Komamanga
ni moja ya matunda yenye faida kwa afya ya binadamu. Komamanga limekuwa
likilimwa kwa miaka zaidi ya 5000 iliyopita huko mashariki ya kati. Komamanga
linakua hadi kufikia kimo cha Meta 5 -10 kutegemea eneo. Jina la kibotania
huitwa Punica granatum linn. Waingereza
huita Pomegranate. Hulimwa sana nchini India. Pia hili ni tunda
linalopatikana sana Afrika Mashariki. Tunda la komamanga lina protini,
nyuzinyuzi, wanga, calcium magnesium, oxalic acid , phosphorus, chuma,
sodium,potassium, shaba, sulphur, chlorine, Vitamin A, vitamin B1, B5, Vitamin
E, riboflavin, Nicotinic acid na vitamin C. komamanga ni chanzo kizuri cha sukari, (glucose na
Fructose), vitamin C na chuma,. Pia komamanga lina utajiri mkubwa wa kuleta
nguvu mwilini. Juisi ya komamanga lililoiva ni nzuri kwa Homa ya matumbo,
Gastric na Homa za pumu. Juisi ya komamanga ni nzuri kwa wenye high blood
pressure kwani inapunguza hali hiyo. Juisi ya komamanga ikichanganywa na Asali
ni nzuri kwa wenye umri mkubwa kwa ajili
ya kuimarisha kumbu kumbu iliyopotea. Upungufu
wa damu changanya juisi ya tunda la komamanga kikombe kimoja cha chai,
¼ tsp mdalasini na Asali 3tsp na kunywa.
Pumu na kikohozi changanya juisi ya komamanga, Tangawizi mbichi na Asali kwa
kiwango sawa. Tumia kijiko cha chakula mara mbili kwa siku. Mbegu za tunda
changanya pilipilimanga na chumvi kidogo mpatie mgonjwa wa homa ya manjano.
Juisi ya komamanga na ndimu pamoja ikitumiwa mara tatu kwa siku ni nzuri kwa
matatizo ya Ini na homa ya manjano. Komamanga hutibu matatizo ya njia ya mkojo
, Juisi ya ya tunda hilo husaidia kuponya saratani, husaidia mtiririko wa damu
kwenda vizuri kwenye mishipa. Hali hiyo husaidia kupunguza hatari ya magonjwa
ya moyo, shinikizo la damu, na kiharusi, ulaji wa mara kwa mara wa tunda hilo
huzuia meno kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu na
maambukizi ya virusi ndani ya mwili, husaidia pia kutibu maradhi ya tumbo
ikiwamo kutopata haja kubwa, komamanga husaidia kuondoa sumu mwilini, kupambana
na tatizo la uzito, komamanga hutibu magonjwa ya muda mrefu kama saratani ya
tezi dume, saratani mbalimbali, kisukari, baridi yabisi na jongo (gout), kuweka
sawa mfumo wa chakula na njia ya usagaji wa chakula. Mbegu za komamanga, magome
na mizizi yakichemshwa na maji ni dawa
ya minyoo aina tapeworms. Gome na ganda la ndani la komamanga (Rind) ni dawa ya
kuwasha ngozi na koo. Pia hutumika kuosha utupu wa mwanamke unaowasha na kuweka
vizuri cervic. Juisi ya komamanga ni nzuri
kwa wenye umri mkubwa kwa Figo na kibofu cha mkojo kuwa na nguvu za
kufanya kazi vizuri. Kuharisha damu: tumia juisi ya majani mabichi machanga.
Maganda ni tiba ya kuharisha na kuhara damu. Majani na maua hutibu virusi vya
macho (conjuctivities virus). Magome hutibu bandama, vidonda vya koo, homa na
leucorrhea yakichemshwa. Saga mbegu na weka ndani ya maziwa hutibu mawe katika
figo. Dozi ya magome, majani au maua tumia gramu 10 hadi 15 katika lita ya
maji. Pia tunatoa ushauri, mafuta ya waliopooza na tiba zingine.
Mazingira
Natural Product
Simu:
+255754807401/- 0719 564 276
Barua
pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment