Pages

Friday, September 6, 2013

Maajabu ya Mmea wa Rumex (Sorrel)



)
Maajabu ya Mmea wa Rumex (Sorrel) Usambarensis katika kutibu mkanda wa Jeshi Msemwasemwa (Kinyakyusa), Kchambo (Wapare. Rumex (Sorrel) Usambarensis- Botanic ni mimea inayoota kwa mtindo wa vichaka vichaka inayopatikana katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Njombe, Ruvuma, Iringa na Kilimanjaro n.k mmea huu umeonekana kuwa na faida kubwa sana kwa afya ya binadamu na wanyama, kwa vile hutibu maradhi mbalimbali.
Tafiti mbalimbali zilizowahi kufanyika nchini Tanzania na Kenya  zinaonyesha umuhimu wa mmea huu kutibu magonjwa mbalimbali kwa mfano majani hutibu kikohozi na maumivu ya tumbo.
Mizizi yake na vikonyo vichanga hutumika kutibu kikohozi cha kawaida na Nimonia(Pneumonia), vidonda na majipu.
Pia mizizi yake ikitumiwa na mimea mingine ni dawa ya baadhi ya minyoo inayosumbua sana watu. Pia wazee wa zamani wal;itumia mmea mzima kwa kutibu ndui (Small Pox) kwa kuwaogesha wagonjwa.
Mazingira Natural Products ya Mbeya tumefanya utafiti wa mmea huu ukichanganywa na mimea mingine kama Black Nightshade n.k hutibu vizuri sana mkanda wa Jeshi (Herper Zoster’s) wa aina zote. Na ukitumiwa vizuri huimarisha kinga ya mwili kwa mtumiaji.
Lakini mmea huu hauishii hapo kwa wale wafugaji wa kuku hapa Mbeya wale wanaotumia watakubali bila shaka  yoyote ile kuwa mmea huu unafaa sana kuwalisha kuku hasa wale wanaotaga mayai hufanya kiini kuwa cha njano sana na kupunguza matatizo ya kuku  kudonoana ovyo.
Hili ni muhimu kwa mwananchi yeyote wa Tanzaniania kulifanyia kazi kwa kupanda na kutumia katika mazingira yake.
Imeandaliwa na Mtafiti Dr. Edgar Kajolo Kapagi
Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; 0754 807401, 0719  564276
Barua pepe: mnp.kaka@gmail.com

MAAJABU YA MTI HUU-DRACAENA USAMBARENSIS



 
DRACAENA USAMBARENSIS
(Tetesyeri, Tsheleli-Kisafwa, Msigandi, Mukwanga-Wadigo, Mtetemu-Wamwera)
Dracaena, Usambarensis au Tetesyeri, Tsheleli-kisafwa ni mti unaopatikana katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Ruvuma na Tanga(Lushoto) nk.
            Mti huu umeonekana kuwa na faida kubwa sana kwa afya ya binadamu kwa vile hutibu maradhi mbalimbali. Mti huu umekuwa ukitumiwa na mababu zetu toka siku  nyingi. Mti huu hutumika hata kwenye matambiko mbalimbali kwa mfano kukiwa na uhaba wa mvua wazee wa kisafwa hutumia kutambikia na uhaba wa mvua unatoweka na hata kama yatatokea maradhi ya ajabu ajabu. Pia miti yake hupandwa kuzunguka zizi la ng’ombe kuzuia watu wabaya(wachawi) ili wasiharibu mifugo na watu wengine hupanda majumbani mwao kama maua. Pia watu wengine  hutumia majani yake kumuoshea mtu anayesadikiwa amerogwa. Majani yake hutumika kutoa kondo la nyuma kwa mwanamke aliyetoka kujifungua. Pia majani yake ni dawa ya degedege kwa watoto. Mizizi yake hutibu maumivu ya tumbo hasa linaloandamana na kisonono. Pia mizizi hutumika kwa maumivu ya kifua . Hili ni muhimu kwa kila Mtanzania kulifanyia utafiti zaidi kwani watu wengi wamepanda hasa wenye nyumba za kisasa hata baadhi ya makanisa hutumia kupamba wakati wa sherehe mbali mbali kama maua.  Pia mti huu unatunza mazingira kwenye vyanzo vya maji. Napenda watanzania wenzangu waujue huu mti manufaa yake kwa jamii.
                        Dr Edgar Kajolo Kapagi.
Mazingira Natural Product Mbeya
Simu namba: 0754807401