Pages

Saturday, May 26, 2018

HIVI VINAONGEZA NGUVU ZA KIUME

Asparagus
Broccoli








         





Leo nitaeleza maelezo ya aina gani ya vyakula ambavyo husaidia kuongeza idadi ya mbegu za kiume zenye afya na ujazo wake na faida zingine za afya ya uzazi.
Mboga ijulikanayo kama Asparagus Officinalis ambayo huwa na kiasi kikubwa cha vitamin C ambayo ina wigo mkubwa katika kusaidia utengenezwaji wa mbegu za kiume.
Vitamini C hutoa ulinzi kwa seli zilizopo katika kokwa za kiume (korodani) zisidhuriwe na radiko huru (Free radicals), hivyo kufanya kiwanda cha mbegu za kiume kutengeneza mbegu zenye afya na zenye uwezo wa kupiga mbizi kwa kasi.
Broccoli ni aina ya mboga ambazo zipo hapa nchini ingawa watanzania wengi hatuli, ila katika migahawa ya magharibi na ya kichina. Broccoli ina kiasi kikubwa cha foliki ambayo hujulikana pia kama vitamin B9. Vitamini B9 ilishajulikana kwa kusaidia wanawake waliokuwa wagumba kuweza kushika mimba, kwa sasa pia inajulikana kusaidia wanaume wagumba.
Spinachi ni moja ya mboga mboga ambayo inakubalika kusheheni tindikali ya foliki ambayo ni muhimu sana katika utengenezwaji wa mbegu za kiume. Ingawa mboga zote za kijani zinakubalika kutokana na kusheheni vitamini mbalimbali.
Pale mwanaume anapokuwa na kiwango kidogo cha folate husababisha kuzalisha mbegu za kiume zisizotimilifu. Mbegu za namna hii zinakua na wakati mgumu katika kufikia na kupenya katika tando za kijiyai cha kike wakati wa Urutubishaji.
Hali kama hii inaweza kusababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye hitilafu za kimaumbile kwa sababu ya kijiyai cha kike kurutubishwa na mbegu yenye hitilafu.
Tunda lijulikanalo kama komamanga ambalo lipo pia katika jamii yetu linajulikana kusaidia kutengenezwa idadi kubwa ya mbegu zenye ubora ndio maana wahindi hutumia sana.
Ndizi ni moja ya tunda ambalo limesheheni vitamin A, B1 na C ambazo husaidia mwili kutengeneza mbegu za kiume zenye afya na vilevile kuongeza wingi wa mbegu hizo.
Pia, Ndizi huwa na kimeng’enya aina ya Bromelain ambacho huzuia mlipuko wa kinga ya mwili, hivyo kusaidia kuongezeka wingi wa mbegu za kiume pamoja na kasi yake.
Mayai ni moja ya vyakula vinavyokubalika kusaidia kuongeza wingi wa mbegu za kiume na vilevile kusaidia kuongeza kasi ya mbegu za kiume.
Kutokana na mayai kusheheni vitamin E na Protini ambavyo vyote kwa pamoja husaidia kulinda mwili kutoka kwa sumu za radiko ambazo hupunguza wingi wa mbegu za kiume.
Vilevile virutubisho hivyo vilivyopo katika mayai husaidia kutengenezwa kwa mbegu imara zeneye afya jambo ambalo ni muhimu kwa Urutubishwaji wa kijiyai cha kike.
Chocholate yenye rangi ya kahawia iliyokolea inajulikana zaidi duniani, sababu kubwa ni kutokana na aina hii ya chocolate kuwa na Tindikali ya amino (Protini) ijulikanayo kama L-Arginine HCL ambayo husaidia kuongeza ujazo wa mbegu za kiume na wingi wake. Vilevile huongeza msisimko wa kilele cha tendo la ndoa.
Nyanya chungu au Ngogwe nazo husaidia sana kuimarisha tendo la ndoa zikitumiwa mara kwa mara.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

KULA KABEJI YA ZAMBARAU NA MNAVU UEPUKANE NA VIDONDA VYA TUMBO


Je nitajuaje kama nina Vidonda vya Tumbo?
Dalili za ugonjwa wa tumbo,
i)kuchoka choka sana bila sababu maalum, Mgongo kuuma, kiuno, kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia,
Kizunguzungu, kukosa usingizi  au kulala mara kwa mara .  Maumivu makali chini ya kifua  kwa ndani kama kwamba  unachomwa na kitu chenye ncha kali , maumivu hayo wakati mwingine  mgongoni ambapo huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali  wengi huita chembe chembe ya moyo. Dalili zingine kichefu chefu, kiungulia, tumbo kuwaka moto, maumivu makali sehemu kilichopo kidonda,  kukosa choo na kupata choo kigumu na chenye kukatika katika kama choo cha mbuzi, shida ya moyo,  kutapika nyongo, kutapika damu au kuharisha, sehemu za mwili kupata ganzi hasa  miguu na mikono. Dalili nyingine ni kukosa hamu ya kula, kula kupita kawaida, kusahausahau na hasira. Kwa kweli ni vigumu kueleza maelezo yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mgonjwa  aliye sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokwambia ni kizima.
Vipimo vya vidonda vya tumbo.
ii)Njia iliyo sahihi na nzuri zaidi ni kupima kwa daktari kipimo kiitwacho barium meal x-ray, Endoscopy au H.Pylori test.
Ulaji wa kabeji na kutengeneza juisi yake utakuepusha kupata vidonda vya tumbo. Pia unapokula mboga ya mnavu wasafwa  huita sungwe utaepukana na kupata vidonda vya tumbo wasafwa hula mboga za kabeji na mnavu mara kwa mara wengi wao hawana matatizo ya vidonda vya tumbo.

LEONOTIS NEPETIFOLIA MMEA UNAO TIBU KIHEREHERE CHA MOYO NA MAPIGO YASIYO YA KAWAIDA


 Nilipokuwa kwenye shughuli zangu za utafiti wa mimea 4/6/2017. Niliona mimea aina ya LEONOTIS NEPETIFOLIA maua yake yakiwa yamezungukwa na nyuki wengi sana wakitafuta chakula. Nyuki hao ndiyo walionifanya niandike makala fupi ya mmea huu.
Leonotis Nepetifolia una majina mengine kama Annual lion’s ear, lion’s ear, klip dagga, gran tiparani, Flor de mundo, mota, Christmas candlestick, shandilay, na bradi-bita. Mmea huu hukua kutoka mita moja mpaka tatu. Mbegu zake husambazwa na maji, matope sehemu yauamopita magari na wanyama.
Leonotis Nepetifolia una alkaloids (leonurine na stachydrene), Iridoid glycoside (Leonuride), Iridoid glycosides (leonurin and leonuridine) diterpenoids (leocardin), flavonoids (rutin, quercetin, hyperoside, apigenin), volatile oil, tannins na vitamin A.
Mmea huu maua yake hupendwa sana na wachunga ng’ombe na vijana huko vijijini wananyonya maji matamu yaliyomo ndani ya maua yaani nectar.
Majani hutibu matatizo ya tumbo, kuuma tumbo, arthritic, kisukari aina ya-2 diabetes mellitus, kizuia pumu, kuzuia kuharisha, homa, malaria, kikohozi, womb prolapsed, kutuliza kiherehere cha moyo, hufanya moyo uwe na nguvu katika utendaji wa kazi, tachycardia, mapigo yasiyo ya kawaida ya moyo (irregular heart beats), kuongeza utokaji wa mkojo, uvimbe, thrush, plasta kwenye vidonda na kaswende. Mchemko wa majani na ukanywewa hutibu kuwasha na magonjwa ya ngozi.
Mizizi hutibu matatizo ya Tumbo. Kwa wale wanaoshughulika na mambo ya nyuki na Asali mmea huu unafaa sana kuwa chanzo cha kupata Asali nzuri.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

MAAJABU YA KARANGA PORI KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI



 Zao la karanga pori ni miongoni mwa zao lisilopewa kipaumbele sana hapa Tanzania, zamani wakati wa ujana wangu, bibi mzaa mama alipanda miti miwili, ilikuwa inakuwa na karanga nyingi tulikuwa tunakula bila kujua faida yake kwa mwili wa binadamu.
Mama mkwe wangu Tamali Mwasomola amepanda miti mitatu na ukifika msimu wa karanga watoto huja kununua.
Miaka ya hivi karibuni kampuni ya maparachichi Rungwe na Enterprise works walikuwa wakihamasisha wananchi wa mkoa wa Mbeya kupanda karanga pori zinazoanza kuzaa kwa muda mfupi tofauti na zingine.
Asili ya karanga pori ni Australia. Pia nchi zingine zinazolima kwa wingi ni Brazil, Indonesia, Kenya, New Zealand na Afrika kusini. Karanga pori ya Hawaii ina ladha nzuri, kuna aina saba ya karanga pori, lakini zinazoliwa ni aina mbili.
Ø  Majina ya kibotania huitwa Macadamia Integrifolia na  Macadamia Tetraphylla, waingereza huita Macadamia Majina mengine huitwa Australia nut, Queen sland nut na Bush nut.
 . Nchini Kenya wanaita Njugu ya macadamia. Hapa Tanzania hustawi sehemu za Rungwe, Ifakara, Morogoro, Kilolo, Arusha, Hai na Lushoto nk.
Karanga pori ina vitamin A, Protini, Chuma, Thiamin, rifboflavin, niacin,folates, zinki, shaba, calcium,phosphorus,potassium na magnesium. Karanga pori ina kizuia Oxidants kama polyphenols, Amino acids, flavones na selenium. Pia kuna sucrose, fructose, glucose na maltose nk.
Faida zitokanazo na kula mara  kwa mara karanga pori ni kukinga magonjwa ya moyo (Heart Disease) kwa kuondoa lehemu, kupunguza uzito, kuimarisha afya ya mifupa, inaboresha akili ukichanganya na maziwa pia zabibu. Ina nyuzi lishe inayosaidia umeng’enyaji wa chakula tumboni na kuondoa ukosefu wa kwenda haja kubwa kwa shida, ina mafuta ya Oleic acid yanayohamasisha kuwa na kumbukumbu nzuri.
Hufanya seli na tishu za mwili ziwe na nguvu, Hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, saratani na arthritis kwa kuwa kuna omega – 3 na Omega – 6 fatty acids, kuondoa radiko huru (free radicals) ambayo husababisha magonjwa ya saratani ya matiti, kizazi na saratani ya Tezi dume. Huchelewesha ngozi kuzeeka haraka, Huzuia ugonjwa wa trans- epidermal water loss (TEWL), Hulinda ngozi na nywele zisiharibirike haraka, Huzuia kukatika ovyo kwa nywele zisiharibike haraka, inasaidia kuboresha afya kwa wale waishio na VVU na Ukimwi hasa kwa kuongeza kinga ya mwili na karanga pori, hutumika kutengenezea mafuta ya kula, kuongeza ladha kwenye chokoleti, ice cream, keki, sherbets, maandazi, brittles, candies, mafuta ya kupaka mwili na mafuta ya nywele.
Pia karanga pori huliwa zikiwa mbichi, kavu au kuchoma kwenye moto.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com




FAIDA YA NDIZI


 Ndizi ni zao moja kati ya mazao ya matunda ambayo huzallishwa kwa wingi katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Kigoma, Tanga, Kagera na Mara. Jina la Kibotania linaitwa Musa paradisiaca na Kingereza huitwa banana.  Wandali huita Indunye na Wanyakyusa huita Amabifu /Amatoki, zao hili hutumika kama zao la chakula na tunda pia. Kando ya kula kama chakula tu, kuna malighafi nyingine tele katika mmea huu inayoweza kuufaidisha mwili wa binadamu kama tiba kwa magonjwa mbalimbali. Asili au tabia ya mmea huu inanukia, imetulia, kizuia vidonda, kiongeza mkojo na ni  kiamshi. Ndizi  ina vitamin, Virutubisho vya kuleta nguvu pamoja na aina nyingi za lishe muhimu. Pia ina madini ya chuma, potassium, Calcium, Sodium, Magnesium, Shaba, Manganese, Phosphorus, Sulphur, Silica, na Chlorine nk. Ndizi husaidia katika kuboresha hali za watu kwa maana zina kemikali za serotonin “na” dopamine” ambazo humfanya mtu kujisikia vizuri.  Ndizi hutibu athari zinazotokana na pombe kwa kusawazisha Msukumo wa damu (kwa msaada wa potassium) pamoja na kuzuia kiungulia. Maua ya ndizi  hupunguza utokaji wa damu nyingi wakati wa hedhi kwa kuyaponda ponda na kunywa.  Maua huuchemshwa na kuliwa na wenye kisukari. Pia utomvcu wake ni dawa ya kutia sikio linalouma. Ndizi mbivu ikipondwa na kuchanganywa na maziwa, sukari ni nzuri kwa kukuza watoto. Ndizi mbivu ikichanganywa na ukwaju na chumvi kidogo ni tiba nzuri kwa hatua za mwanzo za kuharisha na kuharisha damu. Wale wanaosumbuliwa na usagaji wa chakula ni vizuri watumie ndizi na kikombe kimoja cha maziwa wakati wanaenda kulala. Wale wenye bawasiri waponde ndizi na kuzichemsha pamoja na maziwa kikombe kimoja na watumie mara tatu kutwa. Hutibu kikohozi kwa kuchanganya na pilipili manga kidogo na kula mara tatu kutwa. Wenye   kifua kikuu waponde ndizi na kuchanganya na nusu kikombe cha maziwa ya mgando yaliyo salama, kijiko cha chai cha asali na kikombe kimoja cha maji ya dafu (nazi) na kutum,ia mara mbili kwa siku. Homa ya manjano na homa ya matumbo waponde ndizi na kuchanganya na kijiko cha chakula cha asali wale mara mbili kutwa kwa siku kadhaa. Majivu ya maganda ya ndizi ni tiba nzuri kwa vidonda. Ndizi mbichi unga wake ni lishe nzuri kwa wenye kisukari na wale wenye kuvuja damu wenye shida usagaji wa chakula, na wenye asidi tumboni. Majani mabichi hutumika kutibu macho yanayouma na kutuliza maumivu ya kichwa pia ponda majani na kuweka juu ya kidonda. Majivu ya shina la mmea ni tiba nzuri kwa wenye  vidonda. Juisi ni nzuri kwa wenye shida  ya mishipa ya fahamu, kuharisha, kuharisha damu na manjano. Pia inazuia damu isitoke katika vidonda vya kujikata nk. Mizizi ni tiba nzuri kwa maumivu ya ngozi laini ya njia ya mkojo na ya uzazi/uke. Mizizi iliyochujwa na kuongeza asali ni tiba ya kubanwa kwa ini na mlinzi mzuri wa ini. Utumiaji wa ndizi mbivu mara kwa mara huondoa tatizo la kufunga choo, udhaifu wa mwili na vidonda vya tumbo. Pia ukila ndizi mbili zina kutosha kukupatia nguvu za kufanya kazi ngumu kwa muda wa dakika tisini. Ndizi hutumika kwa matumizi mbalimbali kama Ugali, Chips nk.

MAZINGIRA NATURAL PRODUCTS
MBEYA
Simu: +225 754 807 401 +255 719 564 276
Barua pepe: mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com