Mchaichai hupandwa sehemu nyingi Tanzania. Mchaichai
hupandwa sehenu yenye rutuba na tifutifu na kwenye kivuli kidogo.
Gawanya mmea ulio stawi na kupanda.Majani hufikia hadi sm 50
urefu. Mwagilia Maji vizuri katika hatua ya awali. Jina la kibotania huitwa
cymbopogon citrates. Waingereza huita lemon grass, barbed wire grass, silky
heads, citronella grass, fever grass. Michaichai haihitaji uangalizi wa hali ya
juu, na bora ikapandwa katika kila bustani, Zahanati na hospitali. Mchaichai
hutibu maumivu makali wakati wa hedhi kwa kuchanganya na pilipili manga, shida
ya umeng’enyaji wa chakula tumboni, homa kwa kushusha joto la mwili, huzuia na kutibu
mkazo wa msuli, kutibu ringworm, kutibu baridi yabisi, maumivu ya kiuno Neuralgia,
kuteguka unachanganya mafuta ya mchaichai na mafuta ya nazi na kuchua sehemu
iliyo athirika. Kama maumivu yanaendelea tumia mafuta ya mchachai tu bila
kuchanganya na ya Nazi, vilevile husaidia kwa maumivu ya meno, kipindupindu na
tumbo kujaa gesi, pia husaidia kumfanya mtu kukojoa sana , kutapika, kuharisha,
nzuri sana kwa ukosefu wa usingizi, Mchaichai ni mzuri kwa kila mwenye tatizo
la maumivu mbalimbali, pia unatibu magonjwa
yanayopatikana kwa kutumia masufuria ya
aluminium na shinikizo la damu, Bawasiri kwa kuchanganya na majani ya mwembe au
mkaratusi, Malaria na harufu mbaya mdomoni.
Dozi: weka kiganja 1 majani katika maji lita moja 1 yaliochemka,
kwa dakika 15: kunywa nusu kikombe kutwa mara tatu (3) kwa siku.
Matatizo ya kifua, mafua na sinusitis- chemsha kiganja kimoja
(1) cha mchaichai kwenye lita moja ya maji na vuta mvuke wake.
Sehemu nyingine duniani mchaichai hutumika kama kiungo
katika vyakula na kuongeza harufu katika mvinyo.
Mchaichai hutengenezwa mafuta ya watoto na mafuta ya kuchulia,
D away a mafuta kwa ajili ya mwili. Dawa
ya mafuta kwa bawasiri, kutengeneza na sabuni na dawa ya kufukuza wadudu na
nyoka.
Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na wanobabuka na
jua kama Albino (Herbal sunscreen oil) na Tiba.
Mazingira
Natural Products
Simu:
+225 754 807401-0719 564 276
Barua
pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment