Nettle
ni majani ya mimea ya upupu. Ni familia ya urticaceae. Wanyakyusa huita
indandye na waingereza huita stinging nettle. Nettle ni mmea unaopatikana
mashambani na porini wenye manyoya ya kujikinga aina ya vijimwiba. Hupandwa pia
katika bustani za miche. Hupandwa pia katika bustani za miche.
Wakulima
na wafugaji huwa hawapendi mmea huu kwa sababu ukigusana na ngozi ya mwili
huwasha sana. Lakini nafikiri hawaupendi
kwa kutojua faida zake laiti wangejua faida zake wangeheshimu sana.
Ni
mmea unaoweza kukua kwa meta moja hadi tano kutegemea mazingira yaliyopo.
Sehemu inayotumika ni majani na mizizi. Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia
wajerumani walikuwa na upungufu wa pamba katika kutengeneza nguo ndipo
walipotumia kamba ya nettle kutengeneza nguo. Pia askari wa roma wakati wa
baridi walitumia nettle ili kuleta joto mwilini kwa kile kitendo chake cha
kuwasha pale unapogusa mwili.
Nettle
hutibu kusafisha damu, figo, minyoo, kuhara damu, baridi ya bisi, tezi la
shingoni (goita), homa , kuumwa mgongo,
kusafisha njia ya mkojo, kuongeza damu, dawa ya kikohozi, hutibu maumivu , tonic
ya nywele, pumu, kutoka damu puani na mdomoni, kuondoa takataka zisizofaa
mwilini, kuhara, kutoa makohozi mapafuni, kuondoa mawe ya kwenye kibofu,
uterine hemorrhages, kutibu magonjwa ya ngozi, kuondoa mba kichwani na kufanya
nywele kuwa imara jongo(gout) HBP( high blood pressure), hay fever, matatizo ya
hedhi, kulainisha ngozi ya mwili, na ni
nzuri kwa maradhi yote ya mzio(allergy) nk.
TAHADHARI
Usile
majani mabichi yanaweza kuharibu figo. Majani yaliyopikwa ni lishe nzuri na
husaidia utokaji wa mkojo. Majani mabichi yavunwe ukiwa umevaa glavu(Gloves),
shati la mikono mirefu na suruali kwa maana
yakishikwa yanawasha sana.
Na
usiwape watoto chini ya miaka miwili bila ushauri wa daktari. Na kwa vijana wadogo wa kuanzia miaka 65 na
kuendelea waanze dozi na dozi ndogo na kuendelea kuwa kubwa.
Ni
vizuri tuanze kulima, kuilinda na kuihifadhi Nettle.
Ukifanya
jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo
homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito(
Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya
ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali
ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali
wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi
(Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa
hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,
vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine
mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na
kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa
nalo na anahitaji tiba ipi.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Blogu: mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment