Zao la karanga pori ni miongoni mwa zao
lisilopewa kipaumbele sana hapa Tanzania, zamani wakati wa ujana wangu, bibi
mzaa mama alipanda miti miwili, ilikuwa inakuwa na karanga nyingi tulikuwa
tunakula bila kujua faida yake kwa mwili wa binadamu.
Mama mkwe wangu Tamali Mwasomola
amepanda miti mitatu na ukifika msimu wa karanga watoto huja kununua.
Miaka ya hivi karibuni kampuni ya
maparachichi Rungwe na Enterprise works walikuwa wakihamasisha wananchi wa mkoa
wa Mbeya kupanda karanga pori zinazoanza kuzaa kwa muda mfupi tofauti na
zingine.
Asili ya karanga pori ni Australia.
Pia nchi zingine zinazolima kwa wingi ni Brazil, Indonesia, Kenya, New Zealand
na Afrika kusini. Karanga pori ya Hawaii ina ladha nzuri, kuna aina saba ya
karanga pori, lakini zinazoliwa ni aina mbili.
Ø Majina ya kibotania huitwa Macadamia
Integrifolia na Macadamia Tetraphylla,
waingereza huita Macadamia Majina mengine huitwa Australia nut, Queen sland nut
na Bush nut.
. Nchini Kenya wanaita Njugu ya macadamia. Hapa
Tanzania hustawi sehemu za Rungwe, Ifakara, Morogoro, Kilolo, Arusha, Hai na
Lushoto nk.
Karanga
pori ina vitamin A, Protini, Chuma, Thiamin, rifboflavin, niacin,folates,
zinki, shaba, calcium,phosphorus,potassium na magnesium. Karanga pori ina
kizuia Oxidants kama polyphenols, Amino acids, flavones na selenium. Pia kuna
sucrose, fructose, glucose na maltose nk.
Faida
zitokanazo na kula mara kwa mara karanga
pori ni kukinga magonjwa ya moyo (Heart Disease) kwa kuondoa lehemu, kupunguza
uzito, kuimarisha afya ya mifupa, inaboresha akili ukichanganya na maziwa pia
zabibu. Ina nyuzi lishe inayosaidia umeng’enyaji wa chakula tumboni na kuondoa
ukosefu wa kwenda haja kubwa kwa shida, ina mafuta ya Oleic acid
yanayohamasisha kuwa na kumbukumbu nzuri.
Hufanya
seli na tishu za mwili ziwe na nguvu, Hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya
moyo, saratani na arthritis kwa kuwa kuna omega – 3 na Omega – 6 fatty acids,
kuondoa radiko huru (free radicals) ambayo husababisha magonjwa ya saratani ya
matiti, kizazi na saratani ya Tezi dume. Huchelewesha ngozi kuzeeka haraka,
Huzuia ugonjwa wa trans- epidermal water loss (TEWL), Hulinda ngozi na nywele
zisiharibirike haraka, Huzuia kukatika ovyo kwa nywele zisiharibike haraka,
inasaidia kuboresha afya kwa wale waishio na VVU na Ukimwi hasa kwa kuongeza
kinga ya mwili na karanga pori, hutumika kutengenezea mafuta ya kula, kuongeza ladha
kwenye chokoleti, ice cream, keki, sherbets, maandazi, brittles, candies,
mafuta ya kupaka mwili na mafuta ya nywele.
Pia
karanga pori huliwa zikiwa mbichi, kavu au kuchoma kwenye moto.
Na kadri
mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na
anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment