Ndizi
ni zao moja kati ya mazao ya matunda ambayo huzallishwa kwa wingi katika mikoa
ya Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Kigoma, Tanga, Kagera na Mara. Jina la
Kibotania linaitwa Musa paradisiaca na Kingereza huitwa banana. Wandali huita Indunye na Wanyakyusa huita
Amabifu /Amatoki, zao hili hutumika kama zao la chakula na tunda pia. Kando ya
kula kama chakula tu, kuna malighafi nyingine tele katika mmea huu inayoweza
kuufaidisha mwili wa binadamu kama tiba kwa magonjwa mbalimbali. Asili au tabia
ya mmea huu inanukia, imetulia, kizuia vidonda, kiongeza mkojo na ni kiamshi. Ndizi ina vitamin, Virutubisho vya kuleta nguvu
pamoja na aina nyingi za lishe muhimu. Pia ina madini ya chuma, potassium,
Calcium, Sodium, Magnesium, Shaba, Manganese, Phosphorus, Sulphur, Silica, na
Chlorine nk. Ndizi husaidia katika kuboresha hali za watu kwa maana zina
kemikali za serotonin “na” dopamine” ambazo humfanya mtu kujisikia vizuri. Ndizi hutibu athari zinazotokana na pombe kwa
kusawazisha Msukumo wa damu (kwa msaada wa potassium) pamoja na kuzuia
kiungulia. Maua ya ndizi hupunguza
utokaji wa damu nyingi wakati wa hedhi kwa kuyaponda ponda na kunywa. Maua huuchemshwa na kuliwa na wenye kisukari.
Pia utomvcu wake ni dawa ya kutia sikio linalouma. Ndizi mbivu ikipondwa na
kuchanganywa na maziwa, sukari ni nzuri kwa kukuza watoto. Ndizi mbivu ikichanganywa
na ukwaju na chumvi kidogo ni tiba nzuri kwa hatua za mwanzo za kuharisha na kuharisha
damu. Wale wanaosumbuliwa na usagaji wa chakula ni vizuri watumie ndizi na kikombe
kimoja cha maziwa wakati wanaenda kulala. Wale wenye bawasiri waponde ndizi na
kuzichemsha pamoja na maziwa kikombe kimoja na watumie mara tatu kutwa. Hutibu
kikohozi kwa kuchanganya na pilipili manga kidogo na kula mara tatu kutwa. Wenye
kifua kikuu waponde ndizi na kuchanganya na
nusu kikombe cha maziwa ya mgando yaliyo salama, kijiko cha chai cha asali na
kikombe kimoja cha maji ya dafu (nazi) na kutum,ia mara mbili kwa siku. Homa ya
manjano na homa ya matumbo waponde ndizi na kuchanganya na kijiko cha chakula
cha asali wale mara mbili kutwa kwa siku kadhaa. Majivu ya maganda ya ndizi ni
tiba nzuri kwa vidonda. Ndizi mbichi unga wake ni lishe nzuri kwa wenye
kisukari na wale wenye kuvuja damu wenye shida usagaji wa chakula, na wenye
asidi tumboni. Majani mabichi hutumika kutibu macho yanayouma na kutuliza
maumivu ya kichwa pia ponda majani na kuweka juu ya kidonda. Majivu ya shina la
mmea ni tiba nzuri kwa wenye vidonda. Juisi
ni nzuri kwa wenye shida ya mishipa ya
fahamu, kuharisha, kuharisha damu na manjano. Pia inazuia damu isitoke katika
vidonda vya kujikata nk. Mizizi ni tiba nzuri kwa maumivu ya ngozi laini ya
njia ya mkojo na ya uzazi/uke. Mizizi iliyochujwa na kuongeza asali ni tiba ya
kubanwa kwa ini na mlinzi mzuri wa ini. Utumiaji wa ndizi mbivu mara kwa mara
huondoa tatizo la kufunga choo, udhaifu wa mwili na vidonda vya tumbo. Pia
ukila ndizi mbili zina kutosha kukupatia nguvu za kufanya kazi ngumu kwa muda
wa dakika tisini. Ndizi hutumika kwa matumizi mbalimbali kama Ugali, Chips nk.
MAZINGIRA NATURAL PRODUCTS
MBEYA
Simu:
+225 754 807 401 +255 719 564 276
Blogu:
mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment