Pages

Wednesday, April 6, 2016

MUUJIZA WA ASPARAGUS OFFICINALIS.

Mmea huu umekuwa ukilimwa na kustawi sehemu mbalimbali huko ulaya sehemu zenye udongo wa kichanga . Na pia hustawi India, china, Taiwan, Africa na Malaysia . Jina la kitaalamu huitwa chlorophytum borivianum na India shatawar au sootmuli .Na waingereza huita Asparagus. Majani yake huliwa na mizizi yake hutumika kwa dawa .Na hapa Tanzania hupatikana mikoa ya Iringa, Njombe, Dar es salaam na Arusha nk. kwenye asparagus officinalis kuna Protin, mafuta kidogo, nyuzinyuzi, kabohidreti, calcium, phosphorus, magnesium, chuma, vitamin A, Vitamin B-comprex kiasi na vitamin C,
Mizizi(rhizome) yake hufaa  sana kwa wenye matatizo ya moyo uliyotanuka na udhaifu wa moyo . Na ni chakula kinachofaa kwa moyo kikichanganywa na asali.
Na mizizi ya asparagus imekuwa ikitumiwa  katika dawa za Aryuvelda  huko India kwa siku nyingi Kuamsha tendo la ndoa. Asparagus ina mchango mkubwa wa kuchochea homoni za kijinsia hivyo huamsha na kuongeza hisia za nguvu za kike na kiume . kwa sasa kumekuwa na mahitaji makubwa huko mashariki ya kati na ulaya.Dawa hiyo huuzwa kwa kutumia jina la safed musli huuzwa ghali.  Na huongeza ukubwa na uwezo kutanua misuli mirefu na unene wa utupu kama unatumiwa mara kwa mara kwa wanaume. Na kupunguza matatizo ya uhanithi (impotency). Uwepo wa saponins na alkaloids ndizo zinazo ongeza nguvu za uzazi.
Tahadhari.
Watu walio na matatizo ya mawe kwenye figo, cystitis, kisukari, Nephritis au jongo(gout) wasitumie mpaka watibu matatizo waliyonayo.
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

PILIPILI RAFIKI WA MOYO WA BINADAMU

Pilipili hulimwa sehemu nyingi ulimwenguni. Pilipili ziko za aina nyingi ulimwenguni kama Pilipili Kichaa, Pilipili Mbuzi, Paprika, capsicum, Bell pepper, Capsicum Frutescens na cayenne pepper nk. Kwa leo nitaelezea pilipili ya cayenne pepper.
Jina la kibotania huitwa Capsicum Anuum, Waingereza huita cayenne pepper.
Cayenne peppers ina vitamini A,B,C,E,  Betacarotene, Chuma, Phosphorus, Calcium, Thiamine, Riboflavin na Niacin nk.
Pilipili aina hii wengi hutumia kama kiungo katika mapishi yao mbalimbali. Pilipili ina kimeng’enyo aina ya Capsaicin ambacho kina manufaa makubwa kwa mwili wa binadamu.
Watu wa mashariki ya mbali kama India,Thailand nk hutumia sana pilipili katika vyakula vyao na ni mara chache sana hushambuliwa na matatizo ya moyo. Pilipili hii ikitumika vizuri huzuia kushambuliwa kwa Moyo na kufanya usipate na HBP na hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi. Pilipili hutibu vidonda vya tumbo japo watu wengi huona kama inaleta vidonda vya tumbo. Inapotumiwa na wenye vidonda vya tumbo mwanzoni tumbo huuma sana lakini kadri unavyoendelea kutumia tumbo huacha kuuma. Pilipili hutibu maummivu ya viungo    (baridi ya yabisi) rheumatism, kuteguka, maumivu ya misuri, kuvimba kwa viungo (arthritis) maumivu ya kiuno, na kuuma kwa mshipa wa nyuma ya paja. Twanga kijiko kimoja kikubwa cha pilipili mbichi au kavu na kijiko kimoja kikubwa cha mafuta ya mawese. Mchue mgonjwa kwa mchanganyiko huu kwa nguvu sana hadi asikie maumivu.Na uendelee kuviweka viungo katika hali ya joto. Tumbo kujaa hewa na bawasiri ongeza pilipili katika chakula chako. Kisukari cha miguu tumia kama maumivu ya viungo , lakini tibu miguu kwa uangalifu isichubue ngozi. Magonjwa ya ngozi na mkanda wa jeshi (herpers zoster) hutumia mafuta ya mawese yaliochanganywa na pilipili kwa kiasi ambacho mgonjwa atakuwa bado anauwezo wa kuvumilia maumivu.
Pilipili hutibu Arteriosclerosis, Asthma, Bronchitis, Mafusa, Kikohozi, kutosagika vizuri kwa chakula, Homa ya manjano, Bandama, Figo, Pancreas, Flu, na Varicose veins.
Tumia kijiko cha chai cha pilipili weka kwenye kikombe cha maji yaliyochemka. Kunywa nusu kikombe mara tatu kwa siku mpaka mgonjwa apone.
Kutibu vidonda weka unga wa pilipili juu ya vidonda
Pilipili hutumika kutengeneza sosi ya pilipili nk.

Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na wanobabuka na jua kama Albino (Herbal sunscreen oil) na Tiba. 
Mazingira Natural Products
Simu: +225 754 807401-0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com

NUMBU HULETA HAMU YA KULA

Numbu ni zao linalopatikana katika nchi za Tropiki.Hapa Tanzania hupatikana katika mikoa ya Mbeya na Njombe.Na zipo numbu aina zaidi ya tatu.Zipo zinazoliwa mbichi na zinazopikwa.Jina la kibotania huitwa plectranthus esculents.Waingereza huita Livingstone potato.Wasafwa huita numbu.Wanyakyusa huita Njobela.Pia numbu hupatikana nchini Malawi.Hapa Mbeya hupatikana numbu zinazoliwa mbichi na Njombe hupatikana za kupika kama viazi.Wasafwa hula sana numbu kuliko makabila mengine.Kabla ya kuandika makala hii nimefanya utafiti wa kuwahoji baadhi ya watu wanaozifahamu numbu vizuri.Baadhi ya watu hao ni Richard Mbwello, Ngimba Joseph, Sinaida Mwamaso na Nerbat Mngoni wote walitoa maelezo yanayofanana kuhusu matumizi ya numbu.
Moja ya jambo la kushangaza kuhusu numbu kabila la Wasafwa mtu akiwa mgonjwa humpatia numbu ale na mgonjwa akikataa kula numbu hupata mashaka ya kupona maradhi yanayomkabili.Kwa lugha rahisi husema mgonjwa atakufa.Numbu ukila huleta hamu ya chakula, numbu zina vitaminiA, wanga na madini kwa hiyo hufaa sana wakati wa upungufu wa chakula,Huongeza maji mwilini,Huimarisha mifupa,Hupunguza Homa,Hushusha mapigo ya juu ya moyo,Numbu zina ubaridi kwa hiyo zinafaa sana kuliwa wakati wa jua kali ili kutuliza kiu cha maji,
 Numbu hufaa sana kwa wenye matatizo ya usagaji wa chakula tumboni,pumu,bronchitis,numbu hutibu minyoo tumboni na majani yake unaweza kujisugua mwilini na kuondoa harufu mbaya ya ngozi.
Umefika wakati wa Watanzania kulima mazao yasiyopewa kipaumbele kama numbu kwani nazo zina faida kiafya.
Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na wanobabuka na jua kama Albino (Herbal sunscreen oil)
na Tiba. 
Mazingira Natural Products
Mbeya.
Simu: +225 754 807401-0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com

NGENGELE ZAO LILILOSAHAURIKA

Tumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutufikisha mwaka 2016 salama na wale ambao wametangulia mbele za haki mungu awapumzishe salama.
Nimeamua kuandika makala hii baada ya kutoka safarini wilayani RUNGWE. Wakati wa matembezi yangu niliona mmea ninaoufahamu umepandwa kwa mzee mmoja wa kinyakyusa.
Nikakumbuka kuwa hata mimi nimepanda nyumbani kwangu Mbeya. Ikabidi nimwone huyo mzee ili niweze kupata maelezo ya mmea huo na akanikaribisha.
Nikajitambulisha mimi ni nani na natoka wapi. Na yeye akajitambulisha yeye ni nani. Ndipo nilipomweleza shida yangu iliyonipeleka kwake. Yule mzee aliniambia kuwa ule mmea ameurithi kutoka Kwa baba yake mzazi. Akanieleza kuwa miaka zaidi ya 50 njaa iliwahi kutokea unyakyusani na viazi hivyo viliwaokoa wakati wa njaa. Na akaniambia kwamba mzee wake alisema kamwe asiupoteze maishani mwake. Mmea huu kwa kibotania huitwa Dioscorea bulbifera. Waingereza huita Air potato au Bitter yam, Wanyakyusa huita ngengele. Na husitawi kwa mtindo wa kutambaa kwenye miti kama chayote au pesheni.
Na inaweza kukua inchi 8 kwa siku na wastani kufikia futi 60.Na huweza kufika futi 150 kwa urefu kufuatana na eneo lilivyo rafiki na mmea wenyewe. kuna aina zingine ni chungu na haziliwi. Dioscorea bulbifera na Dioscorea Deltoidea ndio huliwa. Lengo langu kubwa ni kwa watanzania kuanza kufufua mazao yaliyokuwa yakilimwa na mababu zetu na kutumiwa kwa chakula lakini yameachwa kwa sababu ya kwenda na wakati.
Huko Kenya kabila la Tiriki wanaita marugu (Dioscorea bulbifera) wanasema ni chakula bora kuliko mkate wa ngano mweupe.Wanasema wakila marugu hukaa muda mrefu tumboni bila kusikia njaa. Hapa Tanzania tunatakiwa tuendeleze zao hili na yale mengine ambayo hayatiliwi maanani.
Dioscorea bulbifera ina flavonoids na isoflavonoids vitu ambavyo ni muhimu kwa afya zetu.
Ngengele huzuia/ hutibu kuharisha, kuhara damu, Homa ya manjano, maumivu ya tumbo, Anorexia, conjunctivitis, na mzio unaosababishwa na kuumwa na wadudu kama spider na whip spider. Wenzetu wahindi na wachina hutumia kutibu maumivu ya koo, saratani ya tumbo na goita. Wapangwa wa Ludewa huita Ing’ing’i hutumia kuondoa matego kwa watu waliofanyiwa hivyo. Wanyakyusa hula baada ya kuvichemsha au kuviweka kwenye majivu ya moto mpaka vikaiva. Aina ya Dioscorea deltoidea huliwa na wale wanaotaka kuwa mabaunsa (body-builders) na wale wanaotaka kuongeza Testosterone mwilini.
                                          ANGALIZO
Kuna aina nyingi za Ngengele zingine ni chungu unapokula, kwa hiyo hakikisha unatumia zile ambazo zinafaa kuliwa. Ngengele haziko kundi moja na viazi vitamu.

MIUJIZA YA MATANGO

Matango ni mboga inayopendwa   sana na kulimwa kwa wingi ulimwenguni. Na hutumiwa sana wakati  wa joto la kiangazi kwa kupooza mwili kutokana na joto na kuondoa kiu ya maji. Kuna aina ya matango American slicer,European cucumber na Gherkins nk. Jina la jumla la kibotania huitwa  cucumis sativus. Waingereza huita cucumber. Na asili ya matango ni India na huita kheera/sukasa na yalikuja kujulikana misri, Ugiriki, Roma na China miaka mingi iliyopita. Sasa hivi yameenea kote ulimwenguni. Yanalimwa kwa wingi  India, Pakistani, china, America na nchi nyingine nyingi. Tanzania pia tunalima na kuyatumia.
Matango yana vitamini B,C,K,Calcium, Phosphorus,Chuma,Shaba,Potassium,Sodium,Manganese,Magnesium,Sulphur,Silicon,Chloline na Fluorine nk.
Kula matango mara kwa mara husaidia kulinda ubongo kuwa na afya njema, kuzuia uwezekano wa kupata saratani kwa kuwa matango yana polyphenols inayoitwa lignans inayopunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti, Uterine,Ovarian na tezi dume. Matango yanapigana na muwako wa mwili (unaowasha au kuchoma). Matango yanazuia Oxidant, matango hudhibiti msongo wa mawazo kwa kuwa yana vitamini B1, B5 na B7 (biotin) Zinazopunguza mtu kuwa na wasiwasi na kuzuia nguvu ya kipigo cha msongo wa mawazo. Matango  yakiliwa hufanya moyo uwe na afya njema kwa kuwa yana potassium inayopunguza shinikizo la damu. Matango yanasaidia umeng’enywaji wa chakula vizuri tumboni.Vidonda vya tumbo na majipu. Ukiumwa na mdudu kata slesi ya tango na bandika penye tatizo. Huongeza utokaji wa mkojo na kufanya bandama liwe na afya njema, Tumbo na utumbo mkubwa kuwa na afya njema. Matango yanapoliwa husafisha damu na kuzuia magonjwa ya ngozi. Matango yakiliwa na ganda lake huzuia mawe ya kwenye figo. Yanaondoa uric asidi katika mwili unapoyala matango. Matango yanaondoa au kuzuia magonjwa ya Ini,Figo na Koo. Wenye kisukari na kupunguza uzito wa mwili watumie matango kuwa sehemu ya mlo wao. Matango husimamisha kichefuchefu na kutapika. Matango husaidia kipindupindu unatengeneza glasi moja la juisi ya tango na unachanganya na maji ya nazi(dafu) unakunywa kila baada ya saa moja inaleta matokeo mazuri kwa mtumiaji. Inaondoa baridi yabisi (Rheumatism) kuvimba miguu kwa kuchanganya na juisi ya karoti na Beetroot. Hutumiwa kuleta uzuri wa ngozi sugulia uso na kipande cha tango.Osha uso na juisi (maji yake utaona matokeo mazuri baada ya wiki moja). Pia matango hutengeneza saladi kwa kuchanganya na Karoti, Nyanya, Radishi, Kabeji na maziwa ya mgando.
                  ANGALIZO
Vitamini na madini mengi yapo kwenye Ngozi kwa hiyo unapotumia usitoe maganda ingawa mengine ni machungu kidogo ikiliwa na maganda lakini bado hufaa zaidi.
Pia matango aina ya American Slicer na European cucumber hufaa kwa tiba na saladi.
Matango aina ya Gherkins hufaa kwa tiba na Achali.