Katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, tende ndio tunda
linaloliwa kwa wingi,pengine kuliko tunda linguine. Pamoja na kuwa ni tunda
lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia lime thibitika kusheheni
madini na vitamin lukuki, hivyo kuwa na faida nyingi kiafya. Katika makala hii,
nimekuorodheshea faida 10 za tende:
1. Ukila
tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za
kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hilo.
2. Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha
protini na vitamin B1,B2, B3,B5, A1na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa
ustawi wa afya ya mwili kwa ujumla.
3. Ulaji
wa tende huimalisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo
utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu
kinacho sababisha maumivi wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna
virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo
ni muhimu mwilini.
4. Ukila
tende, mwili utapata nguvu na kuondolea uchofu ndani ya nusu saa, kwasababu
tende ina virutubisho vya asili kama vile ‘glukosi’
‘sucrose’na fructose’. Ili kupata faida za tende, changanya na maziwa fresh
kasha kula. Pindi unajisikia mchofu, badala ya kunywa vinywaji baridi
vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa
wafunga saumu, ina shauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kurejesha mwili
wako nguvu, iliyopotea siku nzima.
5. Tende
ina madini pia aina ya ‘potassium’ na
kiasi kidogo cha chumvi (sodium).
Madini haya husaidia uimarishwaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua
kwamba ulaji wa vyakula vinavyotengeneza ‘potassium’
huweza kumwepusha mtu kupatwa na kiharusi (stroke).
Pia tende husaidia kupunguza cholesterol
mwilini na LDL Cholesterol.
6. Kwa
wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), waweza kupata haueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina
kiwango chakutosha cha madini ya chuma ambayo huitajika utengenezaji wadamu
mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji
wa meno.
7. Kwa
tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye
maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kasha asubuhi changanya maji hayo pamoja
na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka na kuwa laini.
8. Kwa
matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalumu wa tende, maziwa,
asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja
kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae
usiku kucha.
Asubuhi, sisage tende kwenye maziwa hayo hadi
zichanganyike, kasha weka asali kiasi cha vijiko vitatu ua vine vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha
nusu kijiko kidogo, Kisha kunywa mchanganyiko huo kila siku hadi utakapoona
mabadiliko ya kuridhisha.
9 Tende ni
dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka
kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina
mana kwamba, wale wanahitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi
kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.
10 Tende inatibu
saratani ya tumbo. Hata hivyo tende ni tiba kama tiba nyingine na haina
madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia
na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha
nuru ya macho na tatizo la kuona usiku (night blindness).
Kwa ujumla faida
za tende ni nyingi na unaweza kuila
tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya
na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila
siku ili ujipatie faida hizo 10 na nyingine.
No comments:
Post a Comment