Pages

Saturday, May 11, 2013

Mapishi mbalimbali

WALI WA MCHELE NA TUI LA KARANGA

MAHITAJI  : Mchele
                     : Tui la Karanga
                    : Chumvi
                     : Maji

Utayarishaji na mapishi
Ø  Chagua Mchele
Ø  Loweka unga wa Karanga kwa maji safi ya vuguvugu kwa dakika 10
Ø  Kamua tui kwa kutumia maji ya vuguvugu hii inasaidia kutoa tui na lenye mafuta mengi
Ø  Weki tui jikoni linapokaribia kuchemka punguza tui zito la juu na hifadhi vizuri.
Ø  Ongeza mchele, koroga, usifunike. Pika hadi maji yabakie kidogo, halafu funika
Ø  Ongeza tui ulilopunguza (tui zito). Punguza moto kabisa ivisha taratibu ukishakaukia geuza
Ø  Palia kwa dakika 10-15 wali utakuwa tayari

MATUMUZI:-
Kula pamoja na nyama au samaki au maharage na mboga za majani na matunda
¬  Machicha ya karanga yanayoaaaabakia yanaweza kutumika kuungia mboga ya majani au maharage.*

Imeandaliwa na Edgar Kajolo Kapagi           Mbeya
MOBILE: 0754 807401 – 0788 029500

2: UJI WA KIMEA
MAHITAJI:-  Unga wa nafaka ya mahindi au mtama au ulezi iliyooteshwa, kukaushwa
                      na kusagwa.
                   :  Sukari
                   :  Maji
                   :  Chumvi

Utayarishaji na mapishi.
  • Pima unga wa kawaida wa mahindi au mtama
  • Pika uji mzito mpaka uive kabisa
  • Epua, pooza kidogo
  • Ongeza unga wa kimea kiasi cha kijiko kimoja au zaidi kulingana na kiasi cha uji uliopika, endelea kukoroga mpaka uji ulainike.
  • Rudisha tena uji jikonoi chemsha kwa muda  ongeza sukari au chumvi
  • Epua

Matumizi.
Mlishe mtoto kwa kutumia kijiko na kikombe au sahani au bakuli. Pia unaweza kutumika kama kifungua kinywa kwa watoto wa shule na Familia.

Kumbuka : unaweza kuongeza karanga au maharage au mboga za majani au unga wa Soya au yai au maziwa  kuongeza ubora wa uji unga wa kimea unasaidia kulainisha uji wa mtoto na kumfanya anywe kiasi kikubwa kumwezesha kupata viini lishe vya nguvu kwa wingi.

Imeandaliwa na Edgar Kajolo Kapagi            Mbeya
MOBILE: 0754 807401 – 0788 029500

Wednesday, May 8, 2013

MAAJABU YA MTI WA MLONGE (DRUMSTICK)


KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge unaweza kuwa unaongoza. Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.
Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja lijulikanalo kama Trees For Life, majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.
Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma  (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.
Ili kutengeneza ‘tonic’, saga majani mabichi ya Mlonge pamoja na maji, yachuje kisha changanya na maziwa halisi. Inaelezwa kuwa juisi ya aina hii ni dawa nzuri kwa waja wazito, kwani huboresha njia ya uzazi na kumuwezesha mama kuzaa bila matatizo na kuondoa matatizo baada ya kujifungua.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu, baadhi yake ni kama haya yafuatayo:
Mlonge unaweza kutibu Pumu, Kikohozi na Kifua Kikuu. Aidha, magonjwa mengine kama Kisukari, Shinikizo la damu (la juu na chini), magonjwa ya ngozi, magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI) kuongeza kinga ya mwili (CD4) na kuongeza nguvu za kiume.
chanzo; gpl

Kutana na Mtaalamu wa usindikaji, Lishe na Magonjwa mbalimbali

Mazingira Natural Products (MNP) 

wanasema

Bidhaa asili kwa afya thabiti

Karibu Mazingira Natural Products

MAZINGIRA NATURAL PRODUCTS

S.L.P 1338, Mbeya, Tanzania. 

Sae area. Makutano ya barabara kuu ya Zambia na barabara ya Ituha.

Mob: 0754807401 

Nyumba ya Mlonge na Soya


Ni organaizesheni inayojishughulisha na mambo mbalimbali yahusuyo ujasiriamali, usindikaji, kilimo cha uyoga na masuala ya mazingira. Jipatie ushauri mbalimbali kuhusu ujasiriamali, afya ya mwili na vyakula mbalimbali vilivyosindikwa kama vile achali ya embe na uyoga, wine na mvinyo aina zote na za matunda mbalimbali, kilimo cha uyoga, pia wana semina mbalimbali za mafunzo ya ujasiriamali kama utengenezaji sabuni, usindikaji vyakula na kilimo cha uyoga.
Pia ni msambazaji na muuzaji wa bidhaa za Mlonge na Soya. Atakupatia ushauri wa kitaalamu juu ya faida na matumizi ya Mlonge na Soya

KARIBU UPATE HUDUMA BORA KWA PAMOJA TUBORESHE AFYA NA TUUONDOE UMASIKINI