Pages

Wednesday, April 6, 2016

NUMBU HULETA HAMU YA KULA

Numbu ni zao linalopatikana katika nchi za Tropiki.Hapa Tanzania hupatikana katika mikoa ya Mbeya na Njombe.Na zipo numbu aina zaidi ya tatu.Zipo zinazoliwa mbichi na zinazopikwa.Jina la kibotania huitwa plectranthus esculents.Waingereza huita Livingstone potato.Wasafwa huita numbu.Wanyakyusa huita Njobela.Pia numbu hupatikana nchini Malawi.Hapa Mbeya hupatikana numbu zinazoliwa mbichi na Njombe hupatikana za kupika kama viazi.Wasafwa hula sana numbu kuliko makabila mengine.Kabla ya kuandika makala hii nimefanya utafiti wa kuwahoji baadhi ya watu wanaozifahamu numbu vizuri.Baadhi ya watu hao ni Richard Mbwello, Ngimba Joseph, Sinaida Mwamaso na Nerbat Mngoni wote walitoa maelezo yanayofanana kuhusu matumizi ya numbu.
Moja ya jambo la kushangaza kuhusu numbu kabila la Wasafwa mtu akiwa mgonjwa humpatia numbu ale na mgonjwa akikataa kula numbu hupata mashaka ya kupona maradhi yanayomkabili.Kwa lugha rahisi husema mgonjwa atakufa.Numbu ukila huleta hamu ya chakula, numbu zina vitaminiA, wanga na madini kwa hiyo hufaa sana wakati wa upungufu wa chakula,Huongeza maji mwilini,Huimarisha mifupa,Hupunguza Homa,Hushusha mapigo ya juu ya moyo,Numbu zina ubaridi kwa hiyo zinafaa sana kuliwa wakati wa jua kali ili kutuliza kiu cha maji,
 Numbu hufaa sana kwa wenye matatizo ya usagaji wa chakula tumboni,pumu,bronchitis,numbu hutibu minyoo tumboni na majani yake unaweza kujisugua mwilini na kuondoa harufu mbaya ya ngozi.
Umefika wakati wa Watanzania kulima mazao yasiyopewa kipaumbele kama numbu kwani nazo zina faida kiafya.
Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na wanobabuka na jua kama Albino (Herbal sunscreen oil)
na Tiba. 
Mazingira Natural Products
Mbeya.
Simu: +225 754 807401-0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com

No comments:

Post a Comment