Maharage
mmea huu unapatikana karibu kila sehemu duniani,Kuna aina tofauti zaidi ya
500.Leo nitaelezea aina ya maharage ya kijani Haricot vert maana ya maneno haya
hutokana na lugha ya kifaransa.Haricot maana yake maharage na vert ni kijani. Maharage
haya huchumwa yakiwa machanga na kuliwa pamoja na maganda yake.Maharage haya
pamoja na mengine ya kawaida kama kidney beans, Navy beans na black beans nk. Kwa
jina la kibotania huitwa phaseolus vulgaris. Waingereza huita Beans (string
beans) katika nchi nyingine ni mbegu tu zinazoliwa.Lakini maharage mabichi na
maganda yake pia ni chakula chenye thamani. Kwenye maharage ya kijani kuna
vitamin A, C, E, K, vit. B1, B2, B6, nyuzinyuzi, calcium, potassium,
phosphorus, protini,shaba, magnesium, choline,niacin, chuma,folic acid,omega
3fatty acid, chromium na silicon nk.
Maharage
ya kijani ni dawa ya kuongeza mkojo,hufanya moyo kuwa na afya njema kutokana na
kuwa na vitamin A na C kwa wingi,
kuimarisha mifupa na hata wale waliovunjika kwa kuwa yana vitamin K kwa wingi
inayoshughulika na kuimarisha mifupa, maharage ya kijani hufaa kwa wenye
kisukari aina ya 2 kwa kuwa yana nyuzinyuzi nyingi zinazofaa kwa wenye kisukari
kuendelea kuishi maisha ya kawaida, hufanya Colon kuwa na afya njema,
wanaosumbuliwa na Arthritis na pumu wawe wanakula mara kwa mara watapata nafuu,
Eczema, wanaotaka kupunguza uzito wale mara kwa mara haya maharage, wanawake
waja wazito wale mara kwa mara kwa kuwa yana folic acid ya kutosha, hupunguza
lehemu mwilini, hupunguza uwezekano wa kupata kansa ya matiti, hupunguza
matatizo yanayotokana na kukoma kwa hedhi kwa wanawake,Jongo (Gout), maumivu ya
kuvimba kwa viungo (baridi yabisi) na
magonjwa ya figo nk. Kwa wale watakaotumia maharage yaliyo kwenye maganda
yaliyokaushwa gramu 10 hulowekwa katika lita 1 ya maji usiku kucha, halafu
yanachemshwa baadaye yanachujwa. Kunywa wakati wa mchana kwa wagojwa wenye kisukari tiba hii
hupunguza kidogo kiwango cha sukari katika damu.
Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na
wanobabuka na jua kama Albino (Herbal sunscreen oil)
na Tiba.
Mazingira
Natural Products
Mbeya.
Simu: +225 754
807401-0719 564 276
Barua
pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:
mazingiranp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment