Pages

Sunday, August 24, 2014

MIUJIZA YA AMARANTHUS TRICOLOR




Mchicha wa aina ya amaranthus tricolor L au Amaranthus Gangeticus ni mchicha unaoota sehemu mbalimbali katika nchi yetu. Lakini watu wengi hawautumii labda kwa kutojua faida zake kwa mwili wa binadamu. Mchicha huu ni mwekundu unafanana na mchicha nafaka (grain amaranth). Mchicha huu asili yake ni America kusini (Mexico). Hadi sasa mmea huu umekuwa ukisambaa duniani kote maeneo ya kitropiki na nusu tropiki.
Nchini Indonesia mchicha hulimwa mwaka mzima na hupatikana katika mwinuko wa mita 5 Mpaka 2000 juu ya usawa wa bahari; unalimwa kwenye baridi na joto zaidi unalimwa kwenye rutuba katika maeneo ya chini kwenye eneo la wazi `ambapo hewa na joto ni la kiasi.
Kuna jamii tatu za michicha ambazo ni amaranthus tricolor iitwayo mchicha wa kijani  cha kawaida, Red amaranth ( Blitum rubrum) ambayo shina lake na majani ni mekundu na tatu ni white amaranth (Blitum album) ya kijani nyeupe. Kwenye mchicha huu vinavyotumika ni majani, mizizi na mbegu. Kwenye mchicha huu kuna vitamin A,B,B2,, C, calcium, chuma, magnesium, Phosphorus, Sodium, Potassium, na salfa( sulphur). Pia kuna protini, nyuzinyuzi, wanga na mafuta kidogo. Mchicha huu unatibu magonjwa  kutokuona usiku, mtoto  wa jicho (cataract), bronchitis, asthma, emphysema, kifua kikuu (TB), kufunga choo, kuimarisha fizi, pua, mapafu, kukuza watoto, wakina mama, wajawazito na kuongeza utokaji wamaziwa vizuri, kufunga kuharisha, leucorrhoea, menorrhoagia, uhanithi, kutibu sehemu zenye maumivu na mbegu zake huimarisha nguvu uzazi na uhanithi (impotence).
Watanzania tuanze kutumia mchicha huu kwa faida ya afya zetu.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 


Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com



No comments:

Post a Comment