Matango ni mboga inayopendwa sana na kulimwa kwa wingi ulimwenguni. Na
hutumiwa sana wakati wa joto la kiangazi
kwa kupooza mwili kutokana na joto na kuondoa kiu ya maji. Kuna aina ya matango
American slicer,European cucumber na Gherkins nk. Jina la jumla la kibotania
huitwa cucumis sativus. Waingereza huita
cucumber. Na asili ya matango ni India na huita kheera/sukasa na yalikuja
kujulikana misri, Ugiriki, Roma na China miaka mingi iliyopita. Sasa hivi
yameenea kote ulimwenguni. Yanalimwa kwa wingi
India, Pakistani, china, America na nchi nyingine nyingi. Tanzania pia
tunalima na kuyatumia.
Matango yana vitamini B,C,K,Calcium, Phosphorus,Chuma,Shaba,Potassium,Sodium,Manganese,Magnesium,Sulphur,Silicon,Chloline
na Fluorine nk.
Kula matango mara kwa mara husaidia kulinda ubongo
kuwa na afya njema, kuzuia uwezekano wa kupata saratani kwa kuwa matango yana
polyphenols inayoitwa lignans inayopunguza uwezekano wa kupata saratani ya
matiti, Uterine,Ovarian na tezi dume. Matango yanapigana na muwako wa mwili
(unaowasha au kuchoma). Matango yanazuia Oxidant, matango hudhibiti msongo wa
mawazo kwa kuwa yana vitamini B1, B5 na B7 (biotin) Zinazopunguza mtu kuwa na
wasiwasi na kuzuia nguvu ya kipigo cha msongo wa mawazo. Matango yakiliwa hufanya moyo uwe na afya njema kwa
kuwa yana potassium inayopunguza shinikizo la damu. Matango yanasaidia
umeng’enywaji wa chakula vizuri tumboni.Vidonda vya tumbo na majipu. Ukiumwa na
mdudu kata slesi ya tango na bandika penye tatizo. Huongeza utokaji wa mkojo na
kufanya bandama liwe na afya njema, Tumbo na utumbo mkubwa kuwa na afya njema.
Matango yanapoliwa husafisha damu na kuzuia magonjwa ya ngozi. Matango yakiliwa
na ganda lake huzuia mawe ya kwenye figo. Yanaondoa uric asidi katika mwili
unapoyala matango. Matango yanaondoa au kuzuia magonjwa ya Ini,Figo na Koo.
Wenye kisukari na kupunguza uzito wa mwili watumie matango kuwa sehemu ya mlo
wao. Matango husimamisha kichefuchefu na kutapika. Matango husaidia
kipindupindu unatengeneza glasi moja la juisi ya tango na unachanganya na maji
ya nazi(dafu) unakunywa kila baada ya saa moja inaleta matokeo mazuri kwa mtumiaji.
Inaondoa baridi yabisi (Rheumatism) kuvimba miguu kwa kuchanganya na juisi ya
karoti na Beetroot. Hutumiwa kuleta uzuri wa ngozi sugulia uso na kipande cha
tango.Osha uso na juisi (maji yake utaona matokeo mazuri baada ya wiki moja).
Pia matango hutengeneza saladi kwa kuchanganya na Karoti, Nyanya, Radishi,
Kabeji na maziwa ya mgando.
ANGALIZO
Vitamini
na madini mengi yapo kwenye Ngozi kwa hiyo unapotumia usitoe maganda ingawa
mengine ni machungu kidogo ikiliwa na maganda lakini bado hufaa zaidi.
Pia
matango aina ya American Slicer na European cucumber hufaa kwa tiba na saladi.
Matango
aina ya Gherkins hufaa kwa tiba na Achali.
No comments:
Post a Comment