Nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu
muumba wa mbingu na ardhi kwa kuendelea kunipa afya njema pamoja na wewe
msomaji wa Gazeti hili. Hakika ni jambo la pekee ambalo Mungu ametutunuku kwa
maana wapo hospitalini wakitafuta huduma kwa ajili ya afya zao. Bamia ni mboga
iliyotokea kupendwa miongoni mwa wa watanzania wengi pengine kwa kutotambua au
kutambua umuhimu wake kwa afya ya binadamu.
Bamia hulimwa katika nchi za Tropiki
na nusu Tropiki. Jina Bamia limetokana na jina Bamya asili yake nchi ya waThai
(Thailand)
Nasisi
watanzania tunaita BAMIA. Jina la kibotania huitwa Abelmoschus esculents au
hibiscus esculents linn. Waingereza huita Okra au lady fingers.Bamia ina wanga
, mafuta , protini, sodium, folate , calcium, magnesium,Vitamini A na C. Bamia ikiliwa
mara kwa mara hupunguza sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa
KISUKARI. Bamia ikilo wekwa usiku kucha kwenye maji na kunywewa hupunguza lehemu (cholesterol) na kuweka sawa
sukari mwilini. Bamia ikipondwa na kuwa rojo inafaa kupaka vidonda vya kuungua na
matatizo ya ngozi . Bamia ina MUCIN inayolinda matatizo mengi yanayotokea ndani
ya tumbo na utumbo kwa hiyo ikiliwa utakuwa na afya njema kila wakati. Mtokoso wa
bamia ambazo hazija komaa sana hutibu maumivu ya mucous membrane inayosababisha
matatizo ya upumuaji. Juisi ya Bamia hutibu maumivu ya koo yanayo sababishwa na
kikohozi. Mtokoso wa majani, matunda yake hutibu mfumo wa ukojoaji kwa wanaume na
wanawake kama maumivu ya mkojo unapokojoa, Kaswende na kisonono. Majani na mizizi
ikipondwa na kupakwa vidonda hupona haraka. Juisi ya bamia hutibu homa , kuharisha
na maumivu ya tumbo . Juisi ya bamia hutibu muwasho wa ngozi na ni“moisturizer”
ya ngozi. Bamia zikiliwa mara kwa mara zinasaidia kwa wale wanaowahi kufika kileleni
wakati watendo la ndoa. Bamia zikiliwa mara
kwa mara huima risha na kuboresha kumbukumbu nakuufanya uti wa mgongo ufanye kazi yake vizuri . Mbegu za bamia zikikaangwa
nakusagwa hutumika kama chai na kuongeza utokaji wa jasho. Mbegu za bamia hutibu
mwako wa misuli. Mtokoso wa bamia hutibu kichwa na Arthritis. Bamia zina nyuzinyuzi
kwa wingi na maji zinafaa sana kwa wale wenye tatizo la kuto pata choo vizuri na
gesi ya tumboni kutoka vizuri kwa njia ya kinyesi . Bamia ni kilainishi kizuri
cha tumbo zitumiwe mara kwa mara. Bamia zinalainisha ngozi zinafanya usipate chunusi
nk. Tumia bamia ambazo hazija komaa sana na zilizo chumwa ndani ya siku tatu zaidi
ya hapo usitumie.
Pia
tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopoza na Tiba.
Mazingira
Natural Products
S.L.P
1338 Mbeya
Mob:+255719564276-0754807401
Email:mnp,kaka@gmail.com
Blogu:maziniranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment