Pages

Sunday, August 24, 2014

MAAJABU YA WITHANIA SOMNIFERA. Wasukuma wanauita MTEMUA SHIMBA




Withania somnifera (winter cherry) unastawi kwa mtindo wa vichaka na kukua hadi kufikia kimo cha mita 1.5 (moja na nusu ). Huzaa matunda ambayo yakikomaa huwa mekundu na mbegu zake huwa za njano. Mmea huu una alkaloid somniferine. Mizizi yake ina mafuta ( essential oil) pia ina madini ya potassium nitrate na glucose .
Mmea huu katika Tanzania hupatikana katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Njombe, Iringa, Morogoro, Tanga, Tabora, Singida, Mwanza, Kagera, Shinyanga,   Dodoma , Kilimanjaro  na Arusha. Mmea huu hutibu magonjwa mbalimbali kama ugumba kwa wanawake,  matatizo ya udhaifu wa mwili, rheumatism, kifua kikuu ukichanganya na pilipili manga na asali,  kukosa usingizi, kikohozi na baridi,  matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji chakula,  kukosa hamu ya kula chakula,  kuumwa vidonda vya tumbo (gastric ulcer) , hurahisisha utokaji wa mkojo vizuri,  hutibu baadhi  ya magonjwa ya ngozi, majipu, kuvimba mikono na miguu, kuua chawa mwilini , matatizo ya macho (sore eyes ) kuimarisha nguvu za uzazi (hasa kwa wale wanaowahi  tendo la ndoa) na kutibu maumivu baada ya kujifungua.
Matunda yake yanapendwa sana na baadhi ya ndege  na watu wengine hupanda kama  maua majumbani mwao .
TAHADHARI.
Wajawazito wasitumie inaweza kuharibu mimba .
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com





No comments:

Post a Comment