Pages

Saturday, September 6, 2014

UJUE MNAVU (SOLANUM NIGRUM)



Mnavu ni mboga inayopendwa sana na kabila la wasafwa mkoani mbeya na huita isungwe kwa tafsiri rahisi. Wasafwa wanajua manufaa ya kula mboga hii, waingereza huita Black nightshade, Sun berry, Wonder cherry, Deadly nightshade na wahindi  huita makoy au manathakkal.
Na asili ya mnavu ni Afrika magharibi lakini sasa imeenea ulimwenguni pote. Na kwa sasa kuna aina mbalimbali zinazotumika hapa Tanzania ile inayoota porini  na nayolimwa katika bustani zetu. Aina ya kwanza Matunda kabla hayajakomaa huwa na rangi kijani na madogo na yakikomaa huwa na rangi ya njano. Mnavu mwingine huwa na matunda makubwa ya kijani na yakishakomaa huwa na rangi ya Zambarau nyeusi. Kwenye mnavu kuna maji, protini, mafuta, wanga, nyuzinyuzi, jivu, calcium,phosphorus, iron, thiamine (B1), ribopflavin(B2), niacin (B6) na vitamin C. Na majani yake yana uchungu lakini yakipikwa uchungu hupungua kidogo. Mnavu hutumika matunda na mmea wote. Mnavu una faida nyingi za kiafya kama kuleta hamu ya chakula, homa, matatizo ya tumbo, asthma, dropsy, kuondoa kuvimbiwa, vidonda vya tumbo(peptic ulcers), colitis, kuhara damu, magonjwa ya ngozi kama acne, eczema na psoriasis nk. Baridi yabisi, Jongo(gout) uvimbe wa korodani(kende), majipu na tezi  zilizovimba. Majani yake ni mboga nzuri sana na unaweza kuchanganya na mboga nyingine na mboga jamii za mikunde. Juisi ya mnavu unaweza kuchanganya kiasi na maji ya nazi, tui la nazi, butter milk, maziwa ya ng’ombe na juisi ya matunda.
Watanzania tuanze kuchangamkia kulima mnavu ili tupate faida zake katika mwili.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


No comments:

Post a Comment