Je nitajuaje kama nina Vidonda vya Tumbo?
Dalili za ugonjwa wa tumbo,
i)kuchoka choka sana bila sababu maalum, Mgongo
kuuma, kiuno, kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia,
Kizunguzungu, kukosa usingizi au kulala mara kwa mara . Maumivu makali chini ya kifua kwa ndani kama kwamba unachomwa na kitu chenye ncha kali , maumivu
hayo wakati mwingine mgongoni ambapo
huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali wengi huita chembe chembe ya moyo. Dalili
zingine kichefu chefu, kiungulia, tumbo kuwaka moto, maumivu makali sehemu
kilichopo kidonda, kukosa choo na kupata
choo kigumu na chenye kukatika katika kama choo cha mbuzi, shida ya moyo, kutapika nyongo, kutapika damu au kuharisha,
sehemu za mwili kupata ganzi hasa miguu
na mikono. Dalili nyingine ni kukosa hamu ya kula, kula kupita kawaida, kusahausahau
na hasira. Kwa kweli ni vigumu kueleza maelezo yote apatayo mgonjwa wa vidonda
vya tumbo hasa kwa mgonjwa aliye sugu kwani
hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokwambia ni kizima.
Vipimo vya vidonda vya tumbo.
ii)Njia iliyo sahihi na nzuri zaidi ni kupima kwa
daktari kipimo kiitwacho barium meal x-ray, Endoscopy au H.Pylori test.
Ulaji wa kabeji na kutengeneza juisi yake
utakuepusha kupata vidonda vya tumbo. Pia unapokula mboga ya mnavu wasafwa huita sungwe utaepukana na kupata vidonda vya
tumbo wasafwa hula mboga za kabeji na mnavu mara kwa mara wengi wao hawana matatizo
ya vidonda vya tumbo.
No comments:
Post a Comment