Licha
ya kusambaa kwa mmea huu takribani sehemu nyingi ulimwenguni.Pia uliitwa majina
mengi Adenolepis Spp na campylotheca Spp. Wachina huiita Gui zhen, Wahispania huiita aceitilla
au moriseco, USA huiita beggars tick, Spanish needle au needle grass, India
huita Ottrancedi, Nchi za kusini mwa afrika huita Uqadoro, Afrika Kusini huita
black jack na Brazil huita picao preto au cuamba.
Mmea huu umesambaa takribani kila kona ya
Tanzania na kujipatia umarufu wa kushona nguo (kishona nguo) Wanyakyusa huiita
matatila, Wandari huiita Ukapunika , Wameru huiita Manyungunyungu, Wairaqu QALMIR
BO. Pamoja na uwezo wake wa ulinzi wa kiafya ukiwemo ule uwezo wa kuongeza na
kusafisha damu kwa kasi kuliko hata mchicha, sio jambo la kushangaza. Mtanzania
ambaye nyuma ya nyumba yake kuna vishona Kishona nguo akapatikana ana upungufu
wa damu.
Majani
yake hutumika kamatiba ya maradhi mengi , yakiwemo Malaria, Sickle cell, Kisukari,
Macho yenye ukungu Shida ya kukojoa kitandani,Vidonda vibichi Vidonda vya tumbo
,Tumbo kuuma, huangamiza minyoo, Hutibu homa ya vipindi kwa watoto,Gesi
tumboni, Colds and flue, Chronic hepatitis, na Mambukizi ya njia ya mkojo (UTI)
nk.
Maua
yake yakikaushwa na kusagwa kuwa unga huufaa sana kwa kipodozi cha asili kwani
huondoa chunusi na kulainisha ngozi.
Mmea
huu umekuwa ukiwasaidia sana watu wenye kisukari hasa pale unapochanganya na
mchunga (Dandelion) na kula kama mboga mala 1 au mbili kwa siku. Huongeza damu
kwa kasi sana ikitumika kama chai ama kama mboga. Pia hutumika kwa watu wenye
shinikizo la damu la chini. Kwa kutumia majani mabichi ama yale yaliokaushwa
vizuri hasa yaliyo kaukia kivulini yafaa sana kwa chai kuliko majani ya chai ya
viwandani ambayo yana aina Fulani ya sumu iitwayo thain.
Husaidia
kuondoa sumu mwilini hasa zile zilizo ambatanana na chakula kwa kulisaidia ini,
pamoja na Figo ndio maana inapotumika pamoja na mchunga (Tumbaku ya wazuka)
huleta manufaa mwilini.
Huondoa
tatizo la kufanya choo pamoja na kupunguza uwezekano wakupata saratani ya
utumbo mpana na bawasili (Haemorrhoids). Huondoa tatizo la kufunga choo kwa
watoto na homa, na malaria kwa matumizi ya maji yaliyochemshwa. Pamoja na
mizizi nusu kikombe cha chai kwa muda wa siku tano. Pia huleta hamu ya kula.
Ukichanganya
na mchunga (tumbaku ya wazuka) husaidia
sana wanawake wenye hedhi zisizo na mpangilio.Mizizi yake ni bora sana kwa tiba
ya malaria na huweza kuondoo tatizo la
kufunga choo.
Mmea
mzima hutumika kutibu tonsihitis, Canker sores, kuoshea mdomo na kuongeza
maziwa kwa akina mama. Pia ni chakula kwani majani yake machanga yanaweza
kuliwa mabichi au yakiwa yameokwa lakini yana radha ya uchungu. Huko Zimbabwe
majani yanachemshwa na kuungwa na siagi ya karanga na kuliwa na vyakula
vingine. Nchi nyingi za kiafrika zinakula mboga ya majani ya Bidens Pilosa.
Tahadhali.
Usitumie
kwa wingi sana inaweza kusababisha kuwasha kwa Figo na bladder.
Ukifanya jitihada za kututembelea
ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid),
Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy),
mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya
mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya
kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea),
kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini
(Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi
(vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo
ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa
baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na
kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira
Natural Products
Mbeya
Simu;
+255 754 807401, +255 719 564276
Blogu:
mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment