Wanyakyusa na wandali
huita takapela au kasokela. Ni mti
wenye urefu wa hadi meta 20. Asili
yake ni amerika ya
kusini katika nchi
ya Mexico na nyingine. Wenyeji wa Mexico wa Aztec
neno Avocado lenyewe linatokanana na
neno la Nahuatl ‘ahuacatl’ ni kifupi cha neno la kia-Aztec ‘ahuacacuahatl’
likimaanisha mti wa kende/korodani (testicle tree). Parachichi lilipelekwa Ulaya
na wahispania walioenda Amerika ya
kusini miaka mingi iliyopita. Hapa Tanzania parachichi lililetwa na wajerumani na waingereza kwa nyakati tofauti. Hapa nchini ni
watu wachache wanaojua faida za mti huu. Tunashukuru kwa hapa Tanzania, Chuo kikuu
cha Sokoine, Tengeru na taasisi ya utafiti ya kilimo Uyole Mbeya
zinafundisha na kuzalisha parachichi
zinazokua kwa muda mfupi kuanzia miaka
miwili na nusu na kuendelea kwa njia ya kupandikiza ‘grafting’. Parachichi
(Avocado) ni mojawapo ya matunda ambayo yanatunza na kukuza mwili. Yana vitamini
nyingi sana, madini na pia mafuta halisi yanayopatikana kwenye vyakula, yaani yasiyotengenezwa na binadamu parachichi
ina madini, nyuzi na vitamini. Parachichi lina ubora wa vitamin C, B6 na E
ambazo ni vitamini muhimu sana za kukuza mwili na pia kwa afya ya ngozi. Vitamini B6, ukosefu wa
vitamin hii huleta kufadhaika yaani “mood swings”. B6 pia husaidia kupunguza maumivu yanayoletwa na hedhi yaani ‘Premenstrual stress’ PMS. Vitamin C ni
muhimu kwa kuponya vidonda vya ngozi pia
husaidia mwili kujikinga na magonjwa
kama mafua na ugonjwa wa kuvimba ufizi unaotoa damu yaani ‘scurvy’. Parachichi ni bora kwa
watu walio katika
hali ya kupona baada
yakuugua na wale wanaougua pia. Vitamini
E hupunguza kuchoka kwa akili na
kuongeza tukio la uzazi (Upungufu wa nguvu za
kiume). Vitamini hii pia ni
muhimu kwa afya ya ngozi. Madini K+ ni muhimu sana kwa
maisha ya chembechembe za
mwili ‘Cells’. K+ ni muhimu kwa afya kwa sababu upungufu wake huleta ugonjwa wa kujisikia
mlegevu au kupungukiwa na nguvu. Madini
ya parachichi ni muhimu kwa kukuza mtoto
aliye bado tumboni mwamaake. Parachichi
pia matukio ya saratani furani haswa
zile za mdomo na kishimo kilicho nyuma
ya pua, kinywa na koromeo (yaani pharynx) na pia ugonjwa wa moyo. Parachichi
ina manufaa kwa mzuguko wa damu mwilini. Majani machanga ni dawa ya kikohozi,
yakitokoswa kwenye maji na
yaliyokauswa kijani nyeusi ni dawa ya kuharisha. Majani huongeza damu mwilini [anemia], kuumwa kichwa, koo, tumbo,
uchovu, kuimarisha meno na kuondoa maumivu. Maganda [barks] yanafaa kwa
kutengeneza dawa rheumatism kwa kuchanganya na mafuta ya mboga mboga. Peke la parachichi
ni rafiki mkubwa wa moyo wa binadamu, majipu,
kuimarisha kinga ya mwili na shida ya mkojo
kukwama. Parachichi hutumiwa vizuri hufanya kazi ya kuokoa nywele zinazoanguka (upaa) kama litapakwa pale na husaidia
kukuza nywele zinazodumaa (dandruff). Pia
hutumika kwenye vipodozi mbalimbali. Parachichi
hutumika kwa kutengenezea kinywaji cha
parachichi. Kupaka kwenye mkate, ndizi, viazi, magimbi, kutengeneza kachumbali
,guacamole, avocado na saradi ya nyanya, na avocado spread.
Tunapenda
kila famiilia kutumia parachichi katika mlo ili kuboresha afya zetu.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya
ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali
ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali
wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi
(Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa
hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,
vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine
mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment