguza utokaji wa damu nyingi wakati wa hedhi kwa kuyaponda ponda na kunywa.  Maua huuchemshwa na kuliwa na wenye kisukari. Pia utomvcu wake ni dawa ya kutia sikio linalouma. Ndizi mbivu ikipondwa na kuchanganywa na maziwa, sukari ni nzuri kwa kukuza watoto. Ndizi mbivu ikichanganywa na ukwaju na chumvi kidogo ni tiba nzuri kwa hatua za mwanzo za kuharisha na kuharisha damu. Wale wanaosumbuliwa na usagaji wa chakula ni vizuri watumie ndizi na kikombe kimoja cha maziwa wakati wanaenda kulala. Wale wenye bawasiri waponde ndizi na kuzichemsha pamoja na maziwa kikombe kimoja na watumie mara tatu kutwa. Hutibu kikohozi kwa kuchanganya na pilipili manga kidogo na kula mara tatu kutwa. Wenye   kifua kikuu waponde ndizi na kuchanganya na nusu kikombe cha maziwa ya mgando yaliyo salama, kijiko cha chai cha asali na kikombe kimoja cha maji ya dafu (nazi) na kutum,ia mara mbili kwa siku. Homa ya manjano na homa ya matumbo waponde ndizi na kuchanganya na kijiko cha chakula cha asali wale mara mbili kutwa kwa siku kadhaa. Majivu ya maganda ya ndizi ni tiba nzuri kwa vidonda. Ndizi mbichi unga wake ni lishe nzuri kwa wenye kisukari na wale wenye kuvuja damu wenye shida usagaji wa chakula, na wenye asidi tumboni. Majani mabichi hutumika kutibu macho yanayouma na kutuliza maumivu ya kichwa pia ponda majani na kuweka juu ya kidonda. Majivu ya shina la mmea ni tiba nzuri kwa wenye  vidonda. Juisi ni nzuri kwa wenye shida  ya mishipa ya fahamu, kuharisha, kuharisha damu na manjano. Pia inazuia damu isitoke katika vidonda vya kujikata nk. Mizizi ni tiba nzuri kwa maumivu ya ngozi laini ya njia ya mkojo na ya uzazi/uke. Mizizi iliyochujwa na kuongeza asali ni tiba ya kubanwa kwa ini na mlinzi mzuri wa ini. Utumiaji wa ndizi mbivu mara kwa mara huondoa tatizo la kufunga choo, udhaifu wa mwili na vidonda vya tumbo. Pia ukila ndizi mbili zina kutosha kukupatia nguvu za kufanya kazi ngumu kwa muda wa dakika tisini. Ndizi hutumika kwa matumizi mbalimbali kama Ugali, Chips nk.

MAZINGIRA NATURAL PRODUCTS
MBEYA
Simu: +225 754 807 401 +255 719 564 276
Barua pepe: mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com 

Friday, May 18, 2018

PANDA MIMEA YA BAHATI NYUMBANI KWAKO- 2



 Miti na mimea ni zawadi bora kwa binadamu na hutoa chakula , hewa safi, makazi na mahitaji yote ya maisha.Ni manufaa sana kuwa na mimea karibu nasi  kama iwezekanavyo . Kwasababu hiyo ,bustani ya ndani ni kuwa moyo .Inasaidia katika kutunza nyumba ya kijani na safi , mimea ya ndani pia huwa na manufaa mengi ya afya .Baadhi ya mimea ya ndani au mimea bustani ni kufanyika kumfikisha bahati na mafanikio katika nyumba. Mimea hii inasemekana kung’ara nishati chanya popote kukua . Orodha ya mimea michache unaweza kupanda katika nyumba yako kuleta furaha na bahati ni kama ifuatavyo.
Mianzi aina ya goodluck bamboo inajulikana kwa kuvutia  furaha na mali na inatoa ulinzi wa bahati. Mianzi inasemekana kuwasaidia kuongeza kubadilika akili, msaada katika ukuaji wa kiroho na kuwasaidia watu kuendeleza vipaji kisanii, na moyo afya njema. Kama wewe una huzuni, mianzi ni mmea mkubwa kwa kuwa katika nyumba yako, kama unaweza kukusaidia kujisikia chini kukwama.
Mmea aina ya honeysuckle huleta fedha katika nyumba yako na inatoa ulinzi, baadhi ya watu wanaamini kuwa kusagwa maua na kuwekwa kando ya paji la uso wako unaweza kuongeza nguvu (psychic). Pia mbali na kunusa ajabu kabisa. Honeysuckle pia ina ladha ya aina ya  nectar.
Mimea ya sage (salvia officinaries) ni maalumu kwa ajili ya sifa yake ya ulinzi. Pia inawakilisha kutokufa, maisha marefu, hekima na utoaji wa matakwa
Mimea ya lavender ina harufu ya ajabu na inajulikana kwa ajili ya moyo mwinuko na mali kutuliza. Lavender hutumika katika mambo mengi ya ubani na nyumba harufu. Harufu ya lavender huleta unafuu, kutoka maumivu ya kichwa. Harufu ya lavender inasemekana huvutia wanaume na madai ya kukusaidia kuona vizuka.
Pia kuna mmea kama tetesyeli (Dracaena usambarensis) ,Ulimi wa mama mkwe (mothers tongue in- law) na mimea aina ya orchids
Usipande nyumbani mimea usiyoijua faida yake na hasara
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

PANDA MIMEA YA BAHATI NYUMBANI KWAKO



  Miti na mimea ni zawadi bora kwa binadamu na hutoa chakula , hewa safi, makazi na mahitaji yote ya maisha.Ni manufaa sana kuwa na mimea karibu nasi  kama iwezekanavyo . Kwasababu hiyo ,bustani ya ndani ni kuwa moyo .Inasaidia katika kutunza nyumba ya kijani na safi , mimea ya ndani pia huwa na manufaa mengi ya afya .Baadhi ya mimea ya ndani au mimea bustani ni kufanyika kumfikisha bahati na mafanikio katika nyumba. Mimea hii inasemekana kung’ara nishati chanya popote kukua . Orodha ya mimea michache unaweza kupanda katika nyumba yako kuleta furaha na bahati ni kama ifuatavyo.
Kurimbasi(Basil) huleta upendo ,shauku,mali,bahati na uzuri wa nyumba yako,na tunaweza wote kutumia kidogo.Kurimbasi unaweza kuitumia kwa radha ya chakula chako . Na pia inajulikana kwa kuwa dawa ya mfadhaiko , antiseptic na antibacteria pia.
Rosemary kuongezeka ubongo wako nguvu , unaweza kukusaidia kupata kupumzika usiku mzuri . Mimea hii huvutia upendo na moyo tamaa , inatabia ya ulinzi na utakaso , husaidia na uponyaji , na unaweza hata kutumia katika mapepo .
Mimea aina ya miniature roses ina nguvu kubwa ya viumbe hai wote . Huvutia upendo , uponyaji na bahati , kutoa ulinzi na uponyaji na kusaidia na uganga wa kila aina .
Roses maua meupe husaidia kusafishwa na uponyaji na nguvu chanya . Roses nyeupe na nyekundu husaidia ibada na uchu. Roses rangi ya peach husaidia amani, kiroho na urafiki . Roses rangi ya pink husaidia kimapenzi upendo , utamu , furaha na kucheza . Roses aina fuchsia husaidia tamaa kwa maisha , asili kujitegemea upendo , upendo wa kina na kukubalika ya mwili yako ya kimwili.
Roses rangi ya lavender husaidia kiroho. Roses rangi nyekundu husaidia uchu, kina na upendo wa kweli. Ndio maana biashara ya maua ya roses ni kubwa huko ulaya na Asia.
Jasmine huvutia upendo wa fedha katika nyumba yako, na moyo ndoto unabii. Jasmine mafuta inajulikana kwa kuwa  moja wa kuamsha tamaa ya kiume au kike nguvu zaidi, hivyo hii ni mimea ya ajabu kwa watoto wachanga moja au mtu kutaka kuweka mahaba hai. Maua jasmine mara nyingi huvaliwa na makuhani juu. Cha ajabu maua jasmine hufungua maua usiku, ambayo kwa mawazo yangu inawafanya hata baridi.
 Limao na ndimu pamoja na kuwa mkali na furaha limao na ndimu ni kitu ya ajabu  kwa kuwa karibu na nyumba. Ni mfano wa utakaso na urafiki. Panda karibu na nyumba yako.
  Sage ni maalum kwa ajili ya sifa yake ya ulinzi, pia inawakilisha kutokufa, maisha marefu, hekima na utoaji wa matakwa. Panda nyumbani kwako mimea ya sage.
 kwa leo naishia hapa tutaendelea wiki ijayo
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


KOMAMANGA HUSAIDIA KUONDOA SUMU MWILINI



Komamanga ni moja ya matunda yenye faida kwa afya ya binadamu. Komamanga limekuwa likilimwa kwa miaka zaidi ya 5000 iliyopita huko mashariki ya kati. Komamanga linakua hadi kufikia kimo cha Meta 5 -10 kutegemea eneo. Jina la kibotania huitwa Punica granatum linn. Waingereza  huita Pomegranate. Hulimwa sana nchini India. Pia hili ni tunda linalopatikana sana Afrika Mashariki. Tunda la komamanga lina protini, nyuzinyuzi, wanga, calcium magnesium, oxalic acid , phosphorus, chuma, sodium,potassium, shaba, sulphur, chlorine, Vitamin A, vitamin B1, B5, Vitamin E, riboflavin, Nicotinic acid na vitamin C. komamanga  ni chanzo kizuri cha sukari, (glucose na Fructose), vitamin C na chuma,. Pia komamanga lina utajiri mkubwa wa kuleta nguvu mwilini. Juisi ya komamanga lililoiva ni nzuri kwa Homa ya matumbo, Gastric na Homa za pumu. Juisi ya komamanga ni nzuri kwa wenye high blood pressure kwani inapunguza hali hiyo. Juisi ya komamanga ikichanganywa na Asali ni nzuri kwa wenye umri mkubwa  kwa ajili ya kuimarisha kumbu kumbu iliyopotea. Upungufu  wa damu changanya juisi ya tunda la komamanga kikombe kimoja cha chai, ¼  tsp mdalasini na Asali 3tsp na kunywa. Pumu na kikohozi changanya juisi ya komamanga, Tangawizi mbichi na Asali kwa kiwango sawa. Tumia kijiko cha chakula mara mbili kwa siku. Mbegu za tunda changanya pilipilimanga na chumvi kidogo mpatie mgonjwa wa homa ya manjano. Juisi ya komamanga na ndimu pamoja ikitumiwa mara tatu kwa siku ni nzuri kwa matatizo ya Ini na homa ya manjano. Komamanga hutibu matatizo ya njia ya mkojo , Juisi ya ya tunda hilo husaidia kuponya saratani, husaidia mtiririko wa damu kwenda vizuri kwenye mishipa. Hali hiyo husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, na kiharusi, ulaji wa mara kwa mara wa tunda hilo huzuia meno kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu na maambukizi ya virusi ndani ya mwili, husaidia pia kutibu maradhi ya tumbo ikiwamo kutopata haja kubwa, komamanga husaidia kuondoa sumu mwilini, kupambana na tatizo la uzito, komamanga hutibu magonjwa ya muda mrefu kama saratani ya tezi dume, saratani mbalimbali, kisukari, baridi yabisi na jongo (gout), kuweka sawa mfumo wa chakula na njia ya usagaji wa chakula. Mbegu za komamanga, magome na mizizi yakichemshwa na maji ni  dawa ya minyoo aina tapeworms. Gome na ganda la ndani la komamanga (Rind) ni dawa ya kuwasha ngozi na koo. Pia hutumika kuosha utupu wa mwanamke unaowasha na kuweka vizuri cervic. Juisi ya komamanga ni nzuri  kwa wenye umri mkubwa kwa Figo na kibofu cha mkojo kuwa na nguvu za kufanya kazi vizuri. Kuharisha damu: tumia juisi ya majani mabichi machanga. Maganda ni tiba ya kuharisha na kuhara damu. Majani na maua hutibu virusi vya macho (conjuctivities virus). Magome hutibu bandama, vidonda vya koo, homa na leucorrhea yakichemshwa. Saga mbegu na weka ndani ya maziwa hutibu mawe katika figo. Dozi ya magome, majani au maua tumia gramu 10 hadi 15 katika lita ya maji. Pia tunatoa ushauri, mafuta ya waliopooza na tiba zingine.

Mazingira Natural Product
Simu: +255754807401/- 0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com

BAMIA HUSAIDIA KWA WANAO WAHI KUFIKA KILELENI MAPEMA



 Nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi kwa kuendelea kunipa afya njema pamoja na wewe msomaji wa Gazeti hili. Hakika ni jambo la pekee ambalo Mungu ametutunuku kwa maana wapo hospitalini wakitafuta huduma kwa ajili ya afya zao. Bamia ni mboga iliyotokea kupendwa miongoni mwa wa watanzania wengi pengine kwa kutotambua au kutambua umuhimu wake kwa afya ya binadamu.
Bamia hulimwa katika nchi za Tropiki na nusu Tropiki. Jina Bamia limetokana na jina Bamya asili yake nchi ya waThai (Thailand)
Nasisi watanzania tunaita BAMIA. Jina la kibotania huitwa Abelmoschus esculents au hibiscus esculents linn. Waingereza huita Okra au lady fingers.Bamia ina wanga , mafuta , protini, sodium, folate , calcium, magnesium,Vitamini A na C. Bamia ikiliwa mara kwa mara hupunguza sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa KISUKARI. Bamia ikilo wekwa usiku kucha kwenye maji na kunywewa  hupunguza lehemu (cholesterol) na kuweka sawa sukari mwilini. Bamia ikipondwa na kuwa rojo inafaa kupaka vidonda vya kuungua na matatizo ya ngozi . Bamia ina MUCIN inayolinda matatizo mengi yanayotokea ndani ya tumbo na utumbo kwa hiyo ikiliwa utakuwa na afya njema kila wakati. Mtokoso wa bamia ambazo hazija komaa sana hutibu maumivu ya mucous membrane inayosababisha matatizo ya upumuaji. Juisi ya Bamia hutibu maumivu ya koo yanayo sababishwa na kikohozi. Mtokoso wa majani, matunda yake hutibu mfumo wa ukojoaji kwa wanaume na wanawake kama maumivu ya mkojo unapokojoa, Kaswende na kisonono. Majani na mizizi ikipondwa na kupakwa vidonda hupona haraka. Juisi ya bamia hutibu homa , kuharisha na maumivu ya tumbo . Juisi ya bamia hutibu muwasho wa ngozi na ni“moisturizer” ya ngozi. Bamia zikiliwa mara kwa mara zinasaidia kwa wale wanaowahi kufika kileleni wakati  watendo la ndoa. Bamia zikiliwa mara kwa mara huima risha na kuboresha kumbukumbu nakuufanya uti wa mgongo ufanye  kazi yake vizuri . Mbegu za bamia zikikaangwa nakusagwa hutumika kama chai na kuongeza utokaji wa jasho. Mbegu za bamia hutibu mwako wa misuli. Mtokoso wa bamia hutibu kichwa na Arthritis. Bamia zina nyuzinyuzi kwa wingi na maji zinafaa sana kwa wale wenye tatizo la kuto pata choo vizuri na gesi ya tumboni kutoka vizuri kwa njia ya kinyesi . Bamia ni kilainishi kizuri cha tumbo zitumiwe mara kwa mara. Bamia zinalainisha ngozi zinafanya usipate chunusi nk. Tumia bamia ambazo hazija komaa sana na zilizo chumwa ndani ya siku tatu zaidi ya hapo usitumie.
Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopoza na Tiba.
Mazingira Natural Products
S.L.P 1338 Mbeya
Mob:+255719564276-0754807401
Email:mnp,kaka@gmail.com     
Blogu:maziniranp.blogspot.com