Komfrey
ni mmea uishio miaka mingi. Ina umuhimu kwa mboga zenye afya kwa familia, pia
malisho bora kwa wanyama wengi. Majani ya mmea huu huweza kutengenezwa mbolea
kwa ajili ya bustani.
Russian
Comfrey-Symphytum Peregrinum au Officinale) ni mmea uliopatikana katika mapori
ya milima ya Kaukasus-Urusi. Pengine ndio maana ukapewa jina la Russian Comfrey.
Mmea huu ulipelekwa uingereza-ulaya katika karne iliyopita na kutoka Uingereza
ulisambazwa Canada, Amerika, Australia, New Zealand na Afrika.
Waingereza
ndio walioleta hapa Afrika ya Mashariki. Mmea huu hupandwa zaidi katika mikoa
ya Ruvuma,Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa n.k. Mmea huu haufai
kupandwa katika nyanda za upepo wenye joto au sehemu zenye joto ukanda wa
Pwani. Hii ndiyo sababu Comfrey inaweza kupandwa katika kivuli cha upenu wa
nyumba au miti. Na watu wengine hupenda kuuita mboga tumbaku kwa sababu majani
yake yanafanana na ya tumbaku.
Comfrey
ni mmea ujengao Protini upesi zaidi kuliko mimea mingine iliyopo. Zaidi ya
protin una viini muhimu vya vitamin na hasa kiasi cha juu zaidi cha vitamin B12
ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa seli mwilini.
Kwa
maana hii mmea huu unafaa sana kutumiwa na wenye matatizo ya Sickle Cell, Sickle
Cell hushambulia chembechembe za damu. Pia kwa kiasi ni ugonjwa wa kurithi.
Sehemu zenye ugonjwa wa Malaria kwa wingi ndio huathirika zaidi. Unatumia
majani, na pia unaweza kuchanganya na mchicha, Chinese, Swiss Chard au mboga za
maboga. Mchanganyiko huu ni muhimu sana katika kupambana na matatizo ya Sickle
Cell. Unga wa majani uliokaushwa kwa kaushio la jua (Solar driers) ni muhimu kwa
kuongeza protini ndani ya vyakula mbalimbali kama supu, mchuzi wa mboga
(ugali), uji n.k
Pia
majani mabichi au yaliyoanikwa unaweza kutumia kwa chai kwa kuongeza asali/
sukari, utaboresha afya yako kwa kinywaji hiki.
Magonjwa
mengine yanayoponywa kwa kutumia Comfrey ni jeraha, michubuko ni uvimbe wa
miguu na mikono. Majani na mizizi ndivyo vinavyotumika kutengeneza dawa.
Comfrey ni malisho muhimu kuwakilisha samaki na
wanyama. Ni malisho bora kwa wanyama wenye tumbo moja kama kuku n.k kwa sababu
ina nyuzi kidogo zaidi kuliko mimea mingine. Inasaidia kujenga mifupa. Kwa
ng’ombe wa maziwa hutoa maziwa mengi. Comfrey kwa mbolea (hupata potashi
kufunika udongo kwa majani ya Comfrey (Mulching) hasa kwa nyanya na viazi.
Ni
vizuri zile sehemu ambazo unastawi wananchi wakachangamkia na kuupanda ili
kupata faida zake.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Matatizo ya
meno, Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi
tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni
pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi
wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo
ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka
moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na
mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
No comments:
Post a Comment